Sina tatizo na ccm kupiga kura, shawishini hata vyama vyote vishiriki, lakini wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kushiriki uchaguzi wa kihuni, ambao rais na chama chake wanaingia kwenye uchaguzi na matokeo mfukoni. Hakuna mtu anayejiheshimu atashiriki huo uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi. Kwa maneno marahisi, huo uchaguzi wa bila tume huru ya uchaguzi ni sehemu ya kuonea ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka.
Mkuu tindo
Tulisha andika sana juu ya hili jambo la "kushiriki au kutoshiriki kupiga kura."
Naelewa unajua ninaposimamia juu ya hili.
Hii ya kususa na kukaa nyumbani, kwa kutegemea tu hao washindi waone aibu eti kwa kutopigiwa kura na baadhi (hata kama ni asilimia 90 ya wapiga kura) ambao walisusa wajibu wao huo sioni kabisa manufaa yake.
Chaguo langu la kwanza, unalijua. Uchaguzi usiwepo kabisa bila ya kuwepo tume huru. Hata kama ni asilimia 30 tu ya wapiga kura wakikataa kupiga kura na kuzuia uchaguzi kuendelea, uchaguzi huo hautafanyika.
Watu hawa wapo sasa hivi, ni kiasi tu cha kuwepo uongozi wa kuwaongoza na kusimamia mipango yote itakayofanikisha kazi hiyo kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Hawa wakishadhamiria kuuzuia uchaguzi usifanyike, hapo ndipo utakapoona watu wengi zaidi wakiunga mkono jambo hili.
Lakini ni lazima pawepo na uongozi kusimamia juhudi zote za zoezi hilo.
Kama unaendelea kuwa na mashaka na uwezo wa raia kuzuia uchaguzi usifanyike, wazo la pili linakaribiana na hilo lako lakini ni tofauti sana na hilo la kusussia uchaguzi na kuruhusu CCM ishinde hata kwa kupata kura hamsini elfu.
Kwenye wazo hili, wanasiasa wote, hata walioko CCM wasiopendezwa na haya mambo ya CCM ya Mwenyekiti (nina hakika unajuwa wapo wengi sana, hata kama hawataki wajulikane bayana), wawahimize wananchi wajitokeze kwa wingi sana kwenda kupiga kura ya HAPANA; kukataa kabisa utawala huu kuendelea miaka mitano mingine.
Kura hizo zikishapigwa, hata watawala wakilazimisha ushindi, hawana njia yoyote ya kuzuia matokeo halisi yasijulikane.
Hii ndiyo AIBU, kushinda hiyo unayoisimamia ya kususa, itakayowaondolea uhalali wa aina yoyote ya kujifanya wanatawala kwa ridhaa ya wananchi.
Dunia nzima itajua utawala wao ni wa kulazimisha, kwa sababu ushahidi bayana upo. Kutokwenda kupiga kura ni halali kabisa kwa watawala kuendelea kukaa madarakani.
Mkuu tindo, naomba tafadhari unisome kwa makini unielewe nilichoandika hapa, na kama bado kwa dhati ya moyo wako bado huuoni unafuu wa njia hizi ukilinganisha na hiyo yako, basi tutaliachia jambo hili hapa, na kamwe sitajisumbua tena kujaribu kukushawishi vinginevyo..