Hapa kuna uongo mwingi ndugu mtoa post. Kwanza UWATA si dhehebu bali ni kikundi cha watu wa madhehebu mbali mbali wanaojumuika pamoja kusali (fellowship). Kila mtu husali kanisani kwake. Hawafungishi ndoa wala hawabatizi, ndoa utafungisha kanisani kwako (katika madhehebu yako) ni watu wanaoheshimu dini za watu wengine na ni watii. Ni watu wasiopenda kuumiza wengine kabisa. Kujiunga na fellowship yao ni hiyari.
Wanachoamini.
1. Biblia ni NENO la Mungu. Hivyo kila ajiungae huamini hivi si kwa kulazimishwa bali kwa kujua hivyo na kuamini mwenyewe.
2. Mwanauwata anaamini kuwa YESU Kristo ni mwana wa Mungu alizaliwa, akaileta injili kwa ajili ya kumkomboa yeyote amwaminie, akasulubiwa msalabani akafa akazikwa akafufuka na yu hai sasa, naye atawahukumu wote ambao hawakumwamini na kuishi uovu.
3. Wanaamini wokovu ni kwa Yesu tu , na kuufikia ni kutubu, yaani kuungama dhambi na kuzicha. Biblia, Mithali 28:13. Azifichae dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamae na kuziacha atapata msamaha.
4. Wanaamini kuwa kuishi wokovu wa Kristo Yesu ni kuwa na amani na watu wote. BIBLIA, Webrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
5. Wanaamini kabisa kuwa familia ilianzishwa na Mungu, hivyo wao hawawezi kamwe kufusa ama kuharibu familia.
Kwa haya tu sidhani kama ndio hao au ni impersonation imefanywa na hao watu wabaya wanaojiita uwata lakini si UWATA niwafahamuo.