Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Uwanja wa Uhuru washindwa kuwamudu waliojitokeza kuaga mwili wa Hayati Magufuli

Tatizo hujiongezi wanaposema kafa mapema wanamaana yao ikiwemo alostahili kumaliza muhula wake na kumalizia alivyovianzisha kwani kumekuwa na desturi kiongozi anapofariki basi alivyoanzisha navyo huwekwa pembeni kwa hila mf. Sokoine
Kipi hakikuendekezwa kwa Sokoine? kufirisi watu ? kwa kuwaita waujumu uchumi
 
Hali halisi.. wengi wa wananchi wanyonge walimpenda kwa kuwa aliwagusa kwa njia moja ama nyingine. Hakupendwa na majizi na wabadhirifu wa mali za umma
 
Kwani wasipompenda au wakampenda ndio inasaidia kuingia mbinguni? naona umeumia sana

Ofcoz kifo chake kimeniuma sana, bila magufuli sidhani kama ningekua mwajiriwa wa serikali tena kwa hii taasisi niliyokwepo bila connection huwezi pata kazi. Intake yetu wote tumeumia sana, Mungu amlaze mahali pepa peponi. [emoji120]
 
Hali halisi.. wengi wa wananchi wanyonge walimpenda kwa kuwa aliwagusa kwa njia moja ama nyingine. Hakupendwa na majizi na wabadhirifu wa mali za umma
Hakika mkuu...

Umesahau na wahanga wa vyeti feki.
 
Lazma uende mkuu?? Si unaenda home tu, mbna sisi wafanyakazi wa serikali hatujaambiwa masuala ya kuaga. Acheni uongo na unafiki hautakusaidia
Mi niko kariakoo mkuu tangia asubh hakuna alienifata kuniuliza kwanini hujaenda msiban... na wafanyabiashara wapo kama kawaida kama kuna walioenda bas wameenda kwa mapenz yao tu...!!! Ila ukifika Gerezan kituo cha mwendokas unakuta wamachinga wapo wanafanya biashara zao kama kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanijua mimi mkuu mpaka uniite mnafiki? Sio Leo ni jana, Meza karibia zote zilikuwa empty, na ameniambia machinga mwenyewe wameambiwa waende msibani.
Umeembiwa? Mi nipo kariakoo mtaa wa Lindi na Msimbaz tangia saa 3 asbh mpaka sasahivi na picha nikuweka waliotaka kuwepo wapo wanaendelea na biashara zao na waliotaka kwenda uhuru kuaga kaenda.
20210321_145320.jpg
20210321_145332.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anawachukua watu wema haraka sana ili waende kupumzika. Wabaya anawaacha kwanza wale bata afu wajifunze maisha.

Lakini kuna wabaya wengine toka wana zaliwa mpaka kufa wanakula bata. Hata kifo chao kinawakuta kwenye bata.

Lakini ni mipango ya mungu. Hatuwezi jua mungu anakusudia nn kuwafanya wabaya wale bata na wazuri kuwahi kuchukuliwa. So tumuachie mungu
Ni mema yapi aliyoyafanya? Kulazimisha watu huko vujijini watoe ela wachangie uendeshaji wa miradi ya ujenzi wa mashule na mazahanati? Mema yapi ikiwa watanzania wanakosa haki na Uhuru wa kutoa maoni? Mema yapi wakati tumeshuhudia akifosi Tanzania iwe ya chama kimoja?
Tumeona ndani ya utawala wake wamepotea watu wengi, wamekufa watu wengi, watu wasiojulikana wamejitokeza ndani ya utawala wake na hakuna aliyekamatwa
Mema gani ikiwa vyombo vya habari wanalazimishwa kuripoti yanayomfurahisha yeye tu?
Mema gani ikiwa bunge limekuwa likidharaulika, amefanya manunuzi na mikataba pasipo kufuata taratibu
Katiba ikawekwa pembeni nakufuata hisia zake.
 
Hizi tabia za kukuza mambo watanzania tumezitoa wapi?Huo si ni uwanja huwa wanajaza Simba tu? dah! huo uwanja unaingiza watu 60,000 Dar ina watu zaidi ya 4,000,000 - 6,000,000 do your maths on it.

Pia Watu wengine wametoka mikoa jirani kuja kuaga,wengine wamekuja kufafanya biashara maeneo hayo,wengine vibaka wamekuja kuiba,wengine wakiona mikusanyiko hupenda kwenda huko,wengine wamekuja kumuona hayati live wapate cha kusimulia,wengine hata hawajui kwanini wapo pale uwanjani wapowapo tu.
 
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Kujitokeza kwa watu wengi vile sio kwamba wote wanakuja kwa vile wanakupenda bali wapo miongoni mwao hawakupenda utawala wake lakini leo wanaenda kumuaga kutokana na utu waliokuwa nao hasa inapotokea mtu amefariki, unaachana na yale matendo yake au chuki zako juu yake unaamia kwenye kumuonea imani kwa kifo chake. Kifo cha mtu ni ishu nyingine, mtu unaweza kuwa na uadui naye ama akakuuzi kweli kweli katika maisha yake lakini ikitokea amefariki lazima moyo wako utamuonea imani

Wanafiki bhana[emoji23]
 
Ofcoz kifo chake kimeniuma sana, bila magufuli sidhani kama ningekua mwajiriwa wa serikali tena kwa hii taasisi niliyokwepo bila connection huwezi pata kazi. Intake yetu wote tumeumia sana, Mungu amlaze mahali pepa peponi. [emoji120]
Hata mimi nimeumia,tulikuwa tumeishamzoea na tulishajitune akamilishe miaka yake 5 lkn ndio hivyo tena, poleni watz.
 
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
We sema unachuki na Lisu na alipokoswa zile risasi inaoneka uliuzunika kweli.Huo upendo unasema unaupima na nini ? au kwa kujaa uwanja wa uhuru ambao hawazidi 23,000 na dar kuna 6mln kama vipimo vyoko ndio hivyo pole sana. RIP JPM nenda salama ila huku umeacha watetezi wa ajabu.
 
Back
Top Bottom