Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

I'm afraid, the lime left is too little too late.
Kuhamasisha kususia uchaguzi ni kumsusia ngedere shamba la mahindi, utayavuna mabua!.
Akijitokeza mpiga kura mmoja tuu, akapiga kura ya ndio, mgombea huyo atakuwa ameshinda kwa asilimia 100%.
P.

Sio ww tu, wote wasiotaka hiyo tume huru wanajificha ndani ya sababu dhaifu ya muda, huenda na ww umeingia kwenye hiyo hadaa ya muda kwa makusudi au bahati mbaya. Hata kama ww na baadhi ya watu mnaona muda hautoshi, lakini hiyo haiondoi hitaji la ww kuonyesha hiyo tume shirikishi iwe vipi.

Inaonekana Paskali unadhani sisi wapiga tunajali sana hao jamaa kushinda wakiwa wenyewe, kwa taarifa yako bora washinde ila wajue fika hawajashinda kwa kura zetu. Hiyo utatengeneza mazingira rafiki ya kupata viongozi bila kutumia njia ya kura. Njia hiyo ni ya hatari lakini haina budi kutokea.
 
Tatizo usipo piga Kura watapiga wanachama wa CCM na washind watatangazwa so bado hujamkomoa mtu sababu watu wote sio CHADEMA Kuna CCM pia,[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Iwapo haitapatikana tume huru ya uchaguzi, tutatumia ushawishi wetu humu jukwaani na huko mitaani kuhakikisha wananchi wengi kadiri iwezekanavyo kutokushiriki upigaji kura. Hatuko tayari kupelekwa kwenye mfumo wa chama kimoja kwa kubariki uchaguzi wa kihuni. Tutatafuta njia mbadala ya kupata viongozi, lakini hiyo njia ya kura ambayo inaonekana wazi rais aliyepo madarakani na chama chake hawaiheshimu hatuko tayari kuendelea kuitumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ww tu, wote wasiotaka hiyo tume huru, Hiyo utatengeneza mazingira rafiki ya kupata viongozi bila kutumia njia ya kura. Njia hiyo ni ya hatari lakini haina budi kutokea.
Serikali za mitaa CCM imepata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%, kumetokea hatari gani?.
Uchanguzi Mkuu ujao, wembe ule ule uliotumika kunyolea serikali za mitaa, utatumika uchaguzi Mkuu but this time victory margin will be a bit low due to Zanzibar factor. Kutatokea hatari gani wakati dola ipo?.
P
 
Pascal Mayalla,
in other words, kwenye katiba NEC "imepewa tu jina la 'tume huru'" lakini "haina muundo wa 'tume huru'".

so wapinzani haven't missed any point at all - rather wapo sahihi kabisa kudai 'tume huru' kwa vile iliyopo haiundwi kwa mujibu wa jina lililotumiwa katika katiba.
 
Tatizo usipo piga Kura watapiga wanachama wa CCM na washind watatangazwa so bado hujamkomoa mtu sababu watu wote sio CHADEMA Kuna CCM pia,[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app

Sina tatizo na ccm kupiga kura, shawishini hata vyama vyote vishiriki, lakini wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kushiriki uchaguzi wa kihuni, ambao rais na chama chake wanaingia kwenye uchaguzi na matokeo mfukoni. Hakuna mtu anayejiheshimu atashiriki huo uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi. Kwa maneno marahisi, huo uchaguzi wa bila tume huru ya uchaguzi ni sehemu ya kuonea ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka.
 
Serikali za mitaa CCM imepata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%, kumetokea hatari gani?.
Uchanguzi Mkuu ujao, wembe ule ule uliotumika kunyolea serikali za mitaa, utatumika uchaguzi Mkuu but this time victory margin will be a bit low due to Zanzibar factor. Kutatokea hatari gani wakati dola ipo?.
P
kumbuka kuwa until and unless neno "polisi" linaondoka kwenye comparative equation hii hapa chini, neno "beberus" litabaki pia daima dawamu.

hakuna polisi iliyowahi kushinda nguvu ya beberus duniani!

CCM + polisi VS upinzani + umma + beberus
 
Serikali za mitaa CCM imepata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%, kumetokea hatari gani?.
Uchanguzi Mkuu ujao, wembe ule ule uliotumika kunyolea serikali za mitaa, utatumika uchaguzi Mkuu but this time victory margin will be a bit low due to Zanzibar factor. Kutatokea hatari gani wakati dola ipo?.
P

Uko sahihi kabisa na usemayo, lakini bado hujajibu swali langu la msingi kwako kuwa tume shirikishi iweje. Huo ushindi wa 99.9 wa SM za mitaa mbona mdogo watanagaze hata kushinda kwa 200% ila sio kwa kura za walio wengi. Kama dola ipo hapo ni sawa ila sio kwa kura, kwa dola hakuna tofauti na serikali ya kijeshi.

Katika mazingira hayo hata wakijisifia kupendwa itakuwa ni kama kujipaka mafuta ukiwa umevaa nguo. Usipindishe swali langu la msingi, tume shirikishi usemayo iwe na muundo gani. Hayo ya ushindi wa 99 kwakuwa dola ipo wala sio hoja sana kwenye uzi huu.
 
Maaskofu wameliona hilo, lkn kwa sheria ya kanisa lao wameshindwa kuwa wawazi moja kwa moja. Kwa hiyo kama HAWA MAASKOFU NI KWELI kama ni KWELI ni watumishi wa MUNGU aliye hai anaye ishi. Waukemee unyanganyi wa HAKI unao FANYWA na hawa CCM kwa kutumia udhaifu wa sheria zetu za uchaguzi zilizotungwa na haohao CCM.

Biblia inasema kisima kibovu hutoa maji mabovu CCM na BUNGE lao hawawezi kututungia sheria nzuri zenye matokeo ya HAKI. Ndiyo maaba hawasti kusema wanatumia dola kubaki madarakani.

Lakini kibaya zaidi wachungaji uchwara wa makanisa karibu yote wakiwemo hao maaskofu hawana uwezo na hata utashi tu wa kujitokeza hazarani kumtetea MUNGU ambaye ndiye MUNGU MWENYE HAKI.

KUNA kisa cHa Balaki na Balaam katika Biblia ndiyo maaskofu wengi leo wanatumika kulaani NA kudhulum HAKI. Bila tume huru ya uchaguzi hakuna haki itakayotendeka mbele ya CCM inayojitangaza kutumia dola lkn kibaya zaidi unyanyasaji wa wapinzani hasa chadema unaofanywa leo ni kithibitisho tosha kabisa hakutakuwa na uchaguzi ulio sawa.

Kwa walaka huo ambao umechambuliwa ni hakika hao maaskofu hawana uwezo wa kutetea HAKI bali wanajifanya kusemea pembeni au tuseme kujibaraguza ilikuwa shitua watu wengine wadai hiyo HAKI. Ili hata wakiulizwa waseme sisi tulikuwa tunasemea mambo ya ufalme wa MUNGU. Katika nchi nyingi za ukandamizaji wenye akili na waoga hukaa pembeni wakijidai kuchochea moto kupitia wengine.

Hayo maazimio au malengo yao wanatakiwa waya hubiri wakitumia lugha ya uwazi zaidi.

P.
Kasema tume iko huru bali sheria ndiyo mbovu, ubovu wa sheria haumfanyi Mtua wa HAKI, mtu MWENYE haki aitumie kudhulum haki ya wengine. Lkn kwa sababu tangu kutungwa kwake na madhumuni ya kutungwa kwake na hao watungaji wake walilenga kunyanganya HAKI, na kutoa mwanya wa kudhulum basi SHIDA ITAZIDI kuwa mbaya. Na maaskofu hawa basi tutakuta kila anayepinga ataauawa

Kama viongozi wa dini watakuwa ni qatu wasio HAKI na hakuna juhudi kuingiza kwenye utawala watu wa haki. Basi tutamalizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Umeshutumiwa na kila mtu kwamba unaumwa kichaa cha kudhani unafahamu kila kitu kuliko mtu yeyote , kwamba wewe unajua sana kuliko baraza la maaskofu ni uthibitisho wa tatizo kubwa linalokukabili , acha ccm yenyewe kwa maana ya viongozi wake walete hoja za kipuuzi kama hizi za kutetea uozo , unless otherwise useme leo kwamba wewe ni miongoni mwa viongozi wa ccm unayewakilisha upande wa JF

Kiongozi wa Tume ateuliwe na dikteta Magufuli halafu awe huru ! hii itakuwa maajabu ya dunia !

Jaji Lewis Makame ni miongoni mwa majaji walioheshimika kwa kutenda haki Mahakamani , lakini alikuja kuharibiwa baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwa hisani ya mwenyekiti wa ccm , Profesa Abdallah Safari popote alipo anajua umahiri wa Lewis Makame Mahakamani, Makame akalazimika kutii maagizo ya kijinga ya ccm hadi akadharauliwa na kila mtu , hadi kufikia msiba wake kugusa familia yake tu , pamoja na umahiri wake Mahakamani lakini Hakuna mtanzania yeyote aliyeguswa na kifo cha Makame ikiwemo hata ccm iliyomtumikisha

Kumtumikia shetani kukaua mazuri yote aliyoyatenda kwa uaminifu mkubwa .

Apumzike anapostahili kutokana na matendo yake hapa duniani , Amina
 
Makala nzuri ila wavivu wa kusoma hawatajikita kwa kilicho andikwa.Ndio maana sishangai kuona wengi wakimjibu P na kuacha kujadili yaliyomo kwenye makala.
 
Uwanja ni uleule, gharama za kuleta katapila kusawazisha ni kubwa, Na kama lengo ni kucheza... Basi Sjyo lazima kucheza football, tucheze mchezo wa pamoja. Join CCM and practice your free will and politics
 
Makala nzuri ila wavivu wa kusoma hawatajikita kwa kilicho andikwa.Ndio maana sishangai kuona wengi wakimjibu P na kuacha kujadili yaliyomo kwenye makala.

Asante nawe tupe summary ya waraka huo kama ulivyouelewa ili tuendelee kuujadili vizuri zaidi
 
Pascal Mayalla,
Mbona hili ni rahisi sana ndugu Pascal Mayalla , kwa chombo kama NEC na kwa majukumu nyeti kilichopewa kwa mujibu wa sheria na katiba, kitendo cha kukosa ushirikishi pekee tayari kinakuwa kimepoteza Uhuru.

Kwa hiyo hapo hakuna namna NEC inaweza ikaacha kuwa tatizo. Kama Sheria mbaya ya uchaguzi ndiyo imeipa NEC mamlaka au kama sheria mbaya ya uchaguzi ndiyo imepelekea kunndwa kwa NEC sijui ni kwa namna ipi unaijenga hoja yako kwamba yule fisi ndiye aliyemzaa huyu ndama wa ng'ombe.
 
Ahsante Mama Amon kwa bandiko lako. Kuna kitu tofauti ambacho binafsi nimekiona umefanya kimakosa.

Umerejea vizuri uzuri wa waraka wa Zambia na Kenya, lakini ulipokuja kwenye Waraka huu wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania ambao umeokosoa haukujikita kwenye kuurejea sana wenyewe bali ulijikita zaidi katika kurejea kauli za akina Mnyika, Majaliwa na Bashiru.

Ingekuwa vyema kama ungeambatanisha waraka tajwa, ningetafuta muda niusome, labda contents zake zinaweza zikawa zinamsukuma msomaji kuukwepa kuujadili na hivyo kutafuta ya kujadili kutoka kwingine.
 
Back
Top Bottom