Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Mfumo wa TAUSI ambao unanunua viwanja moja kwa moja serikalini una uzuri na ubaya wake. Ni mara ya pili sasa najaribu kununua viwanja ambavyo vimeandikwa viko manispaa ya Kinondoni na navikosa. Mara ya kwanza ilikuwa mwezi wa tano kama sio wa nne mwaka huu ambako vilitangazwa viwanja Mabwepande nikaingia kwenye mfumo, muda wa kuuza nikakuta vyote vimeshanunuliwa.
Juzi kati hapa wametangaza vingine Mabwepande vilikuwa viwili ambavyo leo ndio dirisha ilibidi lifunguke. Muda wa soko mtandao ukawa unazingua, hadi muda ukapita viwanja vikjawa havipo.
Najiuliza mbona viwanja vingine vipo kwanini hali iwe tofauti kwa viwanja vilivyoko Dar tu. Kuna mchezo?