UV-CCM na Vijana wa CCM mmelala sana katika mitandao ya kijamii, mko wapi?

Wamechoka na kulegea kwa kutetea hoja zisizobebeka kwa miaka mitano 2015-2020.
Hoja gani hazibebeki. Awamu ya tano imefanya mengi bali kwa vipofu kama wewe ambao mlikuwa na maslahi mnaona tonge lenu limeondolewa mnawewesekaweweseka JPM hana mpinzani.
 

Tarehe 28 ndio utaanza kujua wako wako wapi😁😁😁😁
Siasa ni sayansi
Maendeleo hayana vyama
 
Walikuja na propaganda za miradi ya kimkakati watu wamewapuuza
Hujaona hata mgombea wao siku alipozindua kampeni dodoma akajigamba nimenunua ndege 11 mkinichagua tena nitanunua ndege nyingine 5 na ya mizigo moja baada ya hapo hajarudia tena cha moto amekipata
 
Ccm wapo tbccm na channeltenccm, na bahati mbaya sana huko watu hawazitazami tena hizo channel maana zinatangaza habari zilizochacha, hazipendwi na wala hazina mvuto, kila siku tu jiwe,jiwe,jiwe,jiwe!
 
UVCCM wamepotea hakuna hazina za hotuba za vijana wa mtaa wa Lumumba 2015 - 2020 ktk maktaba kwa ajili ya rejea-tajwa kama za kwetu BAVICHA

MHE PATRICK OLE SOSOPI AKIHUTUBIA KAMATI TENDAJI YA BAVICHA TAIFA​

 
9 Jul 2020
Kampeni ya BAVICHA TOKOMEZA CCM 2020


Mwenyekiti BAVICHA Taifa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Butimba ndugu kamanda Comrade Mwl. John Pambalu, amekiomba chama chake cha CHADEMA kumpa ridhaa na udhamini ili na kusimama kama Mbunge kuwawakilisha katika Bunge lijalo wananchi wa jimbo la Nyamagana
 
..uv-ccm siyo wajenga hoja wazuri.

..wanadhani kutukana na kufokea ni ujanja wa kisiasa.
 
Mkuu vijana wa CCM wanapost kile cha muhimu tu. Hawapost kila kitu. Mfano, ebu angalia walichopost Chadema leo kuhusu kampeni za Lissu Babati halafu uniambie kuna kitu gani cha maana.
Mvua za juzi zimefuta kelele za "tumejenga miundombinu"
 
Mgombea wa CCM kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu hana jipya. Hauziki sokoni. Ndiyo maana unaweza kuona vijana wa mtaa wa Lumumba (Mataga) wamekuwa kama wamepigwa dilemma vile.
 
Kwenye mitandao ya kijamii wajinga Ni wachache.Sasa watamdanganya Nani?
 
Sie sio wajinga, kura haziko kwenye mitandao ya kijamii, tunapiga kampeni kwa wapiga kura, nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda! Hapa kwetu mwakasola na rufwisi hakuna hata smart kitochi
 
Hatunaga mda na mitandao sie tuko kitanda kwa kitanda nyumba kwa nyumba wala huo hapashawishi wapiga kura wetu,nyie kalieni kwenye mitandao lakin msije kusema mmeibiwa kura!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…