Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
- Thread starter
- #141
Nundu_Tanzania,
Ndugu Nundu, umeandika nini hapo? Sikiliza rafiki:
- kazi ya Tume ya uchaguzi ni kusimamia haki ya umma kuamua na kusimika serikali yao kwa sababu wanazozijua wapiga kura hata kama ni wajinga, mbumbu, mabwege au hohehahe.
- Katika suala la haki ya kujitawala (right to self determination) Wapiga kura hawa wanazo haki sawa kabisa na haki walizo nazo wasomi, wajuzi, wajanja, na matajiri.
- ushahidi pekee unaokuwa mikononi mwa Tume sio habari ya elimu, maarifa au ukwasi wa wapiga kura, bali idadi ya kura za ndiyo na hapana mintarafu wagombea.
- kwa hiyo, uhuru wa Tume hautegemei weledi wa wapiga kura.
- badala yake uhuru wa Tume unategeme weledi na uadilifu wa maafisa wa Tume, uimara wa kibajeti wa Tume, kutoingiliwa na serikali, kutoingiliwa na vyama vya siasa, na kutoingiliwa na mahakama pasipo sababu nyeti.
Mjadala uendelee.