UTV Acheni Unafiki. Habari zenu hazina mizania

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
UTV haijawahi kuripoti chochote kuhusiana na mikutano ya CHADEMA inayoendeshwa na Tundu Lissu. Leo wameripoti kuhusiana na kukamatwa kwake.

Hawa hawa UTV hawajawahi kuripoti kuhusiana na waraka pendwa wa TEC badala yake wakawa wanatafuta watu wenye maoni ya kupinga waraka ambao hawajawahi kuusoma.

Nawaomba UTV kama wameamua kuto ripoti habari za wakosoaji wa serikali ya awamu ya 6 basi wasiripoti kabisa sio wana donoa donoa.

Pia huyu Nape Nnauye inabidi ajitafakari sana tena sana.

Pongezi kwa Online media kama JamiiForums na Jambo TV
 
Hivi vyombo vya habari na wanahabari wanafiki, inabidi kuvisusia vyombo vyao na wanahabari njaa wao.

Uanahabari ni kati ya tasnia hovyo kabisa zinazoendeshwa na watu wasiojitambua wala kuuthamini utu wao.
 

Wala usiwalaumu, ni vyombo vyote viko under certain rules.
Waki play out of watafungiwa or kupigwa fine kubwa
 
Kwani lazima?
 
Azam Media ni Kenge tu
 
Hivi kwanini tunalalamika juu ya uhuru wa mfanyabiashara? Kwani unaamini kuna UHURU wa mwandishi dhidi ya matakwa ya mfadhiri? Yaani mwandishi aandike habari inayotishia kibarua chake? Wewe ungeweza? Umma haupewi kila habari ila ile iliyoamriwa tu.
 
Azam ni kama TBC 1; contents zao ni kizimkazi, kisiwandui, uchumi wa buluu, na upuuzi mwingine kama huo.
 
Nashaur CDM waanzishe media platforms, TV station, radio station and the likes, kutegemea vyombo vya hbr vinavyofuata maagizo mtachelewa kuwafikishia wananchi hbr na matukio!!
 
Hao ni Kojani gangs and hata movi zao nying especially tamdhilia zao ni za kidini zaidi wapowapo tuu hata sijui wanataka nini ,nawazaga labda bosi wao ni wa kule Kimimkazi soo ametoa maelekezo
 
Mfanyabiashara makini anaelewa na kujali flow ya audience na mapato yake.Anafuata ni nini watazamaji wanachopenda kusikia na kuona.Hamlazimishi mtazamaji yeyote kutune tv yake kwa hiyo mlalamikaji ana uhuru wa kuchagua chanel anayoyoipenda kwa sababu remote iko mkononi mwake.
 
Hao ni waislamu.
 
Hata ITV nimeshangaa wametangaza kukamatwa kwa Lissu, ila mikutano yake hawakutangaza. Yani Tanzania uchawa hautaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…