Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Ikiwa ni siku ya pili kwa wakazi wa Dar kumuaga Hayati Magufuli. Uwanja wa uhuru ulifurika tangu saa tatu na nusu hali iliyofanya wengine waombwe kusubiri nje

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe aliwaomba wawe wavumilivu kwa kuwa wote watapata fursa ya kuaga kabla mwili haujasafirishwa kwenda Dodoma

Waombolezaji wameonekana wakiwa na uchungu mkubwa, wakilia wengine wakizimia kwa vilio baada ya kuuona mwili wa Rais Magufuli kwenye Jeneza

Mwili wa Hayati Magufuli utasafirishwa leo, Machi 21 kwenda Dodoma ambapo Machi 22 wanaDodoma watapata wasaa wa kuaga

View attachment 1730756mwamba ameumalza mwendo,RIP magufuli!
 
Back
Top Bottom