UV-CCM na Vijana wa CCM mmelala sana katika mitandao ya kijamii, mko wapi?

UV-CCM na Vijana wa CCM mmelala sana katika mitandao ya kijamii, mko wapi?

mie nakataa post za ccm ni kidogo sana kwenye mitandao ya kijamii.Ushawishi ni muhimu kila kona hata kama ni kupost picha za wagombea wa ccm tu nalo linatia hamasa jamani.Tusije na hoja nyepesi jitokezeni mtetee chama kwa mazuri yaliyofanyaka kwa miaka mitano ya JPM
 
Mnachokipuuza ndicho kinachowapeleka shimoni japo ukweli ni kwamba, katika kila vijana 100 uvccm ni 10 tu huku ndani ya hao kumi waliokunywa maji ya bendera ni wawili tu.
Kibaya zaidi hawaonekani sababu jiwe hauziki, habebeki, amechokwa vibaya sana na watanzania alafu kibaya zaidi akiwa kwenye majukwaa anaongea utumbo utadhani kalogwa au hana akili timamu.
Sasa mtu kama jiwe utakuwa na hoja gani ya kumtetea hata kama umejitoa ufahamu? Katika eneo nilipo hapa Arusha mtu aliyenivutia na mwenye hoja ni diwani tu! Mrisho gambo pamoja na magufuli nawaonea kinyaa
Kama kawaida yetu CCM, hatujibu "mere allegations". Sisi tunatumia mitandao kuomba kura. Na tutazipata na tutashinda.
 
Huyu mtu aliyekuja kutoka huko Ubeleji,si wa kawaida,yuko kama nyati aliyejeruhiwa.
Ana hoja zilizoshiba,wala hazijibiki,ana ujasiri wa kusema ukweli bila kuogopa kitu chochote hata JIWE,anazifahamu sheria vizuri kuliko hata hao waliozitunga,na anakubalika kwa wananchi wote isipokuwa UVCCM,POLICCM,NECCCM NA TISSCCM.
Na mwisho amedhamiria kuvunja kofuli la ikulu na kuimwaga pombe yote na kuukomesha kabisa ULEVI wa madaraka kwa kuandika katiba mpya.
Na wao wanamkubali sema njaa na kujipendekeza hawana namna..naamini kabisa watampigia kura TAL mana kura ni siri mana na wao wanataka ukombozi.

#MaendeleoHayanaChama



Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mbona kila siku Elitwege na wenzao wako humu wakiwachafua TL na Chadema?

Vv
 
Mgombea wa ccm hana mvuto ndiyo maana hata uvccm wanashindwa kumtetea. Akipqnda jukwaani anaanza kukoroma kama vile kapandwa na majini..."Nileteeeni Gwajima × 4"

Gwajima atakuwa mbunge wa kawe hilo halina ubishi. Upende usipende, Halima Mdee na cdm walibweteka na kukosea kusimamisha mgombea urais ambaye ni kibaraka.

Mikutano ya Lissu yote angalia akizungumzia jambo la kumshambulia Mh Rais JPM moods za wanaomsikiliza zinabadillika na wanabakia kumshangaa.Ni ungane na Polepole hakukosea, hao wanaoenda kwa Lissu ni kushangaa msukule.

Lakin huyu shehe Ponda kammaliza Lissu kwa kauli yake ya kusema kura zote za waislamu wamekubaliana ziwe kwa Lissu. Ponda alichaguliwa lini kuwa ndiye msemaji wa Waislamu wote wa Tanzania?

Lissu najua ni zuzu flani hivi kafurahia kauli ile yaPonda akifikiri ndio kapata. Na uzuzu wa Lissu ukiendelea kuendekezwa sijui Taifa hili litaishia wapi? Hivi ni kweli kuwa hatari ya Lissu na mieyendo yake canot be anticipated? Na naomba Lissu umuulize Ponda anajua kuwa kuna kura za Wakristo wa Tanzania na siasa haichangamanishwi na udini? Alitumia uhalali gani kuwaapisha watu wa imani nyingine ya tofauti na Sheikh Ponda. Anajua alichofanya ni usumbufu usio wa lazima kwa watu wa imani nyengine tofauti na yeye?
 
Nimekuwa nikifatilia sana juu ya post mbalimbali za vya vyama vya siasa katika mitandao ya kijamii.Kila post ni vyama vya upinzani tu.

Habari za Tundu Lissu zimetamalaki kila kona sasa najiuliza vijana wa UV-CCM mko wapi ? Hampo kabisa katika mitandao ya kijamii hususani Faceboo,Tweeter na mitandao mingine ya kijamii ikiwemo Jamii Forum.

Tunahitaji habari mbalimbali za chama katika mitandao ya kijamii hasa niliyohitaja.

CCM tumelala sana,tunahitaji kupost habari mbalimbali za chama katika mitandao na hakuna kuwaachia upande wa pili kujitawala katika mitandao.

Upotoshaji umetawala sana na watu wa kujibu upotoshaji huo ni CCM na timu yake hasa UVCCM.

TUSILALE JAMANI HUKU NDO KAMPENI ZILIKOHAMIA
Tuandike Nini hasa? Baba zetu ambao ni wajumbe waliwakataa wagombea ambao wanawafahamu lakini mwenyekiti kawarejesha kwa wajumbe as if wao hawakutumia busara! Tuandike juu ya dharau hii kwa wajumbe?

Mwenyekiti anajinadi kwa wapigakura ambao walichagua upinzani na kuwapa za uso kuwa hakuleta na hataleta mradi wa maendeleo eneo Hilo! Hapa anafunja katiba ya nchi aliyoapa kuiishi na kuilinda, hapa namteteaje?

Mwenyekiti wetu wa uv-ccm anatangaza Vita z na kuhamasisha umwagaji wa damu Kama Jana akisema watamchoma mgombea Fulani sindano ya sumu. Huyu haguswi na hataguswa na dola kwani ana wa kumtetea, Mimi uv-ccm mwenzake nikitetea na kuyatamka haya so nitapotelea segera?

Sioni jinsi ya nikitetea chama changu!
 
Wanaekesha wakimtetea na kumpigania habebeki kila siku anashusha vihoja na viroja hadharani ambavyo hata wao vinawaacha midomo wazi.
 
Watakaoipigia kura CCM mwaka huu ni wagombea walioteuliwa kupeperusha bendera katika viti vya ubunge na udiwani na familia zao, viti maalumu wanaosubiri kuapishwa, na familia zao, TISS maana hawa ni CCM B, na wa mikoa na wakuu wa wilaya wachache na familia zao, hata baadhi ya wateuliwa wa Magu hawatompigia kura magu maana wameishi roho mkononi kwa miaka yote mitano, hawana hamu nae wanamchekea usoni tu. Hili ndio kundi pekee ambalo CCM wana uhakika na kura zao.

Makundi mengine inahitaji mtu uwe kichaa ndio uipigie kura CCM.
 
Tarime, Tanzania

Ilani ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu imekubalika na kueleweka. Ilani hii ni mtambuka na inafafanuliwa kwa wepesi kabisa :

 
Back
Top Bottom