UWATA wamesambaratisha familia yetu

UWATA wamesambaratisha familia yetu

dadake_

Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
22
Reaction score
59
Mnamo mwaka 2013 baba yangu alikutana na mchungaji mmoja huko Moshi na baba yangu akamueleza kiu yake ya kuwa karibu na Mungu kwani ujana wake hakuwa mtu wa kwenda kanisani. Mchungaji(jina limenitoka lakini ningemtaja) akamueleza habari za uwata na kwamba angemkutanisha na kiongozi wa dhehebu hilo, basi wakaanza kwenda wote faraghani na hata ilipofika wakati wa kurudi Dar(nyumbani) baba hakufika kabisa nyumbani na baada ya muda tukasikia amepatiwa mke kanisani na hivyo anafunga nae ndoa ( hakuwa anashaurika tena na tuliona walakini kwenye mental health yake, hakuwa tena kama zamani).

Ndugu zake pamoja na mama walijitahidi kuweka mapingamizi kwenye makanisa ya Dar hivyo hawakuweza kufunga ndoa hapa dar ikawalazimu ndoa ifungwe Morogoro tena wazazi fake walisimama kwa upande wa baba yangu umma ukidanganywa baba yangu wazazi wake wamefariki ilhali wako hai. Aliporudi mambo yalikuwa mabaya zaidi kwenye biashara zake mambo yakabadilika alifukuza wafanyakazi wake wote mpaka ndugu zake wa damu na kuajiri watu kutoka Uwata, alikataa malipo kwa njia ya dollar kwa kusema kwamba ni ushetani, wateja walimkimbia na kumwita kichaa! 😭 pesa alizofanikiwa kupata tunasikia amewekeza kwenye vitegauchumi vya UWATA… alipokuwa akija nyumbani kutusalimia ilimbidi aende kanisani akaungame kwa maana amefanya dhambi( huko walimbatiza mama yangu jina dellilah na kwamba yeye ni mchawi!😢) hata ilipobidi ndugu kwenda kumuona ofisini kwake ni lazima hao watu wa uwata nao wawepo hapo ofisini kusikiliza 🤦🏿.

Hali yake kiuchumi imekuwa mbaya mno waliomjua zamani na sasa wanahuzunika. Alikuwa baba, kaka, mume na mtu bora sana nitawalaumu UWATA siku zote za maisha yangu kwa kuwakosesha malezi ya baba wadogo zangu kwa maana si mapenzi tuu hata huduma hapaswi kutoa kwa watoto waliozaliwa na delila!
 
Ni tatizo la ndugu yako. Mwalimu Andongwisye ni mfuasi mzuri wa UWATA amekuwa mfuasi mzuri wa UWATA kuanzia Diploma na sasa ni DR. Tunae pia mkuu wa shule ya Masukila FUBILE ndiye mwalimu bora zaidi kyela nzima kwa kipindi kirefu sana . Ameingia kichwa kichwa huyo ushauri wangu mumuacheni endeshemni mambo yenu chini ya mama na yeye aendelee na hao watu wake. Amen
 
Angalizo: Ukishakuwa na hela tafuta ama mganga au kinga ya imani, muda wowote unakuwa target ya matapeli wa kiimani.
Utaamua imani yako uikabidhi kwa mababu wa Abrahamu au mababu wa Kiafrika.

It seems hiyo familia haina mtoto wa kiume, ingekuwa mimi ningeshafanya neutralisation fulani kwenye njia za uongo uongo anakopitishwa mzee.
 
“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”

Matapeli wengi wamejificha kwenye mgongo wa dini, pole sana.

Kuna mdada single maza wa watoto watatu, kila mtoto na baba yake, aliwafukuza watoto wake kisa kaambiwa na mchungaji kazaa na mapepo kwahiyo watoto wake nao ni mapepo. Kukosa msaada wa majirani kuita polisi wamkamate wale watoto wangekufa!!
 
“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”

Matapeli wengi wamejificha kwenye mgongo wa dini, pole sana.

Kuna mdada single maza wa watoto watatu, kila mtoto na baba yake, aliwafukuza watoto wake kisa kaambiwa na mchungaji kazaa na mapepo kwahiyo watoto wake nao ni mapepo. Kukosa msaada wa majirani kuita polisi wamkamate wale watoto wangekufa!!
Duh inasikitisha
 
Hicho chama unachokizungumzia ni WAWATA( Wanawake Wakatoliki Tanzania),, ni tofauti na UWATA( am not perfect sure ila nahisi ni Uamsho wa wakristo) kitu kama hicho
Upo sahihi kabisa, tayari nilicheki kumbe ni madhehebu na yana hadi website yao ukigoogle unawapata, aisee wabongo tuna madhehenu mengi bila shaka na Mbinguni tutaenda wengi!
 
Back
Top Bottom