Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Titicomb, Tusipunguze uwezo WA kufikiri kwa kutawaliwa na hisia mzunguko kama hizi.

Hoja, yake ni yetu pia na inalenga kufungua na kufunga kilichosnzishwa na Chadema, twende sote tuone kama italeta maana endapo yakijibiwa maswali yangu ili yatengeneze modality ya majibu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninyi wapinzani mnamajority ya kupitisha jambo linalichefeua serikali na dola yake?

Hapa ndipo unapojikwaa. Once you start from here as your major premise the conclusion is negative.

Hapa tunajenga hoja ya kuishawishi serikali ione na kukubali uhalali, umuhimu, uharaka na ulazima wa hoja ya kukarabati NEC kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Hili likifanikiwa Mengine yote yanafuata automatically.

Lkn wewe naona uko pessmistic, discouraging and discouraged. Tangu jana unaongea as if tayari umedokezwa na wasemaji wa kambi ya MAGUFULI kuwa hawatakubali hoja ya mageuzi.

Hiyo sio kweli. Bado mwanya wa kuwashawishi upo. Tunasonga mbele.
 

Wapi nimekataa mawazo relevant? Jielekeze ktk hoja plz
 

Paschal mayala hajui maana ya neno uhuru. So maelezo yake yote yako internally incosistent. Kama anataka hoja yake ieleweke basi ahariri bandiko lake nankuondoa dosari hiyo.
 
Mama Amon, Ni kweli ndivyo ninavyoamini.

Lkn naomba nikuulize,
Kwanini tuitake kama hisani badala ya sadaka toka kwa magufuli?

Kwa tunataka kuonewa huruma ili tupewe kama mabadiliko ya katiba tulivyopewa na JK lkn ikafia njia? Hamkujifunza kule nyuma?
Kwa nini usiende kama mswada bungeni ukaomba hizo incremental changes au mahakamani akawa order ya mahakama? Hivyo timu magu wasipotaka watakaa kimya na watendelea kuwa kimya kwa kuwa mbinu mliyotumia si lazima mjibiwe.

Hahahahahahhahahahhahahahhaaha

Tutafute hizi incremental changes hata radical kwa hoja isiyoisha na njia nzuri zenye majibu anuai hata kama hayatapendeza au kutotupa tunachotaka.

Pengine ingependeza, rais anaandikiwa barua, mahakamani inakwenda kesi na bungeni wanapeleka miswada kama kumi kupitia watu tofauti.

Lkn bunge letu halitetei maslahi ya wengi Bali wachache kwa sura ya majority bungeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliwasikiliza kwenye kipindi cha malumbano ya hoja ITV wanasema wako huru wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria
Pia niliwasikiliza kwenye malumbano lkn kwenye kipima joto wakakimbia, wangeweza kujibu maelezo ya kibamba?
Pia hawakupata maswali na mambo yaliyoko hapa ktk huu mjadala hasa paragraph za mwanzo za wachangiaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pengine ingependeza, rais anaandikiwa barua, mahakamani inakwenda kesi na bungeni wanapeleka miswada kama kumi kupitia watu tofauti.

Hili ndilo pendekezo bora zaidi. Nitalisogeza mbele kwa team Mbowe.

Lakini pia, nikishukuru. Umaonekana kuwa mweledi na mzoefu wa mfumo wa utawala hapa TZ.

Nikuulize jambo moja la ufahamu: kwa kuzingatia uzoefu wako wa kitaifa na kimataifa, yamkini ya kufanikiwa kwa muswada binafsi unaopelekwa bungeni ni kubwa au ndogo kiasi gani?
 
Mimi niliwasikiliza kwenye kipindi cha malumbano ya hoja ITV wanasema wako huru wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria

Hapana. Rejea maoni ya kitaasisi yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa NEC kwenye tume ya Warioba kuhusu Katiba Mpya. Mwenyekiti anasema hawako huru.
 
Pascal Mayalla,
Si vibaya na ww Paskali ukaweka maelezo ya kina kuhusu tume kuwa huru lakini sio shirikishi, unapotaka iwe shirikishi unamaanisha iwe na muundo gani. Huu ni uzi muafaka wa ile dhana yako
Tume kuwa shirikishi maana yake wajumbe wake watoke makundi mbalimbali ikiwamo Asasi za kiraia, walemavu, vyama vya Siasa n.k kwa usawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majibu yangu yanategemea majibu yako ya bandiko 201 kwa baadhi ya maswali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweyunga, Hili watu wa CCM hawataki kulisikia hata kidogo maana wanajua kabisa itakapopatikana tume huru na kurekebishwa sheria zinazohusiana na utangazaji wa mshindi hasa kiti cha urais wanajua hawana nafasi na chama kitafariki kama kilivyofariki KANU.
Wanachukiwa na wanalifahamu hilo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unavyouliza

Ebu tuambie nani abebe hili badiliko?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa maoni yangu swali la nani abebe hii hoja inapaswa kujibiwa hivi:

- judicial activists

- media activists

- legislative activists

- civic activists

- political activists

Wote hawa wachangamke na kukoleza moto wa mageuzi ya NEC tangu sasa
 

Kwa hiyo tufanye rafiki?
 
Lkn naomba nikuulize,
Kwanini tuitake kama hisani badala ya sadaka toka kwa magufuli?

Kwa vyovyote vile, Tume huru haiwezi kuja kama hisani. Umma unayo haki ya kuwa nayo na unalo jukumu la kuidai kwa njia zote halali zinazowezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…