Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii itabidi uniwekee 'reference' ya sauti, maandishi au video ili tuweke sawa kumbukumbu na kuondoa mashaka yoyote ya ukweli wa hoja hii.Umejieleza vizuri. Shida kubwa ambayo hujagusa ni hii: Bosi wa NEC alisema alikuwa anatangaza matokeo anayoletewa na watu wasiojulikana
Jambo lingine la muhimu ni lazima tutambue hatua ya kutangaza matokeo halali ya uchaguzi ni hatua ya mwisho kabisa katika kutupatia viongozi halali na safi kwa njia ya kidemokrasia.Umejieleza vizuri. Shida kubwa ambayo hujagusa ni hii: Bosi wa NEC alisema alikuwa anatangaza matokeo anayoletewa na watu wasiojulikana. Tukiziba tobo hilo mengine ni rahisi. Tunataka NEC itoke kwapani mwa bosi wa watu wasiojulikana. Umeelewa?
Hii itabidi uniwekee 'reference' ya sauti, maandishi au video ili tuweke sawa kumbukumbu na kuondoa mashaka yoyote ya ukweli wa hoja hii.
Nahofia isijekuwa ni maneno ya kutengenezwa.
Nchi nyingi hazikujengwa na wanasiasa zilijengwa na wanaharakati pamoja na wanataaluma kwa kuwatumia wanasiasa.
Uingereza wenye mamlaka ya kuamua sura ya nchi ni maaskofu na malords achana na wanasiasa WA house of Commons
Sent using Jamii Forums mobile app
Bosi wa NEC alisema alikuwa anatangaza matokeo anayoletewa na watu wasiojulikana.
Hapa kipi ni kipi?Mwaka 2015 Bosi wa NEC alibanwa na Lowassa aeleze kwa nini taarifa anazotangaza ni tofauti na matokeo halisi yaliyoko vituoni.
Jibu la boss lilikuwa fupi: "Inawezekana ni tofauti kwa kuwa mimi natangaza kile ninacholetewa mezani na wasaidizi wangu".
Hapa kipi ni kipi?
Kisheria "wasaidizi wangu" siyo sawa na "watu wasiojulikana".
Aisee uchambuzi ni nadra kufanywa na mwanamke,,,,Nina wasi wasi kama ni mke, kama ndyo basi nampongezaDuh, Mama Amon Pongezi kwa uchambuzi, Ila mmmmh. Mama Amoni umeiva sana, ni Mama Amoni Kweli?
Basi ngoja turudi kwenye hoja kuu kumbe tatizo ni sheria ya TISS?
Au tatizo ni sheria ya uchaguzi au Tume ya Uchaguzi?
Kwa hivyo mkuu umehamua kuwa dikteta? Unapanga peke yako mjadala wa hoja zipi ni za msingi na unataka sisi wachangiaji wengine tuchangie subserviently kile unachotaka kukisikia?
Sawa wote wanashiriki lakini hoja ipo kwa yupi anayeshika bendera ya badiliko likaleta tija kwa taifa.Wanasiasa, wanaharakati, wanateolojia, wanafalsafa and so on ni change agents ktk mchakato wa kujenga nchi; kujenga nchi ni mradi wenye majukumu mengi, kila mmoja akianzia upande wake; hivyo, hakuna mwenye monopoly juu ya kila jukumu ktk mradi huu.
This being the case, can you reframe your point?
Unaweza kukosa kujuwa suluhisho la kweli la tatizo unalo lalamikia sababu unafunga uwezekano wa kupokea mawazo mbadala.Kwa kuwa bandiko hili nimelianzisha mimi, ninalo jukumu la kuhakikisha mjadala unakidhi mahitaji ya hoja niliyoisanifu. Kuna tatizo hapo?
Jawabu langu tangu jana ni hili:
kuna wakati wa kufanya radical changes na wakati wa kufanya incremental changes; mazingira ya leo hayaruhusu radical changes; hivyo twende na mkakati wa incremental changes kwa kuanza na Tume ya uchaguzi. Simple.