Uwanja wa Mkapa ni eneo gani mtu akikaa anaona mechi vizuri kuliko maeneo mengine?

Kuna raha sana kuangalia mpira live pale kwa mkapa. Kama umezoea kuangalia kwa tv af uingie uwanjani unaweza dhani wachezaji hawako serious kumbe wako serious.

Af uwe na earphones uwe unasikiliza matangazo kwenye radio🔥🔥
Ukizoea kwenda uwanjani TV haina kazi ni full shangwe!
 
Hakuna goli la mashariki kwa mkapa,ni kusini na kaskazini
Mi nawahigi ule mapema ule upande jua linapozama,napigwa kwanza na jua ila mechi inapoanza kivuli ndo inaanza naona uwanja wote bila kuumizwa macho na jua,ila kwa mechi za mapema,ila kama za usiku popote fresh tu
 
VIP A ndio kila kitu, B ile ya blue na C ukipata nafasi mkabala na A ni pazuri pia.

Mzunguko hadi uwe mwenyeji na ujue kujiposition, utapata view nzuri.
 
Sisi watu wa nje ya Dar es salaam hatujui majukwaa ya uwanja wa Mkapa yalivyopangiliwa, hivyo kuuliza si ushamba😃

Ni eneo gani ukiwa kwa Mkapa ndiyo unaweza kuona mechi vizuri zaidi kuliko maeneo mengine ya uwanja huo wa Mkapa?
ni kukaza macho vizuri tu gentleman, ukikaa popote tu unaona mechi vizuri sana...

ukikodoa macho kwa bidii hutojuta kwenda Lupaso🐒
 
Hizo VIP hakuna niliyowahi kukata ticket, maana wengine wanasema unaweza kukata na hakuna nafasi unafika pamejaa, ni kweli unaweza kukata VIP na usikae?
VIP A ndio kila kitu, B ile ya blue na C ukipata nafasi mkabala na A ni pazuri pia.

Mzunguko hadi uwe mwenyeji na ujue kujiposition, utapata view nzuri.
 
Hizo VIP hakuna niliyowahi kukata ticket, maana wengine wanasema unaweza kukata na hakuna nafasi unafika pamejaa, ni kweli unaweza kukata VIP na usikae?
Mara nyingi mno!

Yani naweza kusema VIP nimekosa siti mara nyingi zaidi ya nilizopata, hadi nilipobadili utaratibu nikawa nawahi.

Ule msimu Yanga tuliofika fainali CAFCC wote nilikataa VIP, ilikuwa shida sana na inaumiza kulipa hela nyingi ukakosa siti.

Huo uhuni uko sana VIP B na C, A sio sana.
 
Waodoe running tracks na kuongeza viti. Hizo lines sijawah ona manufaa yake. Uwanja mzuri unapaswa kuwa hivi

1736365777005.jpeg
1736365740463.jpeg

1736365832524.jpeg
 
Mara nyingi mno!

Yani naweza kusema VIP nimekosa siti mara nyingi zaidi ya nilizopata, hadi nilipobadili utaratibu nikawa nawahi.

Ule msimu Yanga tuliofika fainali CAFCC wote nilikataa VIP, ilikuwa shida sana na inaumiza kulipa hela nyingi ukakosa siti.

Huo uhuni uko sana VIP B na C, A sio sana.
Dah hapo kweli inauma,unalipa vizuri uangalie kwa raha zako mwisho wa siku hamna siti,heri ingekuwa siti zina namba kama ulaya hata usipokwepo itakaa wazi
 
Ni kweli,ila mbona hata viwanja vya Misri ,Morocco na South Africa hivo mistari ipo, nadhani wameziweka kwa ajili ya riada pia
Riadha lini kitaifa ilifanyikia hapo kwa mkapa? Hivi vilabu simba na yanga wakitengeneza viwanja vyao, waachane na hizo running tracks. Wastage of space, inafanya mashabiki wakae mbali na pitch
 
Ni kweli mashabiki wanakuwa mbali na pitch hata ukikaa kule mbali kwenye mzunguko sometimes unakuwa na uoni hafifu, Azam sasa hivi washaanza kuweka viti na pameanza kupendeza lakini kwa Mkapa kuna mashabiki wanaangalia mechi zaidi ya umbali wa mita 100
 
Dah hapo kweli inauma,unalipa vizuri uangalie kwa raha zako mwisho wa siku hamna siti,heri ingekuwa siti zina namba kama ulaya hata usipokwepo itakaa wazi
Hii siyo sawa na basi inaonesha kuwa wanaoendesha huo uwanja wana mambo ya kizamani.

Unakuwaje VIP halafu ukose kiti cha kukalia. Ina maana hapo VIP hakuna idadi ya viti inayojulikana?
 
Pale kinachoonekana kuna upendeleo kwa kujuana,kuna waheshimiwa hawakati ticket au hata wakikata ni za mzunguko ila wanaenda kukaa kule,maana idadi ya seats zinajulikana na kama watu wamekata zikaisha haiwezekani kuongeza sasa inakwaje watu wanazidi kuliko viti?
 
Kabisa... Wapo maafande wa polisi na wanasiasa. Utashangaa wakati wa mechi mtu kabaa sare ya polisi Kama vile yupo "duty" ...
 
Back
Top Bottom