Uwanja wa ndege wa Chato ni chaguo sahihi la Bukoba

Mbona jengo la abiria la Mwanza ni bovu, bora hata jengo dogo la Bukoba na Arusha,lakini akina ngosha wanasema "nduhu tabu" ninaamini uwanja mpya wa Bukoba utakuwa Bomba kwa ndege kutua mpaka airbus. Hata jengo jepya linalojengwa airport Mwanza ni bure tu kwa kiwango cha kimataifa. Mwanza wabaki walivyo. Bora hata bukoba ujengwe uwanja saizi ya Dodoma Msalato kuwakilisha kanda ya ziwa.
 
Runway iongezwe upande upi kuelekea wapi na itakuwa na uwezo wa kuaccomodate ndege za ukubwa gani na duration gani mkuu, twende kiuhalisia kidogo ili tuisaidie serikali na miradi hewa
In my view, Mita 200-300 haziwezi kukosekana upande ambao sio wa uelekeo wa ziwa.
Hata ikibidi kuhamisha watu kidogo urefu uongezwe.
Ndege zitakazo kuwa accomodated ni dash-8, atr, pc12, cessna na nyingine ambazo zitaweza kuruka na kutua within 1700-1800m.
Na tukizingatia umaskini wa nchi yetu, kila mkoa hauwezi kuwa na uwanja wa mita 3000 ili kuaccomodate ndege kubwa zaidi.
Kibubwa ni at least kila mkoa uwe na kiwanja cha tarmac chenye angalau mita zisizozidi 2000 ili kuharakisha shughuli za maendeleo.
 
Kwa mujibu wa kumbukumbu za kitaasisi mradi wa uwanja wa Bukoba ulikuwa ujengwe eneo

la kyetema karibu na bandari ya kemondo kweny miaka ya 1960
m
Hilo la kujenga airport Kyetema badala ya Omukajunguti na Uhaya wangu na kuzaliwa na kukulia Bukoba ndio nalisikia kwako leo.
 
Wahaya wana majivuno sana
Wahaya wana majiivuno sana lakini isivyo bahati wakifanikiwa nje ya mkoa wao huwa hawana tabia ya kurejesha maendeleo kwao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma huko mikoa ya kusini. Wanakimbilia kwenda kujenga na kuwekeza Mwanza, Dar Es Salaam na Arusha.

Biashara wanasafirisha sana ndani na nje ya nchi lakini hakuna maendeleo ya maana hapo Bukoba.

Watumie uwanja wa Chato kisha barabara kutoka Chato hadi Bukoba ipanuliwe kuwa njia tatu wakifanya hivi baada ya miaka kadhaa maendeleo yatashamiri sana kuanzia Chato, Biharamulo mpaka Bukoba hivyo kuvunja mpango wa Chato kujitanua kuwa mkoa maana haina tija yoyote kuweka mikoa mingi eneo moja bila sababu zozote za msingi.
 
Kwa taarifa tu...
Mimi sio mwenyeji wa kanda hiyo ila kijiografia
Kutoka Mwanza kwenda Bukoba ni karibu zaidi ya kutoka Bukoba kwenda Chato
Sasa utawezaje kuchukulia uwanja mbadala ulio mbali zaidi wakati upo mwingine (mwanza)ambao ni mzuri zaidi na upo Karibu?
Jambo lingine ni kuwa; unapohamisha uwanja unafikiria, Umbali na Facility (sehemu za kulala na huduma nyingine za kijamii) na pia urahisi wa kupata usafiri mwingine wa kuunganisha...
Kwa hapo tu, CHATOI imeshakosa sifa!
 
Huna akili, ni mpuuzi mmoja unayejifanya kujua mambo wakati kilaza tu. Na huo uwanja hujawahi fika unaropoka unavyojisikia.

Umeandika uongo mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…