Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 229
So sad, ukiongezea na ujinga wa watu wengi kushindwa kuhoji baadhi ya hizo imani kwa mfano ipo dhana moja viongozi wengi wa hizi imani huwaaminisha wafuasi wao eti kwamba kuna laana sijui mizimu ya mababu na mabibi au hata shangazi na watu engineo wa karibu inayoweza kukudhuru. Kutwa kucha wanahubiri uchonganishi kwenye nyumba za ibada.“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”
Matapeli wengi wamejificha kwenye mgongo wa dini, pole sana.
Kuna mdada single maza wa watoto watatu, kila mtoto na baba yake, aliwafukuza watoto wake kisa kaambiwa na mchungaji kazaa na mapepo kwahiyo watoto wake nao ni mapepo. Kukosa msaada wa majirani kuita polisi wamkamate wale watoto wangekufa!!
Hebu imagine Bibi yako au babu aliyemzaa mama/baba yako eti alikuwa na maroho mabaya, hivi inaingia akilini kweli? Jiulize, huyu kiongozi ni mganga au mpiga ramli? Anapata wapi ujuzi wa kutambua kuwa bibi/babu yako alikuwa na hao roho wachafu? Huoni hata na wewe wajukuu zako wakija kuaminishwa imani hizi za kishenzi hata na wewe utakuja kuitwa mchawi au mshirikina wakati huo umeshatangulia mbele za haki? Tuwe na Imani lakini vitu vingine ni lazima tuhoji kama vina ukweli wowote ama ni njia ya wajanja kuchukua sadaka