Uwanja wa Sokoine | Vodacom Premier League (VPL) Tanzania Prisons Vs Simba SC

Uwanja wa Sokoine | Vodacom Premier League (VPL) Tanzania Prisons Vs Simba SC

Kimenyaaa anapiga shutiiiii, lakini linashindwa kulenga lango la Simba, ilikuwa hatariiiii lango la Simba
hahahaha lile shuti la uwezo mkubwa mno mbele ya beki legevu
 
42' Miraji anachanja mbuga lakini anavutwa jezi, ni free kick kuelekea Prisons

Inapigwaaa na Ajibuuuu... Wanaokoa Prisons
 
45+2' Kuelekea kuwa mapumziko VPL uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya

Anakwenda, Ajibu kwake Kageree anajiandaa Offside

Wanapiga Prisons katikati wanamiliki Simba wanagonga

Naaaam ni mapumziko VPL uwanja wa Sokoine huku kila timu zikitoka bila kufungana kipindi hiki cha kwanza

HT, VPL; Tanzania Prisons 0-0 Simba SC
 
Viongozi wangu wa Mbumbumbu wahakikishe Prison wanapata Muamala wao mapema vinginevyo hatushindi
 
Kipindi cha pili kimeanza huku Simba SC wakifanya mabadiliko

Ametoka Ajibu, ameingia Cloutis Chama
 
  • Thanks
Reactions: Lee
46' Kagere pembeniii ya uwanja anapiga kwake Mirajiii anapiga oooooh Kisubi anacheza maridadi kabisa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

Ilikuwa hatariiiii na nafasi kwa Simba SC kuandika bao
 
Fraga anafanyiwa madhambi kwa kukwatuliwa, lakini refa mpira uendelee

Simba SC wameanza kwa kasi kipindi hiki cha pili
 
60' Kimenya anatoka, na ameingia Ismail Aziz upande wa Prisons huku mchezaji wao akionyeshwa kadi ya njano

Na Erasto Nyoni akionyeshwa kadi ya njano upande wa Simba SC
 
67' Luis Miquissone ameingia na ametoka Hassan Dilunga upande wa Simba SC
 
70' Jaribio lango la Simba SC, Aishi Manula anatokea nakucheza na kupangua mpira ule

Kona, inapigwaaa wanaokoa Simba
 
Kudundadunda kwa maharage ndo kuiva kwake! Ni suala la muda tu mnyama anaukwaa ubingwa💪
 
Kwa mara ya pili Tanzania Prisons wanakosa bao la wazi kabisa, baada ya mpira uliopigwa kutoka sentimita chache juu ya lango
 
77' Miquissone ameingia eneo la hatariiiii, anakwenda anawekwa chini mwamuzi alikataa kwa madai si penati

Tanzania Prisons 0-0 Simba SC
 
Huku CCM Kirumba Mbao anaongoza bao moja dhidi ya Polisi Tanzania dakika ya 77
 
Back
Top Bottom