Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Wanaenda kuongeza vichwa. Hadi magari ya JWTZ nao wanabeba vichwa
JWTZ wanakuwa wajinga kiasi hiki kutumiwa na CCM ??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaenda kuongeza vichwa. Hadi magari ya JWTZ nao wanabeba vichwa
Ngoja tungoje sanduku la kura litatupa jibuWengi wameletwa na mabasi ya Abood kutoka Morogoro, JWTZ wamevalishwa tshirt za CCM n.k
Zanzibar walikimbia baada ya burudaniMageti yamefungwa hakuna kutoka nje
Kwa tume ipi?Ngoja tungoje sanduku la kura litatupa jibu
Well notedNilikua natania tu mkuu...
Ngoja nimwulize bwana mdogo kama kweli wamevalishwa miguo ya CCM! Ni hatari sana kwa mstakabari wa nchi!JWTZ wamevalishwa tshirt za CCM n.k
Dar yenye wakazi milioni 6 uwanja una uwezo wa kuchukua watu elfu 60 walio kaa CCM wameshindwa kuujaza!!!
It is a realityshame on you...Yani kea miaka hii unawaza kuhusu udini khaaaa!!!!!
Hawawezi kwenda, hawajaongezwa mishahara kwa miaka mitano.Mapumziko ya anko Magu yalikuwa ya kimkakati, hakupenda wanafunzi wa darasa la saba na walimu wao kuvurugika ktk kutimiza ratiba ya mitihani yao ya taifa kumaliza darasa la saba!
Leo wote hao wanajaza uwanja, kazi kweli kweli!
Na wewe ni liongo piaZanzibar walikimbia baada ya burudani
Baada ya kupumzika kwa siku kadhaa, mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea na kampeni leo katika mkoa wa Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Up dates;
HOTUBA YA DKT. MAGUFULI
....gonjwa hili la Corona na kilio cha Wanakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta katika kuliombea taifa na kumuomba Mungu kuondoa Ugonjwa huu, napo Kenya utaondoka. Kwasababu Mungu ukimuomba hakuna kitakachoshindikana, na Mungu ni mwema siku zote. Mungu hoyeeee! Tanzania hoyeee! Kenya hoyee!
Ndugu zangu wana Dar es Salaam, jiji la Dar es Salaam ni muhmu sana hapa nchini. Ni kwasababu jiji hili lina idadi kubwa ya watu kuliko miji mingine yote nchini. Takwimu zinaonesha jiji hili linakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Na itakapofika mwaka 2030 linatarajiwa kuwa na watu wapatao milioni 10.
Hii italifanya jiji hili kuwa miongoni mwa majiji manne yenye hadhi ya “Megacity” barani Afrika. Majiji mengine ni pamoja na Lagos, Luanda pamoja na Kinshasa.
Kwahiyo jiji la Dar es Salaam ni jiji muhimu sana. Mbali na kuongoza kwa idadi, Dar es salaam ni jiji kuu la biashara hapa nchini ambalo linachangia mapato mengi ya serikali, lakini pia linatoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa.
Takwimu zinaonesha kuwa kwa tarkribani miaka mitano iliyopita Dar es Salaam imekuwa ikiongoza kwa uchangiaji mapato ya serikali, hususani mapato ya kodi.
Takriban 90 % ya kodi yanatoka Dar es Salaam. Nataka nitoe takwimu.
Mwaka 2015/16, mapato ya Dar es Salaam yalikuwa Tshs. Trilioni 11.9 ambayo ni asilimia 89.9
Mwaka 2016/17 ilikuwa Trilioni 12.6, asilimia 88.6
Mwaka 2017/18 ilikuwa Tshs. Trilioni 13.6 ambapo ni asilimia 89
Mwaka 2018/19 ilikuwa Tshs. Trilioni 13. 9 ambayo ni asilimia 88.7
Mwaka 2019/20 ilikuwa Tshs. Trilioni 16.01 ambayo ni asilimia 89.7
Aidha, kwa miaka mitano Dar es salaam imeendelea kuongoza katika kuchangia pato la taifa. Mwaka 2015 ilichangia Tshs Trilion 16.2 ambapo pato la Taifa lilikuwa Tshs. 94.3
Mwaka 2016 Dar es Salaam ilichangia Tshs. Trilioni 18.4 wakati pato la taifa lilikuwa trilioni 108.4
Mwaka 2017 Dar es ilichangia Tshs. 20.5, pato la taifa lilikuwa Trilioni 118.7
Mwaka 2018 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 22.5, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 129.04
Mwaka 2019 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 23.9, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 139. 9
Hii inahihirisha umuhimu wa jiji hili kwa maendeleo ya nchi yetu. Hongereni sana wana Dar es Salaam.
Ndugu zangu wana Dar es Salaam, kama hilo halitoshi, jiji hili ni lango kuu lashughuli za uchukuzi na usafirishaji. Siyo tu kwa hapa nchini, lakini pia kwa nchi nyingi zinanotuzunguka.
Kama mnavyofahamu, nchi yetu inapakana na nchi 8 na nchi 6 hazina bandari, na hivyo kutegemea Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao.
Ndugu zangu Wana Dar es Salaam, ni kwa kuzingatia hayo yote nilipokuja hapa Dar es Salaam kuomba kura mwaka 2015. Niliahidi mambo mengi lakini leo nitataja mambo maubwa manne ambayo niliahidi mwaka 2015.
La kwanza, niliahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Pili, niliahidi kuimarisha miundombinu ili kurahisisha usafiri wa hapa Dar es Salaam lakini pia usafiri wa kwenda mikoani pamoja na nje ya nchi.
Tatu, niliahidi kuboresha huduma za jamii ikiwemo Afya, Elimu, Maji pamoja na Umeme.
Na nne, tuliahidi pia kuboresha mazingira ya biashara kwa ajili ya Wana Dar es Salaam na kwa ajili ya Watanzania wote.
Nafarijika kuona kwamba kwenye hii miaka mitano muliyotupa tdhamana ya kuliongoza taifa, tumeweza kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo.
Wakati tunaingia madarakani, hapa Dar es Salaam, vitendo vya ujambazi hususan vya kutumia silaha vilikuwa vimeanza kushamiri. Ilikuwa mtu ukienda benki kuchukuwa hela, unakuwa na hofu kama fedha zako utazifikisha salama maana uhakika ulikuwa mdogo kwasababu ya ujambazi. Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kudhibiti vitendo hivyo. Sio tu hapa, bali maeneo ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti.
Kwa kuimarika hali ya usalama, wananchi wanaendelea na shughuli zao za Maisha bila hofu.
Nawapongeza Wana Dar es Salaam lakini pia navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama.
Mambo mengine ni kuhusu miundombinu…tumefanya mambo mengi sana.
Kwanza, tumejenga barabara za lami kwenye mitaa ya Dar es Salaam. Ukijumlisha hizo barabara zote za lami zilizojengwa na zinazojengwa, ni zaidi ya kilometa 200 ambapo tumetumia zaidi ya bilioni 660.
Ninyi Wana Dar es Salaam ni mashahidi kwamba hivi sasa mitaa mingi ya jiji hili la Dar es Salaam ina lami na nyingine zimewekewa mpaka na taa, ikiwa barabara ya njia nne kutoka Morocco hadi Mwenge inayojengwa kwa gharama ya Tshs. Bilion 74.8; barabara ya Bamaga-Shekilango, na barabara nyingine. Lakini, barabara ya njia nane ya kutoka Kimara-Kibaha inayojengwa kwa Tshs Bilioni 140, nayo inaendelea kwa kutumia fedha zetu.
Kuhusu hii barabara ya Kimara-Kibaha yupo mgombea mmoja wa Urais amesikika akisema eti tunajenga barabara pana sana. Tena anasema yeye ametembea nchi nyingi na hajawahi kuona barabara pana kama hii. Majibu yake ni kwamba si kweli kwamba hii ndiyo barabara pana kuliko zote duniani, kule “Hoston” (Houston), Marekani ipo barabara inaitwa Katty Freeway, ina njia 26.
Lakini, hata kama kwa mfano, ingekuwa barabara yetu ni pana kuliko zote duniani, mimi sioni ubaya wowote. Hakuna ubaya wa Tanzanania kuwa na kitu kikubwa kuliko chochote duniani. Siyo lazima kila kitu kizuri, kikubwa kiwe kipo Ulaya.
Wawe wanawaacha huru Watu kuondoka shoo ikiisha sio kuwazuia Watu kinguvuWatu wanafuata burudani tu kutoka kwa akina Ali Kiba, Diamond, Harmonize,nk Hakuna jipya.
Baada ya Wasanii kuperform sidhani Kama Watu walibaki kwa kiwango kilekileCcm leo kuujaza uwanja wa taifa ilikuwa ni mtihani wa fizikia dar bado ni ya chadema
Ilivyopita Ambulance tu Watu wakapata mpenyoMageti yamefungwa hakuna kutoka nje
Hivi leo Lisu si ndio ana maliza kale ka penalty ka tumeccm siyo, na kesho atakuwa hewani auKumekucha.
Hii sio ya kukosa.
Asiye na mwana aelekee jiwe.
Leo ndio leo msema kesho ni muongo.
Ni zamu ya wana dar es salaam kuonesha mapenzi yao kwa chama chao na mgombea wake.