Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Kwa hiyo tufanye rafiki?
Cha msingi ni kushinikiza kuanzia asasi za kiraia, taasisi zinazohusika na haki ya binadamu pia vyombo vya kimataifa vinavyopenda kuona demokrasia ya kweli, haki sawa na uhuru kupiga kelele kwa pamoja kushinikiza tume huru.

wananchi wanna nafasi yao ambayo ni adhimu na adimu ni swala la muda tu.
 
Cha msingi ni kushinikiza kuanzia asasi za kutaka, taasisi zinazohusika na haki ya binadamu pia vyombo vya kimataifa vinavyopenda kuona demokrasia ya kweli, haki sawa na uhuru kupiga kelele kwa pamoja kushinikiza tume huru.
wananchi wanna nafasi yao ambayo ni adhimu na adimu ni swala la muda tu.

Inputs taken.
 
Nikuulize jambo moja la ufahamu: kwa kuzingatia uzoefu wako wa kitaifa na kimataifa, yamkini ya kufanikiwa kwa muswada binafsi unaopelekwa bungeni ni kubwa au ndogo kiasi gani?[/QUOTE]




Ni matumaini hilo swali tayari umelijibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika, "Tunaweza Kupata tume huru kwenye makaratasi lakini Kupata tume huru kiutendaji ni Kazi ngumu mno."

Nafurahi kwamba umeongelea ugumu na sio kutowezekana. Yaani unakubali kuwa inawezekana kupata Tume huru kiutendaji. Sasa basi, tueleze ni kwa nini unafikiri inawezekana kupata Tume huru kiutendaji. Hiyo ndio pointi muhimu katika bandiko hili.
Asante, nitakujibu nikipata Wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama Amon, Kabla ya kuchangia.

Swali LA mwisho.

Muda unatosha?
Au unakubali kuwa tume si muhimu kuliko bunge?


Si lazima mama amon mtumishi WA mahakama na mama WA rafiki zangu jack na betha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark,
Mradi wa mageuzi ktk Tume unahitaji mwezi mmoja tu. So, muda unatosha.

Mradi wa mageuzi ktk Bunge sijautafiti na hivyo siwezi kuujadili kwa ufanisi. Nakuachia weww
 
Mradi wa mageuzi ktk Tume unahitaji mwezi mmoja tu. So, muda unatosha.

Mradi wa mageuzi ktk Bunge sijautafiti na hivyo siwezi kuujadili kwa ufanisi. Nakuachia weww
Samahani
Kivipi only one month tupe plan tuone utekelezaji wake kama utafaa

Usijali counter attack hawawezi maana wanaamini haliwezekani kama mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni matumaini hilo swali tayari umelijibu

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana. Sijalijibu. Nataka kujua: ukitafuta relative frequency ya hoja binafsi bungeni na hoja za serikali, uwiano ukoje kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, tuseme? That is my question to you, sir.[/QUOTE]Sawa,
Miaka mitano inakwisha hatuna hoja binafsi kutoka vyama vyote.
Nakumbuka 2010-2015 zito alipeleka mswada binafsi WA zao LA katani kama sikosei kwa bahati mbaya baada ya kusomwa hoja haikuungwa mkono hivyo ikatupwa.

House of Commons pale UK wanakanuni tamu ya miswada binafsi ambayo inatoa nafasi kupitia kura za wabunge na kupeleka taarifa kama sikosei
Na mswada unaposomwa bungen hujadiliwa kwa kupata 25 ya wabunge ili ijadiliwe then ipitishwe au ifanyiwe marekebisho ipitishwe
Hivyo hoja ikishaungwa mkono haitupwi itatengenezwa inavyotakiwa kisha kura. Hata serikali imekuwa ikiwatumia wabunge wenye nafasi hizo ili kupitisha jambo kwa haraka bila majadiliano makali.

Naamin wapinzan wanamajibu mazur na ndiyo maana hakuna miswada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani
Kivipi only one month tupe plan tuone utekelezaji wake kama utafaa

Usijali counter attack hawawezi maana wanaamini haliwezekani kama mimi

Sent using Jamii Forums mobile app

TANZANIA' S NEC TRANSFORMATION PROJECT


IMPACT
- more freedom to nec achieved

OUTCOMES
- nec accountable to parliament
- nec bosses endorsed by parliament
- nec officers deployed at lga level without outsourcing public servants
- nec budget funded from consolidated fund

OUTPUTS
- Bill drafted (expert workshop)
- bill marketed to mps, civil society, faith based organisations and general public (workshops and media campaigns)
- bill tabled in parliament, passed and signed into law
- narional nec team recruited
- local nec team recruited

ACTIVITIES
- as per outputs above

WORKPLAN

- one week for drafting bill
- one week for ministerial consultations
- one weeks for marketing bill to non-mps and mps
- one week for debating the bill
- one week for signing the bill into law
- one month for recruiting and endorsing nation nec team
(Total 2 months)

BUDGET
- to be determined

HAPO VIPI?
 
Wakati tunasubir majibu ya mama among katika swali langu,
Tuendelee kidogo kudadavua majibu ya maswali ya awali

Mwanasheria Mkuu WA serikali ni mtendaji kwa mujibu WA ofisi, ni wazir kivuli katika cabinet ya mawaziri, ni mbunge lkn pia mwanasheria WA bunge na bado ni serikali bungeni.

Anaweza kuibeba hoja hii hadi bungeni -----:- jibu n hapana, atajayeipeleka bungeni ni baraza LA mawaziri kupitia waziri WA katiba.

Upo muda WA kufanya desk research na tume ya kubadili sheria? Ofisi ya mwanasheria Mkuu WA serikali na wizara ya katiba na sharia halafu uandaliwe mkutano WA baraza?
Itengewe muda bungeni, na kamati kuipitia, sawa inawezekana kwani hata 2015 tuliunda sharia kupitia ya hoja ya dharura. Lkn tumeshapata maridhiano ya kitaifa?
Rais na baraza lake wanainterest na hili?
Lkn tukumbuke bunge linavunjwa na rais mwishoni mwa June au mwanzoni mwa July, bunge LA hovyo kabisa. Yaani sehemu ya nchi inaondoka mpaka itakapoitwa na rais kwa dharura au atakapoliunda tena. Upuuzi kabisa

Bunge likishavunjwa biashara ndiyo imekwisha maana tunakwenda rasmi kwenye uchaguzi .

Kwa muda uliobaki tutaipata hiyo tume ambapo sheria itungwe na bunge KISHA kurudi majina kupigiwa kura na wabunge then tume iunde timu za majimbo kisha iratibu taratibu za uchaguzi tutawahi muda WA kikatiba rais kukaa madarakani kabla ya uchaguzi?

Na muda tulionao tayar induced demand imetawala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramark,
Hello, tayari workplan yangu hiyo hapo juu. It can be accomodated in April to June parliamentary sessions
 
Mama Amon, Woow
Safi sana

Unaonaje cdm tangu mwanzo wangenadi mswada unaopendekezwa?

Mswada kama huu bungeni hauhitaji wiki nzima unahitaji hata siku moja tu kupitishwa kulingana na ulivyoandaliwa na utavyonadiwa.

Nani atabeba huu mswada kwenda kwenye cabinet?

Nani atawashawishi wabunge ccm? Wakati bosi ni waziri Mkuu ?

Nani ataupeleka hasa bungeni? Atakayepeleka ndiye ataamua kupita au kurudi.

Binafsi nashauri
JF tuandae huu mswada kupitia mawazo ya humu ya threads zingine. Then tuikabidhi kwa wenyeviti WA vyama vyote vya siasa, taasisi kuu za dini, azaki na vyuo vikuu bila kusahau vyombo vya kisheria vya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina tatizo na ccm kupiga kura, shawishini hata vyama vyote vishiriki, lakini wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kushiriki uchaguzi wa kihuni, ambao rais na chama chake wanaingia kwenye uchaguzi na matokeo mfukoni. Hakuna mtu anayejiheshimu atashiriki huo uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi. Kwa maneno marahisi, huo uchaguzi wa bila tume huru ya uchaguzi ni sehemu ya kuonea ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka.
Mkuu tindo

Tulisha andika sana juu ya hili jambo la "kushiriki au kutoshiriki kupiga kura."

Naelewa unajua ninaposimamia juu ya hili.

Hii ya kususa na kukaa nyumbani, kwa kutegemea tu hao washindi waone aibu eti kwa kutopigiwa kura na baadhi (hata kama ni asilimia 90 ya wapiga kura) ambao walisusa wajibu wao huo sioni kabisa manufaa yake.

Chaguo langu la kwanza, unalijua. Uchaguzi usiwepo kabisa bila ya kuwepo tume huru. Hata kama ni asilimia 30 tu ya wapiga kura wakikataa kupiga kura na kuzuia uchaguzi kuendelea, uchaguzi huo hautafanyika.

Watu hawa wapo sasa hivi, ni kiasi tu cha kuwepo uongozi wa kuwaongoza na kusimamia mipango yote itakayofanikisha kazi hiyo kufanyika kwa ufanisi mkubwa.

Hawa wakishadhamiria kuuzuia uchaguzi usifanyike, hapo ndipo utakapoona watu wengi zaidi wakiunga mkono jambo hili.
Lakini ni lazima pawepo na uongozi kusimamia juhudi zote za zoezi hilo.

Kama unaendelea kuwa na mashaka na uwezo wa raia kuzuia uchaguzi usifanyike, wazo la pili linakaribiana na hilo lako lakini ni tofauti sana na hilo la kusussia uchaguzi na kuruhusu CCM ishinde hata kwa kupata kura hamsini elfu.

Kwenye wazo hili, wanasiasa wote, hata walioko CCM wasiopendezwa na haya mambo ya CCM ya Mwenyekiti (nina hakika unajuwa wapo wengi sana, hata kama hawataki wajulikane bayana), wawahimize wananchi wajitokeze kwa wingi sana kwenda kupiga kura ya HAPANA; kukataa kabisa utawala huu kuendelea miaka mitano mingine.

Kura hizo zikishapigwa, hata watawala wakilazimisha ushindi, hawana njia yoyote ya kuzuia matokeo halisi yasijulikane.

Hii ndiyo AIBU, kushinda hiyo unayoisimamia ya kususa, itakayowaondolea uhalali wa aina yoyote ya kujifanya wanatawala kwa ridhaa ya wananchi.

Dunia nzima itajua utawala wao ni wa kulazimisha, kwa sababu ushahidi bayana upo. Kutokwenda kupiga kura ni halali kabisa kwa watawala kuendelea kukaa madarakani.

Mkuu tindo, naomba tafadhari unisome kwa makini unielewe nilichoandika hapa, na kama bado kwa dhati ya moyo wako bado huuoni unafuu wa njia hizi ukilinganisha na hiyo yako, basi tutaliachia jambo hili hapa, na kamwe sitajisumbua tena kujaribu kukushawishi vinginevyo..
 
Ingekuwa vyema kama ungeambatanisha waraka tajwa, ningetafuta muda niusome, labda contents zake zinaweza zikawa zinamsukuma msomaji kuukwepa kuujadili na hivyo kutafuta ya kujadili kutoka kwingine
Wazo lililoniijia akilini mara ya kwanza kabisa nilipoisoma mada yake hii; lakini nikaona labda alikuwa na sababu maalum zilizofanya asiuweke waraka wenyewe hapa.

Wazo linalokuja kwa msomaji wa yaliyowekwa kwenye mada ni kana kwamba huu waraka wa Maaskofu wa Tanzania umenakiriwa tu kutokana na hiyo ya Zambia na Kenya, jambo ambalo sidhani kuwa wanaweza wakalifanya hawa Maaskofu wetu hapa.

Jambo la pili. Ni vigumu kujua ni kiasi gani cha mchango uliofanywa na Nyaraka hizo mbili, Kenya na Zambia katika kuleta matokeo ya chaguzi zao, mbali ya uhusika wa mambo mengine mbalimbali yaliyokuwepo katika nchi hizo.

Kwa mfano Kenya. KANU na Moi kama kichocheo cha wananchi kukataa wote wawili (Kenyatta ulikuwa mpango wa Moi, ijulikane hivyo).

Hapa kwetu ni CCM ndiyo 'constant', hawa wengine - Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli..., inafanya hali iwe tofauti kidogo na ile hali ya Kenya.

Mwai Kibaki pekee, angechuana na Kenyatta, hakuna anayejua matokeo yangekuwa vipi pamoja na uwepo wa waraka huo. Wapiga kura, hasa Kikuyu, wangegawanya kura zao pande mbili.

Lakini kuingia kwa "Kibaki Tosha" ya Odinga ilibadili kabisa hali ya uchaguzi huo.

Kwa hiyo, tusitegemee sana uwepo wa waraka kuwa ndio unaoweza kuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko. Ni lazima pawepo na mambo mengi mengine ambayo yanawafanya wapiga kura kuamua ni wapi kura yao waielekeze.
 
Kalamu1,
Sorry rafiki. Usijadili bandiko langu kwa kuanzia ktk comment ya msomaji. Usome bandiko kwanza na kuelewa.

Hata majibizano kati yangu na huyo unayemjibu hujayasoma. Niliona comment yake na kuifanyia kazi.

Waraka wa TEC nimeshauweka ktk marejeo. Na mtajo wa Kenya na Zambia hauna mahusiano na hoja kuu ya Maaskofu wa TEC.

Soma vizuri. Ukiridhika ufute uzi wako huu ili usipotoshe wasomaji baki. Mwisho usisahau kuwa online contents ni dynamic.

Mf, kule mwisho bandiko langu lina timestamp ya march 21 mara tu baada ya reference unayosema hujaiona.

Ongeza umakini.
 
Back
Top Bottom