Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Mbumbumbu mbumbumbu[emoji445][emoji444][emoji445][emoji441][emoji444]
Hello Tanzania na kando ya Tanzania

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya March 8, 2020 kwa kuwakutanisha watani wa Jani katika jiji la Dar es salaam, ambapo Yanga African SC, Wananchi wa Jangwani wanawakaribisha Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, Mabingwa wa Nchi, kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na mkali kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na kuwa mchezo muhimu kwa kila timu huku Yanga SC yenye alama 47 kwa michezo 24 wakihitaji alama tatu muhimu katika mchezo wa leo dhidi ya Simba SC vinara wa Ligi wenye alama 68 wakiwa na michezo 26, ambao ushindi kwao ni kutaka kujiimarisha zaidi kileleni na hatimaye ubingwa.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC Luc Eymael, amesema wamejipanga kuwakabili wapinzani wao Simba SC huku akiongeza kuwa ana uzoefu na derby kama hizi.

"Nina uzoefu wa kutosha wa mechi kama hizi (Derby) tangu nafundisha Sudan, DRC Congo na Kenya hivyo mchezo huu ili upate matokeo ni mazuri ni kuandaa mbinu na si kuangalia rekodi au matokeo ya nyuma", amesema Eymael

Kwa upande wake Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck, amesema amekiandaa kikosi chake kuchukua alama tatu ili mwisho wa msimu kushinda ubingwa.

"Tunacheza mchezo huu kama si mchezo wa Ligi kwa sababu kila mmoja anajua tumewaacha kwa alama kadhaa, tutaucheza kama mchezo wa kweli wa wapinzani hivyo tumejiandaa kuchukua alama tatu na tusonge mbele ili mwisho wa msimu tushinde ubingwa", amesema Vanderbroeck

Kwenye mzunguko wa kwanza wa VPL, timu hizi zilitoka sare ya mabao 2-2 Je awamu hii ya lala salama itakuwaje? Safari ya dakika 90 kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.
Karibuni sana Jopo la WanaJF, Kuongoza Jahazi Sambamba Nami Nahodha Ghazwat, Tunakuambia Usibonyeze Kitufe, USIKOSE UKAHADITHIWA.

============

Takwimu Yanga na Simba VPL, 2019/2020.

Simba SC |
Nafasi 1
Alama 68
Ushindi 22
Sare 2
Vipigo 2
Magoli ya kufunga 55
Magoli ya kufungwa 14
Clean Sheets 15

Yanga SC |
Nafasi 4
Alama 47
Ushindi 13
Sare 8
Vipogo 3
Magoli ya kufunga 29
Magoli ya kufungwa 18
Clean Sheets 12

====================

UPDATE;

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad, atakwepo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo wa VPL, Derby ya Yanga African na Simba SC

Rais huyo wa CAF, ambaye amealikwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF), kwa ziara ya siku tatu, na atakutana na viongozi wa Serikali na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuzumgumzia maendeleo ya soka na ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye huo wa watani wa Jadi ambao utapigwa leo Jumapili ya March 8, 2020.

View attachment 1380521View attachment 1380522View attachment 1380523[/B]
Uchebe amewapa pole alafu kapost kimbwa koko
Pat.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile Liverpool yenyeweyenyewe, ile iliyoupiga mwingi kwa miezi 14 mfurumfuru ndo hii Yanga ya leo.

Umepigwa mpira safi leo mpaka nkajua labda wanacheza na Mafyetelo FC ya huku kijijin kwetu maana nao wanavaaga jezi nyekundu.

Kumbe alikuwa mnyama bwana! Hahahaaah! Simba kibogoyo, Simba mla nyasi.
Aiseee, aibu sana!

Afu yale mabishano ya nani mkali kati ya fundi mtembea juu ya mpira MORRISON na kale ka andunje ka ntwara sijui ka MIKISON (spellings si jukumu langu) uishe. Hatuwezi kuwa tunamfananisha Nyangumi na Vidagaa.
 
Japo nimeumia ila nipende tu Kuchukua nafasi hii bila Kinyongo au Unafiki Kuwapongeza walioniadhibu leo.

Uzuri wa Walioshinda leo ni...

Waliingia Uwanjani wakiwa wameamua kabisa kujitoa hadi tone la mwisho ili washinde
Walitusoma Udhaifu wetu na wakafanikiwa Kuutumia na Kutuadhibu
Walikuwa hawana Dharau na Mchezo husika
Walicheza Kitimu na Kimaelekezo zaidi
Walitumia nguvu palipostahili na akili pale ilipohitajika
Kocha Wao ni mzuri katika Kuwasoma Wapinzani na ana Wasaidizi wenye Uchungu na Timu yao
Mikakati yao ya nje ya Uwanja (hasa Kiufundi) ilikuwa ni Kabambe na ilifanikiwa kwa 95%


Mapungufu ya Waliofungwa ( nami nikiwemo humo ) ndani yake ni....

Kocha hakupanga Kikosi Maalum cha Watu Maalum kucheza na Wapinzani wetu waliojiandaa
Viungo Mkude na Chama waliwekewa Mkakati Maalum na Timu yetu ikakosa kabisa Plan B
Timu imeshaathirika kwa Kuamini kuwa Wapinzani wetu ni Wabovu hivyo mara nyingi tunawadharau
Kisaikolojia Timu haikuandaliwa vyema na hilo lilionekana hata wakati wanawasili Uwanjani
Kocha ana tatizo la Kuchelewa kufanya Mabadiliko ila hana Wasaidizi wenye Jicho la Tatu Kimchezo
Uwekezaji wa Timu umewaathiri Wachezaji na muda mwingi wanajiona Wao ni Barcelona ya Ilala
Waliopewa Majukumu ya Mikakati ya nje ya Uwanja walifeli na Timu ipunguze Kuamini Ushirikina


ANGALIZO

Kiujumla Timu haikucheza vibaya sana na tusisahau pia kuwa katika Mpira suala la Bahati lipo kulingana na Upepo wa Siku husika. Ni Mpumbavu tu pekee ndiyo atakasirika na kuchukia kwa Matokeo haya ya leo lakini kwa Mwanamichezo aliyekomaa kabisa atayakubali Matokeo, atawapongeza walioshinda, atawatia Moyo Wachezaji na atajikita zaidi katika Kufanya vyema Michezo ijayo ili Timu iwe Mabingwa tena.

Kuna Wapumbavu kadhaa niliwasikia na kuna Mmoja wao ilibakia kidogo tu leo nizichape nae hasa pale alipoanza kusema kuwa Goli tullofungwa ni Makosa ya Kipa Wetu Manula. Tena Mimi Mzukulu nadhani kama kuna Mtu ambaye leo ameikoa Timu yetu na Aibu ya Kufugwa Goli zaidi hata ya 5 alikuwa ni Kipa Manula. Goli alilofungwa hata Kipa awe anatokea Sebuleni Kwake Mwenyezi Mungu Mbinguni angefungwa tu.

Halafu mnaomlaumu Kipa Manula hivi Logically tu lawama zenu zinatakiwa ziende Kwake au mnatakiwa mzielekeze kwa Mchezaji ambaye leo ndiyo amecheza vibaya na kwa kiasi Kikubwa Kuigharimu Timu Jonas Mkude? Halafu mnapomlaumu Manula na Goli alilofungwa hivi kuna Mtu ambaye anajua Mpira kabisa atahoji Uwezo mkubwa na Kiwango Kikubwa alichonacho Mchezaji aliyetulaza mapema leo Bernard Morrison?

Wala Timu yangu haina haja ya Kupaniki kwa Kufungwa (japo inauma na hata Mimi Mzukulu naumia mno tu) ila tushikamane, tusigombane, tusitafute Mchawi na tuendelee na Umoja Wetu ili tucheze Mechi zetu zote zilizobaki vyema, tushinde na tuwe Mabingwa tena na tuweze Kushiriki Michuano ya Kimataifa tena Mwakani.

UJUMBE WANGU KWA BENCHI LA UFUNDI

Haraka sana naomba Beki Kennedy Juma Wilson aaminiwe sasa rasmi na pia Beki ambaye namkubali kwa 100% Yusuph Mlipili apewe Nafasi na ikiwezekana hawa Wachezaji Wawili ndiyo sasa wawe mbadala wa akina Erasto Nyoni na Pascal Wawa ambao siyo Siri tena sasa wameshakuwa Saa 12 Jioni (Wamechoka na Kuzeeka Kimchezo) na hili wala halina Ubishi.

KUTABIRI SIYO DHAMBI HIVYO NAMI NATABIRI

Najua tumeumia, kusikitika na wengine sasa bado tupo Mafichoni tukisubiri wale waliotufunga waweze kutoka katika Mabaa na Kuingia Majumbani mwao na wale wanaotusubiri kwa hamu Kutuzomea Wachoke Kutusubiri waingie Kulala ili nasi tuingie Makwetu kimya kimya (Nyatu Nyatu) tujipumzishe na Maumivu ya Morrison.

Ila natabiri kuwa kuna uwezekano wa kuwa na Derby nyingine ya Sisi na Wao katika Michuano ya Kombe la ASFC ambapo nina uhakika kuwa nasi tutalipiza Kisasi na tena najua Wao ndiyo wataumia zaidi kuliko Sisi leo kwakuwa si tu kwamba tutakuwa tumewafunga katika ama Nusu Fainali au Fainali hiyo ya ASFC bali pia tutakuwa tumewanyima Nafasi ya Kushiriki Michuano ya Kimataifa ( ya Kombe la Shirikisho ) Kitu ambacho nina uhakika Kitawauma mno kuliko hata Sisi tulivyoumia leo.

USHAURI WA BURE KWA KAMATI YA USAJILI

Acheni Kusajili Wachezaji kwa Mihemko au kwa kutaka Kuwakomoa Wapinzani wetu waliotukomesha leo na Morrison Wao. Hivi kuna Mbrazili anayejua Mpira kweli atoke Kwao kuja Kucheza Mpira hapa ( Madafu Nation ) Tanzania?

Kulikuwa na haja gani ya Kumrudisha Kikosini Winga Shiza Kichuya ambaye alikaa Nusu Msimu pasipo Kucheza Soka la Ushindani na tukaacha Kumrudisha Mchezaji wetu na Mshambuliaji Marcel Kaheza ambaye hivi sasa yuko katika Kiwango chake bora cha Kiuchezaji kuliko hata huyu Kichuya wenu?

Kama tayari tulikuwa tunae Kiungo bora kabisa (japo nashangaa kwanini hapangwi wakati ana uwezo mkubwa tu) Said Hamis Ndemla kulikuwa na haja (mantiki) gani ya Kumsajili Mchezaji Ibrahim Ajib ambaye Mimi sioni aibu (haya) kusema kwamba hakuwa na hata sasa hana Kiwago cha kuichezea timu yetu ila nasikia alisajiliwa kwa Shinikizo la Mtoto wake Mwekezaji. Huu kama siyo Upumbavu Uliokubuhu ni nini?

HITIMISHO

Jamani nina mengi ya Kusema kama siyo Kutapika usiku huu ila naomba nikomee hapa kwani nimeshapigiwa Simu na kuhakikishiwa kuwa Watu (Wapinzani) waliokuwa wakinisubiria njiani na katika Baa za Mtaani ili wanizomee na wanikoge hadi nikome wameshaondoka hivyo nami nataka sasa kuwahi zangu nikapumzike japo sina uhakika kama lile Goli zuri la Morrison sitoliota Ndotoni. Bora ufungwe Goli 5 kuliko Goli 1 kwani linauma sana.

Hongereni mno mliotufunga kwani mlistahili na mlicheza vyema sana hasa mkichagizwa na Kipa wenu Mahiri Metacha Mnata.
 
Yule shabiki aliyesema simba ikifungwa na Yanga atatembea uchi lakini ataikana dini yake hakuishia hapo lakini pia hata mke wake atamtoa. Hii imekaaje okay ngoja tuone manake Simba kesha amizwa.

FB_IMG_1583576804601.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWA.MZIKI HUU WA YANGA
NI WAZI YONDAN APATE PUMZIKO LA.MILELE.MECHI ZA.SIMBA NA YANGA

MLIOONA.MTAEELEWA SIMBA WENGI WAMELIA SABABU YA WAZEE NA WALICHOFANYA YANGA N KUWAKIMBIZA NA KUWEKA.MPIRA CHINI MWAMZOMMWISHOI

ZZILE.CHENGA AZIKUCHAGUA KAGERE WALA MDOGOWAKE HAKIKA NISEME AHSANTE YONDAN UMETUSAIDIA SANA ILA SPEED HII NGUMU KWAKOO KWA.MECHI KUBWAA

Sty
BLSD YONDANI
 
Back
Top Bottom