Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Mama Amon, Tunapoamua kujadili hoja hii tuweke mapenzi pembeni ya vyama.

Nimependa Leo hoja polepole
" wanaotakiwa kuizungumzia tume ya uchaguzi ni umma"
Kumbuka hao kina mbowe si malaika hivyo nchi itajengwa na wenye nia safi hata wanasiasa wakiwemo je wanapotaka Leo tume ni kwa maslahi yapi wakati miaka minne imepita bila kutaka tume huru au muda umepita tangu Cdm na Nccr zilipofungua kesi ya tume?

Mabadiliko ya katiba ni muhimu kuliko kipengele hiki kidogo ambacho mnang'ang'ania kwani hakitakuwa na mashiko kwa kuwa nchi hii ya vyama vingi haina katiba ila imekopa katiba na sheria za chama kimoja.

Ukitumia mahakama kama Mtafiti yule juu, kujustify Uhuru WA Tume mnayotaka bado shida itakuwepo tu kama iliyopo kwa Mahakama na bunge vinavyoongoza kwa hisani ya rais WA nchi.

Tuna tume huru ya haki za binadamu, umewahi kuisikia ikiipinga serikali katika Yale inayokiuka has a mauji, utumiaji Nguvu kupita kiasi kwa polisi na magereza na mengi yaliyotokea.
Huu ni mfano WA nchi tuliyonayo, angalia tume na vyombo huru vya marekani vinavyofanya kazi.

Hiyo tume mnayotaka ni tume ya kisiasa ambayo haitakuwa na uhai kwa siasa na uongozi WA nchi hii.

Ebu tufikiri zaidi ya hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali za mitaa CCM imepata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%, kumetokea hatari gani?.
Uchanguzi Mkuu ujao, wembe ule ule uliotumika kunyolea serikali za mitaa, utatumika uchaguzi Mkuu but this time victory margin will be a bit low due to Zanzibar factor. Kutatokea hatari gani wakati dola ipo?.
P
With all those sponsored acrobatics you still maintain that ule ulikuwa ni ushindi wa kishindo. If the answer is yes then I have to retire from this discussion
 
Ramark,
Tume ni chombo kilichoundwa na katiba huwezi kufumua tume peke yake lazima iendane na kuondoa ukiritimba uliopo chini ya katiba ya sasa.

Ingawa Kuna mgawanyo wa madaraka lakini kiuhalisia na chini ya katiba ya sasa dhana hiyo haiwezi kufanya kazi. Ona jinsi jinsi tume ya mahakama inayoundwa na katiba ilivyo, ni utani kwa dhana ya huru wa mahakama na mgawanyo wa madaraka.

At the bottom line kinachotakiwa ni katiba mpya
 
Sikatai kuwa tume inautumwa lkn pia mkumbuke system ya nchi yetu inautumwa chini ya MTU mmoja anaitwa rais hivyo hadi katiba inautumwa kwa rais na ccm

Hahahahah acha nijichekee Mimi
Yaani hatuna katiba huru yenye Nguvu ya kumbalance na kumcheki rais WA nchi yetu hahahahahahahahhahah

Hii ndiyo ingekuwa chukizo kwa wanataaluma makini wote pamoja na wale wanaotaka siasa safi na uongozi makini.

Chekeni kama linafurahishwa na nitukaneni kwa hoja kama kicheko changu kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark,
Nina mapenzi binafsi ya kisiasa. Lkn ktk suala la hoja ninao uwezo wa kuyaweka kando.

Kuhusu ukimya wa chadema kwa miaka minne jawabu liko wazi. The squeezed public space where media, judicial, civic and other activisms have virtually been eliminated.

Umeona juzi kina Mbowe wanafungwa akaunti ya Mbowe yenye fedha nzuri ya kuweza kujiokoa na kuwaokoa wenzie inabanwa. Hali sio rafiki.

Lkn suala la Tume huru ni kubwa kuliko Tume ya haki za binadamu. Linahusu uhai na kifo cha Taifa.

Mwalimu wangu wa ujasiriadola na usalama wa nchi alifundisha sequences hizi:

1. WEAK POLITICAL PARTY+WEAK ELECTORAL BODY+WEAK GVT+FRAGILE STATE=FAILED STATE.

2. STRONG POLITICAL PARTY+STRONG ELECTORAL BODY+STRONG GVT+STABLE STATE=ENDURING STATE.

Hivyo, akanambia kuwa Tume Huru ya uchaguzi ni miongoni mwa vyombo muhimu kwa ajili ya kulinda uhai, na hivyo, usalama Taifa.

Kwa hiyo, hoja ya Mbowe imoortant, urgent and necessarily unavoidable kwa sababu za kiusalama.

Ni sawa na kumuwahisha mgonjwa kwenda Muhimbili kwa ambulance.

Tusiipuuze. Tayari CCM ni dhaifu, tuna serikali dhaifa as defined by prevalent extra legal operations, tuko ktk nchi yenye sifa zote zinazohitajika kubatizwa jina la FRAGILE STATE.

Linalowezekana leo lisingoje kesho. Nadhani hata wabunge wa CCM wenye uelewa wa mambo haya wataunga mkono hoja.
 
Ngambo Ngali,
That is ok. But Tume ya Mahakama na Tume ya Haki za Binadamu, kwa upande mmoja, na Tume ya Uchaguzi, kwa upande mwingine, ni vitu viwili tofauti.

Kuvifananisha ni sawa na kusema maembe na viazi yote ni matunda. Kwenye makala yangu hapo juu nimemrejea Makulila kwa kirefu kwa sababubhii. Hoja yake ni nzito sana.
 
Ramark,
Halafu madai kuwa wanaopaswa kuongelea hoja ya Tume huru ni umma badala ya wanasiasa inatengeneza false dichotomy.

Umma unawachagua viongozi. Hawa viongozi wanaongea kwa niaba ya na kwa faida ya umma unaowakilishwa.

Kwa hiyo hapa hakuna either/scenario. Kilichopo ni both/and scenario.

Mjadala usonge mbele.
 
Sawa nakubali

Ninachokikataa ni wanasiasa kuona hii ni hoja yao na ndiyo wanaotaka matokeo pekee, hivyo nasi umma tuone kuwarekebisha kuwa hautuahitaji tume pekee tunataka mfumo WA nchi nzima ubadilike na hiyo ndiyo iwe hoj yetu kuliko nasi kubaki kwenye hoja ya mahitaji ya wachache

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark,

Ulichosema kuhusu katiba ni kweli. Hakuna wa kukucheka. Shida iko hapa:

- ajenda ya katiba mpya imepigwa stop na Rais huyu

- Rais huyu anaruhusu viraka kuwekwa ktk katiba ya sasa.

- hii ni fursa inayoweza kutumika kuhuisha Tume ya uchaguzi.

Hapo vipi?
 
Sawa nakubali

Ninachokikataa ni wanasiasa kuona hii ni hoja yao na ndiyo wanaotaka matokeo pekee, hivyo nasi umma tuone kuwarekebisha kuwa hautuahitaji tume pekee tunataka mfumo WA nchi nzima ubadilike na hiyo ndiyo iwe hoj yetu kuliko nasi kubaki kwenye hoja ya mahitaji ya wachache

Sent using Jamii Forums mobile app

Ajenda ya katiba mpya imepigwa nyundo tayari. Viraka vinaruhusiwa. Hiyo sio fursa ya kuboresha Tume? There is time for radical change and a time for incremental change.
 
Mama Amon,
Mahakama ina mchango mkubwa sana Kwenye hili. Mahakama nzuri na huru inapatikana pale ambavyo tume ya mahakama ni huru.

Kutenganisha vyombo hivyo mahakama na tume ya mahakama na kuwa na dhana kuwa havina uhusiano na tume ya uchaguzi haitaleta matokeo chanya hata Siku moja
 
Mama Amon, Unaonaje kama wote tukisema tunanchi inayoelekea kuvunjika kwa hatuna strong polical party Kwa maelezo yako hapo juu?

Mwalimu wako alikufundisha kwa chama kitakachokuwa madarakani itaonekana hivyo na hasa mfumo WA chama kimoja.

Lkn chama cha ccm kiko hivi tangu 1977 na inawezekana kinanguvu zaidi ya 1995 kwa kuwa kinafedha, ushawishi kwa watu wenye Nguvu nchini, pia kinamtandao WA watu ambao bado unatumiwa na serikali mpaka Leo.

Hivyo tumekuwa na nchi imara tangu awali kwani wakati wote huo hakukuwahi kuwa majaribio ya kuhatarisha usalama wa nchi wala madaraka ya rais na ndiyo maana tangu muda WA mpito WA katiba ya 1977 kuisha nchi imekuwa salama.

Kwangu naona, tumeishi ktk vyama vingi tukiwa hatuna chama imara ikiwemo ccm ndiyo maana system nzuri ya nchi ikiwemo tume ya uchaguzi, kwa kulingana na hoja yako.

Lkn siasa ya vyama vingi inategemea system ya nchi iliyoundwa na katiba hivyo hata mgombea huru akishinda nchi itaendelea kuwa salama au chizi akiwa rais bado tutakuwa salama.

Tuache uoga kupitia mgongo WA uvyama, pia uoga WA sababu rahisi katika kuidai tume huru kuanzia January 2016 kama yalivyokuwa hayo sijaona kama yamebadilika lkn hoja mmeileta

Najua tume ni muhimu kwenu na sisi hasa tunapoona umuhimu WA kura zetu zisipozingatiwa, na hatuwezi kudai katiba mpya sasa lkn mngeonesha zaidi ikiwemo na tume mnayotka yabadilike sisi wenye hoja hizi tungeona msingi WA kuibadili nchi yetu itawalike kwa maoni ya wengi.

Bunge ambalo chadema inahudumu bado ni bovu na hamjaonesha nia ya kulibadili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na je, ni batna ya nani inaendana na maslahi mapana ya taifa?
BATNA ya wataka tume huru ndiyo njia ya kufuata lakini kwa angalizo lifuatalo.

  • Tume huru bila sheria nzuri ya uchaguzi ni sawa na gari zuri kwa muonekano wa nje na ndani lakini halina kizibiti mwendo (break), Gari hilo linaweza kusababisha ajali na malengo ya abiria yakaishia njiani.
  • Sawa sawa na ndege nzuri kimuonekano lakini haina viongoza njia (navigation systems), Ngege hiyo inaweza kupoteza muelekeo ikawapeleka siko au ikapata ajali na kusitisha safari yetu ya maisha bora.
  • Sawa sawa na kujenga nyumba nzuri ya mbao na vioo katikati ya hifadhi ya wanyama ya Selous bila kuweka uzio wenye mfumo wa umeme unaoweza kuzuwia wanyama wakali wasidhuru watu, nyumba hiyo inaweza kugharimu maisha ya wakazi wake na kukatisha malengo yao.

Na hizo sheria ziwape uhuru wagombea wa vyama vyote na kuweka uwanja sawa wa kushindania kushika dola, ziondoe mianya ya wagombea wote kuwekwa na watu au taasisi zenye malengo kama ya familia ya Gupta(The Gupta family) wa SA.

Familia au taasisi kama zile ndiyo zinaondoa kabisa dhana za BATNA kusaidia kutupatia matokeo mazuri pale serikali inapofanya majadiliano kuhusu mikataba ya kusimamia rasilimali za taifa, au maslahi mengine ya kiuchumi na kijamii.

Sheria ikitoa mwanya kwa wagombea kufadhiliwa au kuwekwa madarakani kwa fedha za kishetani kisha raisi anakuwa wakala wa kutekeleza 'agenda' za dola zingine nje ya mipaka ya nchi yetu, basi ni afadhali tubaki na tume mbovu lakini tusiishi tumepiga magoti kwa hao mawakala wa shetani toka nje.

Waswahili wanasema bora zimwi likujualo halikuli likakumaliza, ni afadhali dikteta au mnyonyaji miongoni mwetu ambae atatuibia na kutunza au kuwekeza pesa nchini mwetu kisha moja kwa moja pesa hizo zitaenda kunufaisha watanzania wengine wengi, iwe kwenye ajira au mikopo ya bank zilizohifadhi fedha za kiongozi wetu alie tuibia. Kuliko pesa hizo zingeenda kukopeshwa watu wengine kwenye bank za nje.

Kwa kusema hivi sihalalishi wizi, nimesema hivyo nikijua katika maisha halisi hakuna serikali inayo kosa wezi na wala rushwa.

Tatizo ni kiwango na aina ya rushwa zinaathiri jamii yote kwa kiasi gani? Ikifikia rushwa inasababisha walio wengi kushindwa kumudu gharama za maisha kama makazi bora, elimu, huduma za afya na maji hapo kunakuwa ni tatizo kubwa.

Ubaya wa kiongozi wakala wa mashetani wa nje unaweza kuja kuonekana kwenye mambo yetu ya tamaduni, mila na desturi. Anaweza kuja kutekeleza kampeni za mambo yaliyo nje ya mila na desturi zetu kwa sababu hana kauli wala nguvu ya kumpinga mtu alie muweka hapo kwenye kiti cha enzi. Mtu aneye shindwa kushikia mila na desturi zake anakuwa amepoteza utambulisho na uhuru wake.

Kwa kumalizia ningeomba pia hizo sheria safi za uchaguzi, na tume huru pia ziwabane vyama tawala kutotumia rasilimali za umma kujibakiza madarakani. Hapa nisingependa kuchambua sana sababu umekwisha elezea vizuri sana kwenye hoja yako kuu.

Labda tu niseme rasilimali hizi ni pamoja na watumishi wa umma sekta nyeti zile. Namaanisha ziondoe vyombo vya ulinzi na usalama au watu wa serikali za mitaa kwenye upande mmoja wa mizani ya wagombea na kuwaweka nje ya kabisa ya vita hivi vya madaraka.

Maana kubaki madarakani kwa njia kama hizi kunaweza kuja kutuletea vita kubwa ya wenyewe kwa wenye mbele ya safari hata kama sio miongo miwili au mitatu ijayo.
 
Na je, ni batna ya nani inaendana na maslahi mapana ya taifa?
BATNA ya wataka tume huru ndiyo njia ya kufuata lakini kwa angalizo lifuatalo.

  • Tume huru bila sheria nzuri ya uchaguzi ni sawa na gari zuri kwa muonekano wa nje na ndani lakini halina kizibiti mwendo (break), Gari hilo linaweza kusababisha ajali na malengo ya abiria yakaishia njiani.
  • Sawa sawa na ndege nzuri kimuonekano lakini haina viongoza njia (navigation systems), Ndege hiyo inaweza kupoteza muelekeo ikawapeleka siko au ikapata ajali na kusitisha safari yetu ya maisha bora.
  • Sawa sawa na kujenga nyumba nzuri ya mbao na vioo katikati ya hifadhi ya wanyama ya Selous bila kuweka uzio wenye mfumo wa umeme unaoweza kuzuwia wanyama wakali wasidhuru watu, nyumba hiyo inaweza kugharimu maisha ya wakazi wake na kukatisha malengo yao.

Na hizo sheria ziwape uhuru wagombea wa vyama vyote na kuweka uwanja sawa wa kushindania kushika dola, ziondoe mianya ya wagombea wote kuwekwa na watu au taasisi zenye malengo kama ya familia ya Gupta(The Gupta family) wa SA.
Familia au taasisi kama zile ndiyo zinaondoa kabisa dhana za BATNA kusaidia kutupatia matokeo mazuri pale serikali inapofanya majadiliano kuhusu mikataba ya kusimamia rasilimali za taifa, au maslahi mengine ya kiuchumi na kijamii.

Sheria ikitoa mwanya kwa wagombea kufadhiliwa au kuwekwa madarakani kwa fedha za kishetani kisha raisi anakuwa wakala wa kutekeleza 'agenda' za dola zingine nje ya mipaka ya nchi yetu, basi ni afadhali tubaki na tume mbovu lakini tusiishi tumepiga magoti kwa hao mawakala wa shetani toka nje.

Waswahili wanasema bora zimwi likujualo halikuli likakumaliza, ni afadhali dikteta au mnyonyaji miongoni mwetu ambae atatuibia na kutunza au kuwekeza pesa nchini mwetu kisha moja kwa moja pesa hizo zitaenda kunufaisha watanzania wengine wengi, iwe kwenye ajira au mikopo ya bank zilizohifadhi fedha za kiongozi wetu alie tuibia. Kuliko pesa hizo zingeenda kukopeshwa watu wengine kwenye bank za nje.

Kwa kusema hivi sihalalishi wizi, nimesema hivyo nikijua katika maisha halisi hakuna serikali inayo kosa wezi na wala rushwa.
Tatizo ni kiwango na aina ya rushwa zinaathiri jamii yote kwa kiasi gani?
Ikifikia rushwa inasababisha walio wengi kushindwa kumudu gharama za maisha kama makazi bora, elimu, huduma za afya na maji hapo kunakuwa ni tatizo kubwa.

Ubaya wa kiongozi wakala wa mashetani wa nje unaweza kuja kuonekana kwenye mambo yetu ya tamaduni, mila na desturi.
Anaweza kuja kutekeleza kampeni za mambo yaliyo nje ya mila na desturi zetu kwa sababu hana kauli wala nguvu ya kumpinga mtu aliye muweka hapo kwenye kiti cha enzi. Mtu anaye shindwa kushikia mila na desturi zake anakuwa amepoteza utambulisho na uhuru wake.

Kwa kumalizia ningeomba pia hizo sheria safi za uchaguzi, na tume huru pia ziwabane vyama tawala kutotumia rasilimali za umma kujibakiza madarakani. Hapa nisingependa kuchambua sana sababu umekwisha elezea vizuri sana kwenye hoja yako kuu.
Labda tu niseme rasilimali hizi ni pamoja na watumishi wa umma sekta nyeti zile.
Namaanisha ziondoe vyombo vya ulinzi na usalama au watu wa serikali za mitaa kwenye upande mmoja wa mizani ya wagombea na kuwaweka nje kabisa ya vita hivi vya madaraka.
Maana kubaki madarakani kwa njia kama hizi kunaweza kuja kutuletea vita kubwa ya wenyewe kwa wenye mbele ya safari hata kama sio miongo miwili au mitatu ijayo.
 
Halafu madai kuwa wanaopaswa kuongelea hoja ya Tume huru ni umma badala ya wanasiasa inatengeneza false dichotomy.

Umma unawachagua viongozi. Hawa viongozi wanaongea kwa niaba ya na kwa faida ya umma unaowakilishwa.

Kwa hiyo hapa hakuna either/scenario. Kilichopo ni both/and scenario.

Mjadala usonge mbele.
Kwa hoja yako hii unataka kusema kura ya maoni yanapohitajika mawazo au maoni ya wananchi wenyewe haina umuhimu sababu wawakilishi (viongozi) wetu tuliowachagua watatusemea mawazo yetu?

Je kama wawakilishi hao wamebadilika kitabia na sasa hawatusemei maoni yetu tulio watuma watuwakilishe?
Inajulikana wazi kabisa, 'it's a plain truth' binadamu hubadilika kutokana na muda mrefu unavyopita tangu kufanya agano na wenzi wao.
 
Mahakama ina mchango mkubwa sana Kwenye hili. Mahakama nzuri na huru inapatikana pale ambavyo tume ya mahakama ni huru.
Kutenganisha vyombo hivyo mahakama na tume ya mahakama na kuwa na dhana kuwa havina uhusiano na tume ya uchaguzi haitaleta matokeo chanya hata Siku moja

Sorry hujaelewa pointi yangu kama nilivyoichukua toka kwa Makulila (tazama makala yangu). Ni hivi: Tume ya uchaguzi inaamua nani aunde serikali, nani ajaze nafasi za Tume ya Mahakama na nani ajaze nafasi za Tume ya Haki za Binadamu. Hivyo, Tume ya Uchaguzi ina first order power na hawa wengine wana second order power. They are incomparable, as Makulila says.
 
Kwa hoja yako hii unataka kusema kura ya maoni yanapohitajika mawazo au maoni ya wananchi wenyewe haina umuhimu sababu wawakilishi (viongozi) wetu tuliowachagua watatusemea mawazo yetu?

Je kama wawakilishi hao wamebadilika kitabia na sasa hawatusemei maoni yetu tulio watuma watuwakilishe?
Inajulikana wazi kabisa, 'it's a plain truth' binadamu hubadilika kutokana na muda mrefu unavyopita tangu kufanya agano na wenzi wao.

Kwani representative democracy maana yake nini? Wananchi wote hawawezi kuwa Bungeni just as wanachama wote wa CCM/CDM hawawezi kuwa Dodoma. Naona kwamba wale wanaoshindwa kuwakilisha waliowatuma ni exception to the rule na haiwezi kuchukuliwa kama kanuni
 
Ramark,
Paragraph yako ya kwanza inayo mantiki kubwa. Chama kinakuwepo pale vyombo vya maamuzi vinapofanya kazi zake za kikatiba.

Kwa sasa CCM hawafanyi kitu kwa sababu mwenye maamuzi yote ni Mlawi mmoja tu.

Chadema hawafanyi kwa kuwa wamekuwa drained na Mlawi. Ngoma draw, lakini chanzo ni huyo Mlawi wa CCM.

Dawa inapaswa kutoka nje ya Walawi. Na CDM wameonyesha njia. Otherwise nchi inavunjika kama unavyosema.
 
Back
Top Bottom