Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Ikiwa ni siku ya pili kwa wakazi wa Dar kumuaga Hayati Magufuli. Uwanja wa uhuru ulifurika tangu saa tatu na nusu hali iliyofanya wengine waombwe kusubiri nje

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe aliwaomba wawe wavumilivu kwa kuwa wote watapata fursa ya kuaga kabla mwili haujasafirishwa kwenda Dodoma

Waombolezaji wameonekana wakiwa na uchungu mkubwa, wakilia wengine wakizimia kwa vilio baada ya kuuona mwili wa Rais Magufuli kwenye Jeneza

Mwili wa Hayati Magufuli utasafirishwa leo, Machi 21 kwenda Dodoma ambapo Machi 22 wanaDodoma watapata wasaa wa kuaga

1616313956896.png
 
Mungu anawachukua watu wema haraka sana ili waende kupumzika. Wabaya anawaacha kwanza wale bata afu wajifunze maisha.

Lakini kuna wabaya wengine toka wana zaliwa mpaka kufa wanakula bata. Hata kifo chao kinawakuta kwenye bata.

Lakini ni mipango ya mungu. Hatuwezi jua mungu anakusudia nn kuwafanya wabaya wale bata na wazuri kuwahi kuchukuliwa. So tumuachie mungu
Niko Airport hapa namsubiri.
Ila JPM alikuea kipenzi cha watu.

Katuacha mapema mno.
Ila apangalo Mungu......
 
Mungu anawachukua watu wema haraka sana ili waende kupumzika. Wabaya anawaacha kwanza wale bata afu wajifunze maisha. Lakini kuna wabaya wengine toka wana zaliwa mpaka kufa wanakula bata...
Kabisa.
Hapo ndipo wale wenye roho nyepesi huanza kukufuru.
Ila yote tuache yatimie.

Raha ya milele umpe ee bwana...na mwanga wa milele umuangazie,
Apumzike kwa amani.
Amina.
 
Back
Top Bottom