Uwanja wa ndege wa Chato ni chaguo sahihi la Bukoba

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Mara ya mwisho niliposafiri na kutua uwanja wa ndege wa Bukoba nilikaa na mama mmoja wa kihaya aliniambia hali ya hewa uwa mbaya kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka around saa sita mchana,kulikuwa na mpango toka awamu ya tatu kujengwe airport kubwa maeneo ya omkajunguti 40km kutoka Bukoba manispaa,ila sababu zilizo nje ya uwezo zililazimisha uwanja kuendelea kuwa pale katikati ya mji na kuugawa mji katikati,kama kuupanua uwanja wa sasa wa Bukoba ilishauriwa kuvunjwa kwa uwanja wa mpira wa kaitaba na mtaa wote wa kashozi kupisha upanuzi wa Uwanja ila haikuwezekana.

Siku kumi na moja zilizopita ndege ya Precision ilipata ajali kwa sababu ya hali ya hewa mbaya,pia leo Atcl imegeuza na kwenda kutua Mwanza kwa sababu bukoba hali ya hewa ilikua mbaya,swali je kiwanja kipya kitasaidia kufanya hali ya hewa kua nzuri? watu wanasema siasa zimeanza kuingia hapo,wahaya wanataka airport mpya kijanja kwa kutumia kivuli cha ajali, wengine wanasema Uwanja wa J F Kennedy New York safari zinaahirishwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa,ndio iwe huu wa Bukoba jamaa zangu wahaya wanaotaka wajengewe?!

Ni kweli uwanja nahisi ni mfupi wakati ndege ikitua (touch down) utasikia kishindo kikubwa tofauti na viwanja vingine na abiria wamekuwa wakilialamikia tatizo mara kadhaaa,lakini suala la uwanja sio mfupi kivile kulingana na ndege zinazoruhusiwa kutua hapo run way ina urefu wa kilomita 1.5,ambayo ni sawa kabisa,na kawaida katika uwanja wa Bukoba,ndege zinapokuwa zina take off,huwa zinatumia kama 60% tu ya uwanja zinakuwa zimesha paa hivyo hivyo wakati wa kutua kwa hiyo hilo sio tatizo kwa sasa,Issue ya runway inategemea aina ya ndege! zile ATR za Precision Air na hizi Bomberdiear sio issue kabisa! Huwezi kukuta Airbus au Boeing 787 haiwez ruhusiwa kwenda Bukoba kutua ata sikumoja.

Issue ya Bukoba actually ni hali ya hewa kwa kesi hizi za sasa tunazosikia,issue yakuhamisha uwanja mwingine ilikuwa ni kutokuwa na nafasi ya kuongeza kwa hii Airport yasasa,watu walisema pale ulipotaka ukahamishiwe yaani omkajunguti ilishindikana si kwasababu za kisiasa au mtu binafsi ila baada ya kufanyika visibility study ya uwanja mpya iligundulika ili ndege iweze kutua katika uwanja wa omkajunguti inabidi ndege iguse anga la Rwanda au Burundi! hali hii ilionekana kuwa ni hatari sababu ikitokea hizo nchi mbili zimefunga anga lake uwanja wa ndege huo usingekuwa unafanya kazi nao ungefungwa,haafu pia ingetakiwa uwe unalipia katika anga la Rwanda au Burundi kila inapotaka kutua au kupaa.

Sasa je,watu wapande kisbo na Mohamed Trans wakifika Mwanza kwa ndege,wamalizie Kagera?kwanini rubani asitue Chato mpaka aende mwanza? Kwanini ameenda mpaka mwanza wakati kuna chato international airport hapo karibu,kama Bukoba Airport ipo Analogy!! Iakini Chato ni digital na ina Automatic systems ndege inatua yenyewe ata kama kuna Ukungu au umeme umekatika etc! tutumie Chato iliyojengwa juzi ambayo ni ya kisasa na ina automation! kama hata dege za atcl ambazo ni mpya na zina auto pilot haziwezi shuka Bukoba Airport basi chaguo sahihi la Bukoba ni Chato International Airport,na usafiri wa mwendokasi uwepo kuanzia Chato hadi Bukoba ambapo ni kilomita 221.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Si mtaalam wa aviation, nahitaji clarification ya matumizi ya anga la Rwanda na Burundi kama ungetua omukajunguti (note. Uganda ipo jirani zaidi na omukajunguti kuliko Rwanda na Burundi lkn ndege hazigusi anga la Uganda, bali Rwanda na Burundi!).
 
Kwa nini hiyo ya Bukoba iendelee na mfumo wa analogy? Kwa nini isifungiwe mfumo wa digitali wenye automatic landing system? Kwa nini runway yake isiwekewe taa ili iweze kuonekana wakati wa mvua na ukungu?

Sawa, Chato international airport ni best alternative landing place siyo tu kwa Bukoba airport bali pia kwa Mwanza international airport inapotokea hali ya hewa kuwa mbaya kwenye viwanja hivyo. Helicopters zinaweza kuandaliwa kuwa air lift wasafiri watakaotua hapo Chato kuwapeleka hadi Bukoba au Mwanza waliolazimika kutua hapo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
 
yaani watu waongo hadi kero....kutoka pale Omukajunguti hadi mpakani kwa TZ na UG haizidi km 30 sasa lakini wameanza kuleta vi sababu vya uongo uongo hapa....mbona mwanzoni walisema shida ni Swamp....leo et shida ni kugusa anga za majirani
 
Nionavyo kabla ya pilot kuruka kwann asiulize hali ya hewa ikoje huko, kwann waende kwa kubahatisha?
 
Mara ya mwisho niliposafiri na kutua uwanja wa ndege wa Bukoba nilikaa na mama mmoja wa kihaya aliniambia hali ya hewa uwa mbaya kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka around saa sita mchana,kulikuwa na mpango toka awamu ya tatu kujengwe airport kubwa maeneo ya omkajunguti 40km kutoka Bukoba manispaa,ila sababu zilizo nje ya uwezo zililazimisha uwanja kuendelea kuwa pale katikati ya mji na kuugawa mji katikati,kama kuupanua uwanja wa sasa wa Bukoba ilishauriwa kuvunjwa kwa uwanja wa mpira wa kaitaba na mtaa wote wa kashozi kupisha upanuzi wa Uwanja ila haikuwezekana.

Siku kumi na moja zilizopita ndege ya Precision ilipata ajali kwa sababu ya hali ya hewa mbaya,pia leo Atcl imegeuza na kwenda kutua Mwanza kwa sababu bukoba hali ya hewa ilikua mbaya,swali je kiwanja kipya kitasaidia kufanya hali ya hewa kua nzuri? watu wanasema siasa zimeanza kuingia hapo,wahaya wanataka airport mpya kijanja kwa kutumia kivuli cha ajali, wengine wanasema Uwanja wa J F Kennedy New York safari zinaahirishwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa,ndio iwe huu wa Bukoba jamaa zangu wahaya wanaotaka wajengewe?!

Ni kweli uwanja nahisi ni mfupi wakati ndege ikitua (touch down) utasikia kishindo kikubwa tofauti na viwanja vingine na abiria wamekuwa wakilialamikia tatizo mara kadhaaa,lakini suala la uwanja sio mfupi kivile kulingana na ndege zinazoruhusiwa kutua hapo run way ina urefu wa kilomita 1.5,ambayo ni sawa kabisa,na kawaida katika uwanja wa Bukoba,ndege zinapokuwa zina take off,huwa zinatumia kama 60% tu ya uwanja zinakuwa zimesha paa hivyo hivyo wakati wa kutua kwa hiyo hilo sio tatizo kwa sasa,Issue ya runway inategemea aina ya ndege! zile ATR za Precision Air na hizi Bomberdiear sio issue kabisa! Huwezi kukuta Airbus au Boeing 787 haiwez ruhusiwa kwenda Bukoba kutua ata sikumoja.

Issue ya Bukoba actually ni hali ya hewa kwa kesi hizi za sasa tunazosikia,issue yakuhamisha uwanja mwingine ilikuwa ni kutokuwa na nafasi ya kuongeza kwa hii Airport yasasa,watu walisema pale ulipotaka ukahamishiwe yaani omkajunguti ilishindikana si kwasababu za kisiasa au mtu binafsi ila baada ya kufanyika visibility study ya uwanja mpya iligundulika ili ndege iweze kutua katika uwanja wa omkajunguti inabidi ndege iguse anga la Rwanda au Burundi! hali hii ilionekana kuwa ni hatari sababu ikitokea hizo nchi mbili zimefunga anga lake uwanja wa ndege huo usingekuwa unafanya kazi nao ungefungwa,haafu pia ingetakiwa uwe unalipia katika anga la Rwanda au Burundi kila inapotaka kutua au kupaa.

Sasa je,watu wapande kisbo na Mohamed Trans wakifika Mwanza kwa ndege,wamalizie Kagera?kwanini rubani asitue Chato mpaka aende mwanza? Kwanini ameenda mpaka mwanza wakati kuna chato international airport hapo karibu,kama Bukoba Airport ipo Analogy!! Iakini Chato ni digital na ina Automatic systems ndege inatua yenyewe ata kama kuna Ukungu au umeme umekatika etc! tutumie Chato iliyojengwa juzi ambayo ni ya kisasa na ina automation! kama hata dege za atcl ambazo ni mpya na zina auto pilot haziwezi shuka Bukoba Airport basi chaguo sahihi la Bukoba ni Chato International Airport,na usafiri wa mwendokasi uwepo kuanzia Chato hadi Bukoba ambapo ni kilomita 221.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Great post, lakini toa hizo credentials zako hapo chini sio mahali pake
 
Wanasiasa wa Kagera hasa wabunge wa miaka ya 2010 na wao wanahusika na hali ya kuwa na uwanja hatarishi, zaidi ya ajali 4 katika kipindi cha miaka 30.

Uwanja ulipanuliwa 2014 ndani ya Manispaa ya Bukoba. Walio wengi walidhani itahamishiwa onukajungiti. Kwenye kampeni ya ubunge, mmoja wa wagombea akasema, nimejitahidi serikalini kuhakikisha uwanja hauami toka Manispaa kwa sababu 2.

Sababu ya kwanza omukajunguti ni jimbo la Nkenge, sifa angelipata mbunge wa Nkenge wilaya ya Misenye badala ya mimi wa Manispaa.

Sababu ya pili wasafirishaji wa taxi wangelikosa abiria, kwenda na kutoka omukajunguti hadi bukoba mabasi ya Kati yangetumika sawa na KIA, maneno ya mbunge kwenye kampeni.

Pamoja na yote, uwanja hadi leo hauna taa kwenye njia ya kutua na kuruka, ikija ukungu rubani wa kutua anarudisha ndege mwanza au anabahatisha kudura za Mungu.

Rubani akitaka kutua kwa dharula, Bukoba hakuna mnara wa kuongoza ndege, anatumia control ya mwanza, taarifa za usaidizi za kutua kwa zarula uwanjani Bukoba zitatoka mwanza kueleza waokoaji wa Bukoba wajiandae kwa ndege kutumia simu ya kawaida.,
 
Mkuu vingi umeandika kweli ila kwenye issue ya ndege kutua Omukajunguti lazima iguse anga la Rwanda/Burundi hapo umetupiga.!

Fanya Geographical research zaidi ya mkoa wa Kagera
 
Imagine!!! aina hii ya wasomi ndo tulionayo nchi hii!!! Sidhani kama hata geografua ya mkoa wa kagera una uelewa vzr.

Hii sababu ya ndege kajunguti kupitia rwanda na burundi umeitoa wap mkuu....yaan kajunguti lilipo kufika rwanda ni zaidi ya km 120..inabidi upite wilaya tatu za mkoa wa kagera yaan sehemu ya misenyi, kyerwa na karagwe ndo ufike rwanda.

Kwenda burundi inabidi upite wilaya tatu pia ni karibu km 250.

Hiyo feacibility study na matokeo yake tunaomba report yake mkuu...au ndo yale yale ya mto mara kuchafuliwa na vinyesi vya ng'ombe[emoji28]..

Hiyo hoja kutumia chato haifai kabisa kuongelewa...yaan mtu unakuja Dar wakushushe kilosa..halafu upande bus?
Yaan Bukoba yote serikali imekosa eneo la kujenga uwanja wa ndege kweli?

Nilishawahi kuandika hapa...no one cares about Kagera...hakunaga mradi wa serikali ulioshawahi kutekelezwa kagera...hata hapo Bukoba mjini eneo la kujenga stendi ya mabasi lipogo toka 2008..lakin hadi leo wanazozana wao CCM...hakujawahi kupatikana hela za ujenzi wa stendi mpya...na ushuru unakusanywa hapo kila basi 10k stendi ya sasa ambayo ni matope mda wote

MUNGU huyu ana lengo lake na Bukoba ndo maana analeta majanga kama haya ili serikali iukumbuke japo kidogo mkoa huu...ili at least serikali iuongelee mkoa huu na trust me huo uwanja utajengwa watake au wasitake vinginevyo wafute safari zote za ndege za mji wa Bukoba ambayo nayo ni hasara kwao ambayo Bukoba airport ni moja viwanja vyenye domestic passengers wengi nchini.

Watajenga tu kama ambavyo tetemeko lilivyosababisha serikali ijenge upya na kukarabati hospital na shule zote za mkoa wa Kagera
 
yaani watu waongo hadi kero....kutoka pale Omukajunguti hadi mpakani kwa TZ na UG haizidi km 30 sasa lakini wameanza kuleta vi sababu vya uongo uongo hapa....mbona mwanzoni walisema shida ni Swamp....leo et shida ni kugusa anga za majirani
Na kutoka omkajunguti hadi rwanda ni zaidi ya 150km maana lazima utapita karagwe, kyerwa nk

Burundi ndo mbali kabisa...kwanza burundi imepakana na kigoma zaidu kuliko kagera
 
Nionavyo kabla ya pilot kuruka kwann asiulize hali ya hewa ikoje huko, kwann waende kwa kubahatisha?
😄😄😄😄!! Aviation ni complex sector... Tafuta documentary za aircrash investigation utapata mawanda mapana Sana kuhusu aviation.. Kwa kuanzia unaweza kuangalia Natgeo kila siku saa Moja jioni au saa saatano asubuhi jumatatu mpaka ijumaa!! Au jumapili mchana!! Ukishindwa kabisa Angalia YouTube wameziweka nyingi tu.. Anza na documentary za bad weather accidents.
 
Kujenga uwanja mkubwa wa kimataifa Omukajunguti Bukoba itakuwa ni kutozingatia vipaumbele vya fedha za serikali,tayari kuna Chato international airport,mipango inaendelea ya kuifanya Mwanza airport kuwa international sasa kutakuwa na viwanja 3 vyenye hadhi ya kimataifa eneo moja.

Na hata huo wa Mwanza waliomba ukajengwe Mabuki nje kidogo ya jiji baada ya ndege ya kubeba minofu ya samaki kupata ajali na kudumbukia ziwani.

Loo huu wa kuongeza maviwanja ya ndege utakuwa upendeleo wa kipekee kanda ya ziwa.Mimi nadhani uwanja wa ndege wa Bukoba uboreshwe tu kwa kuweka taa na automation systems za kusaidia kurudi na na kutua salama pia control tower, na kuboresha miundo mbinu ya uokoaji.

Tatizo hapa ni hali ya hewa nayo siyo kila siku ajali moja tu,watu wanataka watumie kigezo hicho kupata uwanja mwingine, tungoje taarifa ya uchunguzi wa ajali tujue sababu pengine ni matairi, kuishiwa mafuta au makosa ya kibinadamu yalisababisha ajali, tusikimbilie uwanja. Mbona ATCL jana amefaulu kurudi Mwanza.

Tuache siasa, na marubani na idara za viwanja na hali ya hewa wawe makini kwa hili wafanye kazi kama wanataaluma wasiingiliwe na siasa za maendeleo kimaeneo. Iwapo kuna shida ya uwanja marubani wana haki ya kutorusha ndege kwenda eneo hilo hadi kiboreshwe.
 
Back
Top Bottom