Uvumi kuwa Mzee Kikwete yupo nyuma ya Uongozi wa Rais Samia unaweza kuwa Kikwazo cha Ufanisi na chanzo cha kuhujumiwa kwake

Uvumi kuwa Mzee Kikwete yupo nyuma ya Uongozi wa Rais Samia unaweza kuwa Kikwazo cha Ufanisi na chanzo cha kuhujumiwa kwake

Msoga gang wamerudi on fire, tulimwona yule joka la mdimu wa goli la dk ya 89 kule akimwimbia mama mapambio kwa bashasha zote.......na kwenye kuziba pengo lililotokea hivi karibuni kuna uwezekano mkubwa member mwingine kutoka timu msoga gang akatimba ndani, hii ndo inaitwa 'return of the roman empire' tunaenda kuwa koloni la wachina....
 
Mightier nikisema Jambo jua kuna HATARI fulani ama naiona au nimeisikia na nilichokiandika hapa nimekimaanisha na niliowataja wawe Makini na walio karibu nao ( Wasaidizi ) wawashauri.
We jamaa unanichekeshaga [emoji23] sana kujifanya una connection eti nimesikia kitu mara nimeambiwa kitu na mtu wa ndani[emoji16],eti niliowataja wawe makini[emoji1787][emoji1787][emoji1787] you're FUNNNNNYYYYY kwakweli[emoji847]
 
Hakuna binadamu atapendwa au kuchukiwa na watu wote. Watu wa kanda ya Ziwa nikiwamo mimi hata tusipompenda au kumuongelea vizuri mama, ni sawa tu, Tanzania ina kanda nyingi, labda huko kwingine watamuongelea vyema. Kazi iendelee...
Kauli ya kukata tamaa hii,na hii imesababishwa na kumtegemea sana binadamu mwenzenu kiasi chakumfanya yeye ni mungu wenu,sasa kafariki mnadhani maisha hakuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitihada zenu za jumchafua mzee wa watu (kikwete) zitapotea km moshi angani na mtakuwa wa kwanza kuaibika kama walivyoaibika na kumalizika wengine huku yeye akiachwa anaendelea na maisha yake na tabasamu tele usoni!! Mashefani wakubwa nyie
 
Msoga gang wamerudi on fire, tulimwona yule joka la mdimu wa goli la dk ya 89 kule akimwimbia mama mapambio kwa bashasha zote.......na kwenye kuziba pengo lililotokea hivi karibuni kuna uwezekano mkubwa member mwingine kutoka timu msoga gang akatimba ndani, hii ndo inaitwa 'return of the roman empire' tunaenda kuwa koloni la wachina....
Heri Msoga irudi sababu wanajua kula na wengi,kuliko nyie Sukuma Gang mlikuwa mnakula wachache na hamkutosheka mkawa mnawapokonya wengine kidogo walichonacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hatari fulani nimeanza kuiona, kuna maneno fulani nimeanza kuyasikia na kuna Mipango fulani ya kukomoana na kuhujumiana ndani kwa ndani nimeanza kuisikia pia.

Mimi sina uhakika kuwa kwa sasa Rais Samia ni TV Screen tu ila Rais Mstaafu Kikwete ndiye Remote Control kama watu wasemavyo, ila kama hili lina Ukweli basi kuna Hatari moja Kubwa ndani ya CCM na Serikali naiona inaenda kuja (kutokea)

Na wewe Rais Mstaafu Kikwete kama ni kweli una Ushawishi mkubwa katika Utawala huu wa Rais Samia tafadhali jishtukie upesi, kaa mbali nae na mwachie Mama nae atengeneze Legacy yake kwa huongelewi vyema na Watu wa Kanda ya Ziwa hasa baada ya Tukio Kubwa nchini la tarehe 17 Machi, 2021.

Kuna Taa Nyekundu ninaiona mahala!
Problem ni kwamba uwezo wako hauna ujanja zaidi ya mawazo yako ya kufikirika.
Let me assure you that hakuna RED LIGHT wala BLUE LIGHT itakayotikisa serikali,my friend usicheze na Govt na hicho ulicho andika nikuombe kiwe cha mwisho na wala usirudie tena.
 
Ni tetesi hata kipindi cha mwendazake aliopoingia mlisema Kikwete ndo remote control
 
Kwa zile Kashfa, matusi mazito, kejeli, kuvuja kwa siri nzito za serikali kutokea sehemu ambayo huwezi dhania.

Kisha leo ghafla ukurasa uleule unageuka kuwa rafiki wa serikali mpya baada ya kifo cha Hayati Magufuli inatia mashaka sana nani ni mhusika wa ukurasa ule?

Aendelee kupumzika Shujaa wa Tanzania mpya.
Yule jamaa wa twitter, kuna namna alikuwa anatumika na watu wa system au watu wazito kum sabotage hayati na serikali yake.....siyo bure.
 
Hii akili ya Sukuma Gang kwa kila andiko ni kufilisika kimawazo na ni lugha chafu ya kiubaguzi. Mimi si Msukuma ila naamini usawa na udugu tulioujenga kwa miaka mingi. Jadili hoja acha kuhamisha mjadala kwa lugha zako mfilisi za ukabila .SHAME ON YOU

Lugha Za ukabila nazikemea Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,japo mm ni mchagga wa Kule Ntudu
 
Chief umeshasema uvumi aka tayari uvumi...sasa unataka JK achukue hatua gani wakati tayari ni uvumi....Hii nchi kuna uvumi mwingi sana kwenye mambo mengi sana mfano BWM alivumishiwa jambo juu ya JKN hivyo hivyo JPM alizushiwa jambo juu ya BWM...

Hiyo sumu ipo na imeenezwa makusudi na watu fulani lengo ni systema iwaogope isiwaguse kwa kigezo cha wao kuaminika na jamii yenye wapiga kura wengi...Kifo cha Mzee wetu tumuachie Mungu mwingi wa rehema yeye ndiye mjuaji lakini Mzee wetu alizungukwa na wajinga wajinga wengi walioota mapembe na kuamini sasa nchi ni yao milele na hakuna wakuwagusa.
Kiukweli kundi hili lingeachwa huko mbele nchi ingeweza kuingia kwenye hatari sana pamoja na yote...Kama Taifa tunapaswa kujifunza kitu kutoka kwa mwalimu JKN juu ya haya makabila makubwa na uongozi wa nchi...
 
Sukuma gang watulie, zama zao zimekwisha rasmi.

Hakuna cha kanda ya ziwa wala kanda bongoman.

Hebu tuwahi Zanzibar tukapokee ndege zetu mpya.

Ndio mjuwe hizi ni zama nyingine, si zama zile za kila siku jitu moja tu kwenye matukio yote na kujiona ndio ana akili kuliko watu wote.
Hakuna cha kanda ya ziwa wala kanda bongoman.[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Breaking News!

Genta a.k.a JASUSI MBOBEZI amuonya JK
 
Hii akili ya Sukuma Gang kwa kila andiko ni kufilisika kimawazo na ni lugha chafu ya kiubaguzi. Mimi si Msukuma ila naamini usawa na udugu tulioujenga kwa miaka mingi. Jadili hoja acha kuhamisha mjadala kwa lugha zako mfilisi za ukabila .SHAME ON YOU
Kuna kigenge Fulani huenda John (rip) alikidhuru sana hivyo namba ya kumsema kinahusisha wasukuma wote ingawa hata Mimi sipendi mijizi.
 
Ukweli uliopo ni JK kupigwa vita sana na kale kakikundi kakiamini uwepo wa JK ndio sumu kwao kumuoverun mama na kumcontrol ili waendeleze yale maupumbavu yao pamoja kuhakikisha nchi iko himayani kwao milele..

Baada ya kifo cha Mzee inaonekana yale yaliyosemwa na jamaa wa kule twitani yalikuwa na ukweli...na hapo naamini ndio chuki kwa JK ilipoanzia baada ya kuweka msimamo wa kuilinda katiba na kuhakikisha mama anakalia kiti....

Uvumi unaoendelea na kuenea kwa kasi lengo kuu ni kumtisha mama na walionyuma yake juu ya mustakabali wake na nchi huko kanda ya ziwa ili mama aogope arudi upande wao na wao wamuongoze wawezavyo....jambo walitendalo linaweza kuleta hatari kwa Tanzania yote na hata wao hawawezi kuwa salama...Ni vyema vyomba vya usalama vikaanza kudeal na wahusika kimyakimya kuliko hatari iliyombele..
Tusipokuwa makini game hii inaweza kuingiliwa na mafisi waliojirani kama PK na M7 kuzidi kupandikiza chuki maeneo fulani na kutoa support kwa wapumbavu hawa na matokeo yake hali kuwa mbaya maeneo hayo..
 
Back
Top Bottom