Uwanja wa Benjamin Mkapa | Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC Vs Plateau United

Uwanja wa Benjamin Mkapa | Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC Vs Plateau United

Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Jumamosi ya leo Disemba 5, 2020 watakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kupapatuana na Plateau United, kutoka nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku Simba SC wakipewa nafasi nzuri ya kushinda kutokana na kupata ushindi ugenini wa bao moja bila majibu kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria kwenye uwanja wa New Jos matokeo ambayo Plateau United wakitaka kuweka rekodi ya kupindua matokeo.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck kuelekea mchezo wa leo amesema " Utakuwa mchezo mgumu, na mchezo ambao tumepishana kwa goli moja, hivyo lazima tuwe makini na natarajia mashabiki watajitokeza kwa wingi kushangilia. Timu yao ni nzuri hivyo tunahitaji kila aina ya nguvu ambayo tunayo ili tuweze kupata matokeo mazuri" amesema Vanderbroeck

Kulipewa Mwana... Kulitaka Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Mabingwa Afrika ni kuanzia saa 11:00 jioni. Azam Sports 1 HD Live na Ghazwat na Jopo zima la JF litakuwa hapa Mubashara kukuletea mtanange huu kinagaubaga.

Usikose Ukasimuliwa..

Kikosi cha Simba SC;


Aishi Manula
Shomari Kapombe
Mohamed Hussein
Erasto Nyoni
Pascal Wawa
Jonas Mkude
Hassan Dilunga
Mzamir Yasin
John Bocco
Claotus Chama
Luis Miquissone

Subs;

Kakolanya
Gadiel
Ame
Ndemla
Kahata
Kagere
Morrison




View attachment 1642028
Mbona hujaweka kikosi cha Plateau United?
 
Back
Top Bottom