UVCCM yalaani Vikali Mauaji ya Michael Kalinga Mohammed Kawaida kwenda Mkoani Mbeya Kushiriki Mazishi yake hapo kesho

UVCCM yalaani Vikali Mauaji ya Michael Kalinga Mohammed Kawaida kwenda Mkoani Mbeya Kushiriki Mazishi yake hapo kesho

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali mauaji ya ndugu Michael Kalinga.

Ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM Tawi La Machinjioni Makongorosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .Ambaye mwili wake umekutwa umetelekezwa .baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana.

Ambapo jumuiya hiyo ya vijana umeliomba Jeshi la Polisi kufuatilia tukio hilo na mengine ya aina hiyo na kuwakamata watu wote wanaohusika na uhalifu huo na matukio mengine ya aina hiyo.

Katika hatua nyingine jumuiya hiyo katika taarifa yake imesema ya kuwa Mwenyekiti wake Wa UVCCM Taifa ndugu Mohammedi Kawaida atashiriki mazishi ya Ndugu Michael Kalinga.yatakayofanyika siku ya kesho nyumbani kwake Marehemu Makongorosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya
Screenshot_20241203-225419_1.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali mauaji ya ndugu Michael Kalinga.

Ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM Tawi La Machinjioni Makongorosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .Ambaye mwili wake umekutwa umetelekezwa .baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana.

Ambapo jumuiya hiyo ya vijana umeliomba Jeshi la Polisi kufuatilia tukio hilo na mengine ya aina hiyo na kuwakamata watu wote wanaohusika na uhalifu huo na matukio mengine ya aina hiyo.

Katika hatua nyingine jumuiya hiyo katika taarifa yake imesema ya kuwa Mwenyekiti wake Wa UVCCM Taifa ndugu Mohammedi Kawaida atashiriki mazishi ya Ndugu Michael Kalinga.yatakayofanyika siku ya kesho nyumbani kwake Marehemu Makongorosi Wilayani Chunya Mkoani MbeyaView attachment 3168383
Na hapa ndipo mpasuko unapo endelezwa, kwa sababu walipo uawa wana CHADEMA hakuja wahi tokea UVCCM wakakemea au kulaani, maana waliamini walio kufa ni sio binadamu kwa hiyo leo kafa mwenzao ndiyo wameona kumbe wanao kufa ni binadamu, hatuna wazee wenye hekima na busara walinusuru hili taifa kwenye hali hii maana tunako elekea kwambali naona kubaya sana
 
Na hapa ndipo mpasuko unapo endelezwa, kwa sababu walipo uawa wana CHADEMA hakuja wahi
UVCCM na CCM yote kwa ujumla wake imekuwa ikilaani na kukemea matukio ya aina hiyo.

Majuzi tu hapa Mwenezi wetu na msemaji mkuu wa chama chetu cha CCM Taifa Ndugu CPA Amos Gabriel Makalla amelaani vifo vya watu vilivyotokea wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia amekuwa akilaani sana mauji ya watu na kuagiza kufanyika kwa Uchunguzi
 
Matukio kama haya yatuunganishe kama Taifa na siyo kutugawa kwa kuangalia aliyekufa ni kutoka chama gani.

Kifo hakipaswi kuangaliwa kwa sura ya uchama.

Ni lazima tukemee na kupinga Umwagaji wa Damu ya watanzania au mtanzania yeyote yule asiye na hatia.
 
Matukio kama haya yatuunganishe kama Taifa na siyo kutugawa kwa kuangalia aliyekufa ni kutoka chama gani.Kifo hakipaswi kuangaliwa kwa sura ya uchama. Ni lazima tukemee na kupinga Umwagaji wa Damu ya watanzania au mtanzania yeyote yule asiye na hatia.
Lakini wewe hapa watu wakiuliwa na kutekwa Huwa unasema ni drama
Sasa tujifunze kushikamana
Maisha Yana thamani kubwa
 
Matukio kama haya yatuunganishe kama Taifa na siyo kutugawa kwa kuangalia aliyekufa ni kutoka chama gani.Kifo hakipaswi kuangaliwa kwa sura ya uchama. Ni lazima tukemee na kupinga Umwagaji wa Damu ya watanzania au mtanzania yeyote yule asiye na hatia.
Mpe ushauri huo mwenyekiti wako ambaye naye alidhihaki kwa kusema kifo cha Ali Kibao ni sawa tu na kifo cha mlevi fulani huko kwenu Mbozi?? Akahitimisha kwa kusema KIFO NI KIFO TU.
 
Matukio kama haya yatuunganishe kama Taifa na siyo kutugawa kwa kuangalia aliyekufa ni kutoka chama gani.Kifo hakipaswi kuangaliwa kwa sura ya uchama. Ni lazima tukemee na kupinga Umwagaji wa Damu ya watanzania au mtanzania yeyote yule asiye na hatia.
Uwaambie hayo wana CCM wenzako.

Kifo ni kifo bwana mdogo acha drama.
 
Hi
Embu jaribu kuguswa na matukio yenye kugusa hisia za watu kama tukio hili la mauaji ya kikatili.
Hilo tukio ni baya saana mkuu lakini kwa wasifu wako wewe,ungetumia hata akili ya kunya na kukojoa usingekuwa mleta hii mada wala kuhamasisha watu waguswe na hili ni ushauri tuu bro maana najua hata wew uliumbiwa soni na una akili timamu.
 
UVCCM na CCM yote kwa ujumla wake imekuwa ikilaani na kukemea matukio ya aina hiyo.

Majuzi tu hapa Mwenezi wetu na msemaji mkuu wa chama chetu cha CCM Taifa Ndugu CPA Amos Gabriel Makalla amelaani vifo vya watu vilivyotokea wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia amekuwa akilaani sana mauji ya watu na kuagiza kufanyika kwa Uchunguzi
Weka hapa barua ya kulaani hayo mauji au uliiona peke yako
 
Back
Top Bottom