Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

"kutenda haki" ni very subjective term, and is open to a wide variety of interpretations. Haki kwa mtu mmoja inweza kuwa kosa au jinai kwa mwingine. Kwahiyo syllogism yako ni batili sababu premise namba moja haisimami kipekee kama ukweli usiopingika.

Naona umekuja karibu na ukweli. Naongelea kauli yako kwamba, "Haki kwa mtu mmoja inweza kuwa kosa au jinai kwa mwingine." Huu ni umachiavelli. Elewa kuwa, watu wote ambao ni devout Catholics wanaamini na kuelewa hoja ifuatayo:

- it is always wrong to directly choose to do evil so that good outcomes may result.

-a direct choice to override ones duties in order to pursue a proportionate right is an act of intentionally choosing an evil means toward a good end.

- Thus, a direct choice to override ones duties in order to pursue a proportionate right is morally wrong and repugnant to divine plan of human salavation.

Kwa hiyo nikuulize tena, bado unafikiri kuwa JPM ni devout Catholic?
 
Huyu mpumbavu ndiyo kajua sasa hivi kuwa NEC siyo huru ?

Naona umeanza kuweweseka. Jielekeze kwenye hoja iliyo mezani.
Alichokiandika Membe ni mawazo yake. Hajasema kwamba kajua jambo hili leo. Namnukuu kwa kumtafsiri:

"Nilisema mbele ya Kamati ya Maadili na hapa nataka niseme tena: Mazingira ya kisiasa yaliyopo nchini Tanzania leo yanahimiza uwepo wa Tume ya Uchaguzi yenye uhuru mkubwa, yenye uwakilishi mpana na yenye uwazi mkubwa kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya Wilaya. Kwa hiyo naunga mkono kwa nguvu zote sauti zinazopazwa kwa ajili ya ujio wa Tume ya aina hiyo."


1584690246451.png


Kama unapinga kauli yake weka hoja mezani. Hili ni jukwaa la hoja. Kama hujajiandaa kaa pembeni usome hoja za watu baki.

No research no right to speak....
 
Sky Éclat . Hawa kina Membe ndiyo wale wale, wakiwa ndani ya system wanashindwa kuidhauri vizuri kiti. Kwa uhusiano aliokuwa nao na JK , alishindwa nini kumshauri waiache nchi ikiwa katika mfumo unaoeleweka na ulio fair kwa kila mwananchi ?!.

Akili zinawakaa sawa wakishakuwa nje ya mfumo, jambo ambalo halisaidii, kwani aliye na kiti anafaidika na ubovu uliopo .

Maelezo yake yanajibu dukuduku zako. Ameseka "kwa kuzingatia mazingira yaliyopo leo"

Hata Nyerere alisema kuwa Katiba yetu inayo matobo yanayoruhusu udikteta ikiwa tutapata Rais mwenye vimelea vya udikteta. Mbona hakuibadilisha kabla ya kustaafu?

Ni kaz yetu leo, jana imepita.
 
Asante sana Mama Amon kwa Makala iliyo sheheni maarifa. Ungenukuu tarehe ya waraka ingenoga zaidi.

Mkuu,
Tayari nimeweka tarehe, hyperlink na rejea husika kutoka vatican website.
Asante kwa kunikumbusha hilo.
 
Odhiambo cairo,
Sawa mkuu.
Kwa lengo la kulinda mjadala mkuu wa Mama Amon itabidi nikubali kutokubaliana.
I know it's an oxymoron, how can you agree to disagree in the first place?
 
Ahsante @Mama Amon kwa bandiko lako. Kuna kitu tofauti ambacho binafsi nimekiona umefanya kimakosa. Umerejea vizuri uzuri wa waraka wa Zambia na Kenya, lakini ulipokuja kwenye Waraka huu wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania ambao umeokosoa haukujikita kwenye kuurejea sana wenyewe bali ulijikita zaidi katika kurejea kauli za akina Mnyika, Majaliwa na Bashiru. Ingekuwa vyema kama ungeambatanisha waraka tajwa, ningetafuta muda niusome, labda contents zake zinaweza zikawa zinamsukuma msomaji kuukwepa kuujadili na hivyo kutafuta ya kujadili kutoka kwingine.

Asante kwa angalizo.
Nimerekebisha kosa hilo.
Sasa hoja imenyooka.
Sasa nawataja Zambia na Kenya kama njia tu ya kuonyesha pengo la yale madokezo mawili ya mwisho yanayohitaji kusanifiwa na makuhani walei.
 
Sawa mkuu.
Kwa lengo la kulinda mjadala mkuu wa @Mama Amon itabidi nikubali kutokubaliana.
I know it's an oxymoron, how can you agree to disagree in the first place?

Uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana huwa unafanyika.
Na ni pale tu ambapo mshiriki katika majadiliano anacho kitu kinaitwa BEST ALTERNATIVE TO NEGOTIATED AGREEMENT (BATNA).

Katika mjadala wa sasa BATNA ya wale wanaokataa Tume Huru ni kutumia vyombo vya dola kunyamazisha mijadala kama hii.

Wewe BATNA yako ni ipi?
 
Mama Amon,hongera sana kwa bandiko lenye hoja nzito na lililosheheni rejea mbalimbali,yapo mengi ya kujifunza ndani yake.
 
Jambo la muhimu ni wananchi kujitambua.

Hata Mbowe na Chadema wangekuwa Ikulu wangesema NEC ni tume huru na CCM wangepinga!
Hii ndiyo hoja ya Bashiru, Katibu Mkuu wa hovyo kabisa CCM. Ni hoja mfu. Maana yake, kuwadharau watanzania kwamba wanapokwenda kupiga kura wanapoteza muda wao tu. CCM itabaki madarakani si kwa mapenzi ya wapiga kura, bali kwa nguvu za dola. Ni kuwatusi watanzania
 
Mama Amon,
Mama Amon unaonekana umeiva kwenye diplomasia na falsafa itabidi niwe mwanafunzi wako.
Nitakutafuta unipe muongozo kidogo.

Najiuliza ule wakati wa awamu ya kupishana angani ilikuwaje haukutumia uzoefu huu mkubwa wa mambo ya 'negotiation' kutusaidia tusiingie mikataba kama ile ya gesi, na bandari ya kwa shemeji?

Kwanini haukutumia ujuzi huu kutusaidia kuwashawishi wale wengi kwenye jopo la fitina tupate katiba mpya nzuri tena ya wananchi sio ile iliyopendekezwa na hawa unao walilia watupatie tume huru ya uchaguzi?

Kwanini unaamka sasa?
Kwa vyovyote vile madai ya tume huru ya uchaguzi ni ya msingi ingawa yanaonekana kuwa na agenda za ziada nje ya agenda kuu.
 
Kwanini haukutumia ujuzi huu kutusaidia kuwashawishi wale wengi kwenye jopo la fitina tupate katiba mpya nzuri tena ya wananchi sio ile iliyopendekezwa na hawa unao walilia watupatie tume huru ya uchaguzi?

Kwanini unaamka sasa?
Kwa vyovyote vile madai ya tume huru ya uchaguzi ni ya msingi ingawa yanaonekana kuwa na agenda za ziada nje ya agenda kuu.

Nimeelewa concern yako. Lkn niseme manne:

- majadiliano yana kanuni zake. Baadhi ni best alternative to negotiated agreement (batna), worst alternative to negotiated agreement (watna), na effective alternative to negotiated agreement (eatna)

- batna, watna na eatna ni kanuni zenye matumizi ktk majadiliano yoyote including diplomatic, contracting, commercial and similar negitiations.

- hapa tunaongelea kutumia kanuni hizi ktk tasnia ya mjadala wa tume huru ambako kuna chama tawala na serikaki yake, kwa upande mmoja, na civil society plus opposition parties kwa upande mwingine.

- jielekeze ktk mjadala ulio mezani na tujibu pamoja maswali haya: ktk mjadala wa sasa nini batna, eatna na watna ya kambi ya MAGUFULI? Na nini batna, watna na eatna ya kambi ya MBOWE? Na je, ni batna ya nani inaendana na maslahi mapana ya taifa?
 
Mama Amon,
JPM is not a practising Catholic although he uses Catholicism as a religious brand to identify himself. Deep down in his heart, deeds and convictions, he is rather an atheist!!
 
Dini ni makampuni ambayo yapo kwa masirahi, mtu anayeabudu sanamu huitazama sanamu akitumaini kupata msaada.

Kwa jibu hili nimepata nilichokuwa nataka.

Wewe huna weledi wowote kuhusu dhana ya dini na nafasi ya dini katika jamii.

Hata kiswahili kinakupiga chenga. Unaandika "masrahi" badala ya "maslahi".

Tuliza akili ujifunze kutoka kwa watu wenye weledi. Tafuta kamusi soma. Tumia google kupata fasili ya neno "religion" etc. Usikurupuke wala kupayuka tena. Utaumizwa.
 
JPM is not a practising Catholic although he uses Catholicism as a religious brand to identify himself. Deep down in his heart, deeds and convictions, he is rather an atheist!!

Bold statement, though it lacks support. As per standard rules of intellectual engagement, Can you provide grounds, warrants and backings to your claim pls?
 
Masuala ya tume huru, inayotenda haki hutegemea kwa kiasi chote elimu na uelewa wa mambo wa watu katika nchi husika.

Jamii ambayo bado haijawa na elimu na uelewa wa mambo haiwezi kuwa na tume huru na kadhalika.

Kujielekeza kwenye tume huru na vyombo vingine kama chanzo cha kupinga ufalme wa Mungu ni uelewa unaokwepa wajibu.

Hatuwezi kupata majibu ya kweli kwenye matunda.
 
Back
Top Bottom