Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Mama Amon, Ni kweli kama unavyosema,
Hoja ni nani hawachangamshe? Mpaka sasa chadema imeshindwa kuwachangamsha kupitia hoja iliyoletwa kupitia barua kwa raisi?

Anayepaswa kuwa chumvi ni chadema yenyewe, nimeona kanda ya kati je mnawaendea vipi hao

Kumbuka vuguvugu LA membe 2018 liliwezaje kugeuza upepo WA nchi na siasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark,
Maswali muhimu. Nimemsikia Mbowe akisema ajenda ya Tume huru kwa sasa ni kipaumbele namba moja. Hajatwambia mikakati yake ya kuifanikisha. Definitely anahitaji task force yenye weledi, diversity, and so on kufanikisha. Natamani ajitokeze hapa na kutia neno...
 
Ramark,
Pointi zako nyingi nazikubali isipokuwa moja tu: kwamba wananchi hawaungi mkono hoja ya Tume huru. Inawezekana. Je wanaikataa? Sidhani. Kwa hiyo, ni kazi ndogo kuwaweka katika kambi ya watetezi wa hoja. Mengine nayachukua na nitawapa team Mbowe.
 
Majibu yangu ni Yale ya serikali ya mwaka 1999 nilishasema tangu Jana ambayo mtafiti makulilo aliyanukuu lkn utekelezaji wake ukawa shida hasa kwa kigezo cha yupi anayeanateua majaji.
Kwani kunaulazima tume iwe na majaji?

Raisi kama head of state aunde tume ya usahili ya taifa ya watu saba hadi 10 kisha wafanye blind interview kupata majina ya 30 ya watendaji kumi WA juu kwa ngazi ya taifa.
Hao ndiyo wafanyiwe usahili wa kina kuanzia elimu, uzoefu, mwenendo nk kisha tupate majina yasiyopungua 15 yapelekwe bungeni kwa kura tupate wajumbe 10 ambao wataketi na kuchaguana mwenyekiti na wakurugenz WA tume.

Hao ndiyo nao watafanya usahili blind kutafuta watendaji WA chini kadri itakavyohitajika pia kufanya usahili WA wazi WA mwisho kuwaconfirm wanaowahitaji.

Usahili blind utafanyika kwa kuandika au mitihani, through namba pamoja na discussion hivyo kunaweza kukawa na hatua mbili kwenye blind na hojaji katika open
Haya ni maoni murua. Hebu funguka kidogo. Kwa maoni yako Tume huru ya uchaguzi inapaswa iwe na sifa zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pointi zako nyingi nazikubali isipokuwa moja tu: kwamba wananchi hawaungi mkono hoja ya Tume huru. Inawezekana. Je wanaikataa? Sidhani. Kwa hiyo, ni kazi ndogo kuwaweka katika kambi ya watetezi wa hoja. Mengine nayachukua na nitawapa team Mbowe.
Kwetu Mtwara suala LA gesi lilichambuliwa kirahisi na jk wakati WA uchaguzi, lkn wanaharakati na wanasiasa walieleza vizur tukaelewa hoja ya yetu tukataka ibadilike hapo ndipo ilipozua taharuki.
Lkn Tanzania na dunia walijua nini wamakonde wanataka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwetu Mtwara suala LA gesi lilichambuliwa kirahisi na jk wakati WA uchaguzi, lkn wanaharakati na wanasiasa walieleza vizur tukaelewa hoja ya yetu tukataka ibadilike hapo ndipo ilipozua taharuki.
Lkn Tanzania na dunia walijua nini wamakonde wanataka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Noted. Nafiri wananchi wanaweza kutaka kitu kwa njia mbili. Mosi, via autonomous demand. Pili, via induced demand. Suala la Tume huru ni technical kama makala yangu ilivyoonyesha. Hivyo, most likely, wananchi wataitaka Tume via induced demand. Media activism, legal activism, legislative activism, civic activism, theological activism, etc ni baadhi ya njia za kuzalisha induced demand. Mimi hapa nafanya media activism. Tayari watu 7,000 wametazama bandiko hili. Tunasonga mbele.
 
Kwa vyovyote vile, Tume huru haiwezi kuja kama hisani. Umma unayo haki ya kuwa nayo na unalo jukumu la kuidai kwa njia zote halali zinazowezekana
Si lazima ziwe halali ila zinapaswa kuwa angalau kuheshimu sheria ya maumbile.

Intelligence unit zote zinatumia halali zisizo halali kwa manufAa ya wengi pia ndiyo kwenye maadili kuna aina za uongo

Hivyo maadili yanaangalia sana ukombozi WA mtu na maslahi ya wengi.

Padri mmoja akiulizwa mahakamani kuwa mtu huyu aliwahi kuungama ameua hatajibu au atasema sikumbuki, Siku akitoa jibu, ukombozi WA wengi kupitia maungamo yanakufa hapohapo dunia nzima.

Taarifa zote za kuchagiza mijadala 2005-2015 mlikuwa mnazipata kihalali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama Amon,
The late J.K.Nyerere was a devout Catholic in his private life, and yet he had his share of criticisms and blame in his role as leader of Tanzania, to the extent he was even regarded as a ruthless ruler by some. I believe JPM is a devoted Catholic too, in his private life.

The mistake you're making is trying to measure the veracity of one's religious convictions, a completely private and personal affair, from their actions and words as public figures exercising their public roles by using a few logical statements, something I find completely absurd.
 
Ndjabu Da Dude,
Big NO. First, JPM does not compare with Nyerere by many standards. Secondly, public morality and private morality are not mutually exclusive. And three, where sin has been defined as a crime by the legislature, a believer bears a double blame: first at a private level; and secondly, at a public level. Thus, your defense fails. You are just dropping words unreflectively.
 
Bright mind does not discuss people
Big NO. First, JPM does not compare with Nyerere by any standard. Secondly, public morality and private morality are not mutually exclusive. And three, where sin has been defined as a crime by the legislature, a believer bears a double blame: first at a private level and secondly, at a public level. Thus, your defense fails. You are just dropping words unreflectively.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lkn linapingana na imani yako iliyonukuliwa hapo juu.

Kumbuka, maswali yangu ya bandiko 201 Hujayajibu

Sent using Jamii Forums mobile app

Maswali yako nitayajibu nikikaa kwenye PC. Simu ina limitations.

Kuhusu rai yako kwamba: under certain circumstances good ends may justify evil means, that is good for secret service officers as you clearly indicated. Beyond that, we can debate, though not under this thread.
 
Kwa nchi Zetu hizi za Kiafrika, Kupata Kitu huru ndani ya nchi ambayo sio huru, ni Kazi ngumu Kama kutarajia Kupata Mtoto wakati hauna kizazi yaani namaanisha bila ya nguvu ya Mwenyezi Mungu haiwezekani.. Tunaweza Kupata tume huru kwenye makaratasi lakini Kupata tume huru kiutendaji ni Kazi ngumu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi yetu si huru?
Kwa mantiki IPI?

Ukisoma maelezo yote utagundua tunayo nchi huru isiyo na organs huru

Hatuna huru hata ya makaratasi ambayo tunaitka ni hiyo ya makaratasi then tuone kama haitashughulika.
Maana atakaye mcheki ni bunge na kumwajibisha.

Kama uko karibu na Mungu muombe atujalie ya makaratasi tunayoitaka.
Kwa nchi Zetu hizi za Kiafrika, Kupata Kitu huru ndani ya nchi ambayo sio huru, ni Kazi ngumu Kama kutarajia Kupata Mtoto wakati hauna kizazi yaani namaanisha bila ya nguvu ya Mwenyezi Mungu haiwezekani.. Tunaweza Kupata tume huru kwenye makaratasi lakini Kupata tume huru kiutendaji ni Kazi ngumu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark, p

Haya ni maswali ya msingi sana.

Hebu niyajibu kadiri ya ufahamu wangu, moja baada ya jingine:

SWALI: Hiyo tume itaundwa wapi?

JIBU: Tume itaundwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo, Bungeni ndio mahali mwafaka. Lakini, safari ya kufika Bungeni inaweza kuanzia mahakamani, kama kutakuwepo na haja ya kupata amri/mwongozo wa Mahakama.

SWALI: Mswada utapelekwa na nani?

JIBU: Muswada wa sheria ya kufanya mageuzi kwenye sheria za NEC na Katiba ya Nchi, unaweza kupelekwa Bungeni na mbunge yeyote wa CDM kama hoja binafsi au ukapelekwa na mwanasheria mkuu wa serikali kama hoja ya serikali. Kunahitajika mchakato wa ushawishi na utetezo kumfanya mwanasheria wa serikali akubali kubeba hoja hii.

SWALI: Mswada utaandaliwa na nani?

JIBU: Muswada wa sheria ya kufanya mageuzi kwenye sheria za NEC na Katiba ya Nchi, unaweza kuandaliwa na mbunge yeyote wa CDM kama hoja binafsi au ukaandaliwa na mwanasheria mkuu wa serikali kama hoja ya serikali. Kunahitajika mchakato wa ushawishi na utetezo kumfanya mwanasheria wa serikali akubali kuandaa muswada huu.

SWALI: Mfumo WA maoni ya wadau utazingatiwa vipi na nani [atayakusanya]?

JIBU: Maoni ya wananchi tayari yanafahamika kupitia Tume ya jaji Warioba, Tume ya jaji Nyalali na Tume ya Jaji Kipenka. Kinachohitajika ni desk-reserach pekee.

SWALI: Je, wanadau na wabunge wanajua tume tunayoitaka [au Tume inayotakiwa]?

JIBU: Sio wadau wote wanajua Tume inayotakiwa. Lakini, ripoti za Tume ya jaji Warioba, Tume ya jaji Nyalali na Tume ya Jaji Kipenka zinatoa mwanga kuonyesha aina ya Tume inayotakiwa kulingana na maoni ya wananchi waliotoa maoni yao. Bandiko langu hapa na makala za waandishi baki tayari zimetoa fursa kwa umma baki kujua muundo wa Tume unaotakiwa na wananchi hao.

SWALI: Ninyi wapinzani mna majority ya kupitisha jambo linalichefeua serikali na dola yake?

JIBU: Kwa mujibu wa party caucuses tulizonazo, wapinzani hatuna majority ya kupitisha muswada wa Tume huru. Lakini, endapo Bunge litabeba hoja hii kama hoja ya kitaifa, badala ya kuichukulia kama hoja ya wapinzani, majority support itapatikana Bungeni. Kuna kazi kubwa ya ushawishi na utetezi inahitajika hapa. Na kama kazi ya ushawishi na utetezi haitafanyika vizuri, huenda kipengele hiki kikawa ndio show stopper!

SWALI: Mnaweza kuwabadilisha wabunge vilaza WA ccm kufikiri kama binadamu WA taifa hili?

JIBU: Uwezo wa kuwabadilisha kwa hoja zenye ushahidi (logical appeal) tunao. Uwezo wa kuwabadilisha kwa hoja zenye hisia (emotional appeal) tunao. Na bahati nzuri wabunge wa CCM wanaofikiri kiitikadi hawazidi 49% ya wabunge wa CCM. Uwezo tunao, nia tunayo na sababu tunazo.

SWALI: Mnaweza kuunda tume huru kwa dikrii ya rais?

JIBU: Hapana, Tume Huru haiwezi kuundwa kwa decree ya Rais kwa kuwa Tanzania ni Jamhuri. Bunge lazima lifanye kazi yake kwa niaba ya umma.

MWISHO:

Kuna swali ambalo hujauliza. Ni hili: Je, nyie wapinzani mnayo fedha kwa ajili ya kuendesha kampeni ya mageuzi katika Tume ya Uchaguzi kama maswali hapo juu yanavyoonyesha?

Jawabu langu ni rahisi. Nimemsikia Mbowe anasema kuwa ajanda hii ni kipaumbele chake cha kwanza. Huenda ameshafanya mchanganuo wa kibajeti na kuendesha harambee ya kutafuta fedha inayohitajika.

Ni maoni yangu kuwa kiasi cha TZS 1,000,000,000/= zinahitajika ili kufanikisha ajenda ya Tume Huru ya Uchaguzi. Yaliyotokea juzi wakati wa kulipa faini ya viongozi waliofungwa yanaonyesha kuwa Freeman Mbowe anao uwezo wa kutafuta fedha hizi kwa haraka. Tunaomba mchango wako Mhe. Ramark!
 
Kwa nchi Zetu hizi za Kiafrika, Kupata Kitu huru ndani ya nchi ambayo sio huru, ni Kazi ngumu Kama kutarajia Kupata Mtoto wakati hauna kizazi yaani namaanisha bila ya nguvu ya Mwenyezi Mungu haiwezekani.. Tunaweza Kupata tume huru kwenye makaratasi lakini Kupata tume huru kiutendaji ni Kazi ngumu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umeandika, "Tunaweza Kupata tume huru kwenye makaratasi lakini Kupata tume huru kiutendaji ni Kazi ngumu mno."

Nafurahi kwamba umeongelea ugumu na sio kutowezekana. Yaani unakubali kuwa inawezekana kupata Tume huru kiutendaji. Sasa basi, tueleze ni kwa nini unafikiri inawezekana kupata Tume huru kiutendaji. Hiyo ndio pointi muhimu katika bandiko hili.
 
Back
Top Bottom