Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
UVINZA, KIGOMA: Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani ametoa ufafanuzi kuhusiana na tukio la vurugu lililotokea Mei 5, 2026 katika Kijiji cha Kalilani, ambapo vijana watatu walijeruhiwa kwa risasi wakati wa zoezi la kutoa elimu na uhamasishaji kwa wananchi wanaotakiwa kupisha maeneo ya hifadhi.
DC Mathamani amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea wakati msafara wa viongozi wa wilaya na mkoa ulipofika kijijini hapo kuendelea na zoezi la tathmini na uhamasishaji wa wananchi kuhama kwa hiari ili kupisha mipango ya matumizi bora ya ardhi.
HOJA YA AWALI ~ Askari wamewajeruhi vijana watatu kwa risasi – Uvinza wakati wa msafara wa DC, Mei 5, 2026, hatua zichukuliwe
Chanzo cha Mgogoro:
DC Mathamani ameeleza kuwa mgogoro huo unahusu vitongoji viwili vya Mahamaza na Badyonyungu ambavyo vipo ndani ya hifadhi ya misitu ya Mahale. Serikali ilitoa agizo la wananchi hao kuondoka ili kupisha hifadhi hiyo, huku ikiahidi kulipa fidia kwa wale watakaokubali kuhama.
Amesema "Zoezi hili limeanza tangu mwaka 2023. Kaya 205 tayari zimekubali kufanyiwa uthamini, zimepokea fedha zao na zimeshaondoka. Hata hivyo, kaya 171 zimegoma kuhama licha ya elimu na uhamasishaji kutolewa mara kwa mara."
Tukio la Mei 5, 2026
Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa siku ya tukio, kundi la wananchi lilijitokeza na kuwavamia askari waliokuwa kwenye msafara huo kwa nia ya kuleta fujo na kujaribu kunyang'anya silaha. Katika purukushani hiyo, ndipo watu watatu walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kupata matibabu.
Ameongeza kuwa majeraha hayo yalitokea wakati askari wakijihami dhidi ya uvamizi wa wananchi hao.
Amesema “Siyo kweli kuwa Askari walianza kuwafyatulia risasi ila ilitokea katika vurugu hizo na wamepelekwa katika eneo la kufanya huduma, baada ya hapo zoezi halikufanyika, wale Wananchi wakawa wanatoa matamko ya vitisho.
Umuhimu wa Zoezi Hilo
Serikali inashirikiana na Shirika la Tuungane (The Nature Conservancy) katika mradi wa matumizi bora ya ardhi ambao unajumuisha:
Licha ya changamoto hizo, DC Mathamani amesema viongozi bado wapo eneo la tukio wakiendelea na mazungumzo. Hadi sasa, viongozi wa dini (misikitini) wameanza kutoa ushirikiano kuwashawishi waumini wao kukubali zoezi hilo kwa amani kwa kuwa asilimia kubwa ya waliopo hapo ni Waisalmu.
"Hadi jana (Mei 7, 2026), tumeweza kuwapata watu wa Kaya 18 kati ya 171 zilizobaki. Tunaendelea kutoa elimu na uhamasishaji ili zoezi hili likamilike kwa manufaa ya nchi, kwani mipango ya serikali haiwezi kurudi nyuma," alihitimisha DC Mathamani.
Pia soma ~ KIGOMA: Tukio la Watu watatu kujeruhiwa kwa risasi Uvinza, Polisi yasema inafanya uchunguzi

- Upimaji wa ardhi kwa ajili ya makazi bora.
- Ujenzi wa shule mpya na miundombinu ya kijamii.
- Ulinzi wa mazingira na vyanzo vya maji kwa faida ya utalii na vizazi vijavyo.