KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,
Nyasiii.JPG
Hivi kweli tumeshindwa kutunza huu uwanja? Usafi wa vyoo na maeneo mengine imekuwa tatizo sugu lakini aibu kubwa zaidi ni sasa hata pitch imetushinda.

Ni aibu National Stadium nyasi kuisha na kuwa na mapengo ya vumbi. Serikali kwenye hili mnastahili lawama zote kwa kushindwa kusimamia huu uwanja.

Hii nchi kwenye mpira tunachambua mambo mengi ya kijinga na wakati mwingine kuacha vitu fundamental.

Uwanja wa Taifa kuwa na pitch ya namna ile ni aibu ya Taifa. Watu wawajibike kwenye hili! Aibu! Aibu! Aibu!

Shame on us!

Pia soma: Serikali yatoa ufafanuzi madai ya kuwa Uwanja wa Mkapa unatia aibu kwa uchafu
 
Ile mistari kwenye pitch imepauka haiionekani vizuri.

Sijui ni nani mtunzaji wa huo uwanja.

Akakula mapato tu kazi Hana.
Sisi sijui tupewe nini tuweze! Mashirika yametushinda sasa hadi ku manage uwanja? Hadi siku mama Samia asemee hili? Uwanja hadi unakuwa na mapengo? Imagine upo uwanja wa uhuru hautumiki kabisa! Lakini pia kutumika mara nyingi si sababu.

Sasa itabidi tuanze kulisemea kwa sauti tofauti ndio itaeleweka maana nchi yetu mambo hayaendi bila kelele.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Hivi kweli tumeshindwa kutunza huu uwanja? Usafi wa vyoo na maeneo mengine imekuwa tatizo sugu lakini aibu kubwa zaidi ni sasa hata pitch imetushinda...

Boss uwanja ni mmoja, kuna timu kongwe zina miaka zaidi ya 80 hazina viwanja, zote zinatumia uwanja huohuo kama uwanja wa nyumbani, (Overuse) ,

Kumbuka kuna timu ndogo tu zinaanzishwa na tayari zina viwanja vyao na kumbuka kuna ile takataka inaitwa tff huwa inavifungia viwanja vyao wakati wowote (hasa pale hizi timu ndogo mpya zinaposhindwa kujiongeza [emoji383])

Nchi nzima tuna kiwanja kimoja,

Serikali hii ya hovyo bado haijaona umuhimu wa kujenga viwanja vingine hata viwili vyenye capacity ya 20-30k dodoma au moro au Arusha na dsm licha ya kukopa mabilioni ya pesa ulaya.
 
Kama tunakosa akili ya ku manage uwanja tutaweza hayo mandoto tunayoota? Vitu vidogo sana tunafeli. Hivi tumeshindwa kutunza walau, walau, walau eneo la kuchezea?

Aliyeturoga kafa!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Hakuna kitu Tanzania imefanya ikafanikiwa.

Mwendokasi imeshajifia. Inasubiri kuzikwa.
 
Tumeruhusu wezi kushuka nyanja zote za mapato.
Kila Sehemu yenye mapato wanasimamia ni mtandao Wa wezi.
Hawawezi kusimiana.
Nenda kwenye mapato ya setendi, masoko na NHC .
Kila Mahali ni Wizi mtupu.
Watu wanatafuta pesa za Kulewa na wanawake.
Nchi haina dirá inayoweza kufuatwa na watu WOTE na kumweka pembeni MTU anayetupoteza
 
Wampe bakresa kama tumeshindwa ila ni aibu. Sasa tutaweza nini sisi? Alafu ni National Stadium! [emoji35]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app

Kuna ile screen huwa iko off muda wote, halfu kuna mwamba (manager) wa ule uwanja yupo tu, anakula salary.
Sijui hizi kazi huwa wanapeana vipi, inafaa ifike wakati tuhoji,
Yaani tufahamu hii management ya huu uwanja, tuone elimu zao, kisha tuone walipataje hizi nafasi. Kuna haja.
 
Boss uwanja ni mmoja, kuna timu kongwe zina miaka zaidi ya 80 hazina viwanja, zote zinatumia uwanja huohuo kama uwanja wa nyumbani, (Overuse) ,
Kumbuka kuna timu ndogo tu zinaanzishwa na tayari zina viwanja vyao na kumbuka kuna ile takataka inaitwa tff huwa inavifungia viwanja vyao wakati wowote (hasa pale hizi timu ndogo mpya zinaposhindwa kujiongeza [emoji383])
Nchi nzima tuna kiwanja kimoja,
Serikali hii ya hovyo bado haijaona umuhimu wa kujenga viwanja vingine hata viwili vyenye capacity ya 20-30k dodoma au moro au Arusha na dsm licha ya kukopa mabilioni ya pesa ulaya.
Hizi timu kongwe zilitakiwe zipewe hata miaka 5, ziwe zimejenga viwanja vyao.

Wee uwanja kila wiki mechi mbili, unategmea nini hapo. Hata ukitunzaje lazima utazidiwa.
 
Back
Top Bottom