Uvaaji mpya wa wanawake kwenye misiba unatia aibu

Uvaaji mpya wa wanawake kwenye misiba unatia aibu

Unaambiwa msibani ndio sehemu pekee ya mtu kuonekana alivyo.

Mtu anajiuliza avae nguo gani na anaenda na Saluni kabisa.
 
Hayo mavazi yalihuzunisha kweli au yalipandisha mzuka wa ngono? Me ntasikitika labda nikiskia watu wamefariki kwenye ajali
 
Ahaa wachina wao wanagiza wacheza uchi kuburudisha wafiwa. Kwa maudhulio msibani waombolezaji nyomiii mi napenda wanatusahausha kama tunakufa nakuondoa sononeko moyoni
 
Wenzenu wanawapunguzia maumivu na masikitiko ya kupoteza kipenzi chenu, bado mnalalamika?! Kweli binadamu haridhiki aise..🙁😡😕😎
 
Kama upo kwenye Social.media na hamkumjua Kizzo bas tena..in short alikuwa activist, entrepreneur na mwanaharakati wa mabadiliko kwa vijana..n.k
Mnazingua mjuwe nyie maana kizzo insta alikuwa na followers 2K elfu mbili tu.
 
Jana tulikuwa tunamzika brother Kizzo huyu jamaa alikuwa mtu wa watu kweli kweli katika umri wake alioishi duniani amegusa watu wengi waliokuwepo msibani watanielewa.

Kila aliyesimama alisema Kizzo was a friend hata kina Milya, Lema, Nassary waliposimana walisema tumpoteza Rafiki. Kiukweli huyu jamaa alikuwa mtu poa sana kuanzia hometown Arusha hadi Dar.

Kero iliyojitokeza ni wanawake hasa waliotokea Dar es Salaam waliovaa kiaibu sana. Waligeuza msiba kuwa sehemu ya kutangaza viungo vyao.

Cha kushangaza hata Carol Ndosi ambaye ni mfiwa alivaa vibaya sana. Alivaa dera ambalo ni transparent tulikuwa tunaona hadi chupi iliyokuwepo ndani. Hii ilipelekea wanaume kuhamishia macho kwakwe kwa masikitiko.

Wadada wengi kwenye msiba wa jana walivaa nguo zinazoonesha mapaja na hii iliwahuzunisha sana Wazee wa Kimeru.

Wanawake wa Dar es Salaam msibani sio sehemu ya kuonesha fasheni za mavazi.
Usiseme watu wa Dar sema watu wa mikoani mliohamia dar
 
Tatizo lingine lipo kwa sisi tuendao msibani au eneo lisilohusiana na ngono tukiwa na mawazo ya ngono. Hii ni hatari sana ipo siku tutabakana hadharani wallah
 
Dunia inakwenda kulingana na wakati wake. Siku hizi kuvaa sare kwa wafiwa, ao kukodi watu kuja kulia msibani nijambo la kawaida sana.
 
Wazungu msiwahusishe kwa uvaaji. Wazungu wanajiheshimu sana uvaaji kwenye misiba si wanawake si wanaume. Kwa kweli wanavaa vizuri zaidi waendapo makanisani.
 
Wewe ujue kutofautisha watu wa dar na watu wa mikoani waliohamia dar!!.. nyinyi mliokuja dar ndio tatizo mnaiga kila kitu hadi ushoga!!.. huo msiba wenu ulijaa machalii wa kaskazini wamejiremba na kujipamba halafu unawaita wa dar!!.. miyeyusho sana nyinyi wakuja
Hata huku mjini wanaofanya mambo ya ajabu wengi wametoka mikoani sie wazawa hatuna tabu..
 
Back
Top Bottom