UV-CCM na Vijana wa CCM mmelala sana katika mitandao ya kijamii, mko wapi?

UV-CCM na Vijana wa CCM mmelala sana katika mitandao ya kijamii, mko wapi?

View attachment 1604206

Nimekuwa nikifatilia sana juu ya post mbalimbali za vya vyama vya siasa katika mitandao ya kijamii. Kila post ni vyama vya upinzani tu.

Habari za Tundu Lissu zimetamalaki kila kona sasa najiuliza vijana wa UV-CCM mko wapi ? Hampo kabisa katika mitandao ya kijamii hususani Faceboo,Tweeter na mitandao mingine ya kijamii ikiwemo Jamii Forum.

Tunahitaji habari mbalimbali za chama katika mitandao ya kijamii hasa niliyohitaja.

CCM tumelala sana,tunahitaji kupost habari mbalimbali za chama katika mitandao na hakuna kuwaachia upande wa pili kujitawala katika mitandao.

Upotoshaji umetawala sana na watu wa kujibu upotoshaji huo ni CCM na timu yake hasa UVCCM.

TUSILALE JAMANI HUKU NDO KAMPENI ZILIKOHAMIA
Wewe Umekuja Huku umetuletea majibu gani?? Au hujui kuwa tunasubiria majibu ya hoja nyingi zilizotolewa na TL kwenye Kampeni zake??

Haya Tujibu

1) Kwanini mnauza vitambulisho feki vya wajasiliamali na mbaya zaidi hamtoi risiti??

2)Je fedha mnazokusanya kwenye hivyo vitambulisho mnaziweka kwenye kasma gani/account gani?? Huo sio wizi??

3) Kwanini mlipeana tenda ya Kujenga uwanja wa ndege ya Chato kindugu?? Huo sio ufisadi?

4) Trillion 1.5 alizosema CAG zimepotea je zipo wap??

5) Wapi Benny Saanane, Azori na wengine wengi??

6) Kwanini hamuwapeleki Mahakamani Masheikh waliopo Magerezani Kwa miaka sita sasa?

7) Kama mmejenga nyumba za Marais wastaafu Kwa ajili ya kutekeleza takwa la kisheria, je Kwanini hamtekelezi takwa la kisheria la kuwapa nyongeza ya mwaka ya mishahara ya watumishi wa Umma Kwa miaka mitano sasa?

Wewe unadhan wenzako waliotepeta ni wajinga?? Hawana majibu ya msingi ya hoja hizi. Haya tunaomba majibu.
 
Kwa mfano nilitenga siku ya jana tarehe 18 October kuhakikisha nashawishi watu 50 watakao chagua Rais,Mbunge,madiwani kutoka CCM.
mpaka kufikia saa nne usiku nilifanikiwa kuzungumza na watu 65.
kati ya hao watu 65 nimefanikiwa kuwashawishi watu 43 wote wamekubali kubadili mtazamo na kuiamini CCM,nimebadilishana nao namba za simu na wote nimewaunga kwenye group la vijana wazalendo wa CCM.

hili zoezi nina wiki ya nne sasa nalifanya kila j'pili kila ninapoingia mitaani kushawishi watu napata mafanikio makubwa sana.
 
Siku hizi malipo yao yameota mbawa ndio maana hawaonekani online.
 
Back
Top Bottom