illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Wengi tunataka magari ya bei nafuu, hii hupelekea kujikuta tuko tayari kununua gari bila kufanya uchunguzi wa kina, baada ya kujiridhisha kuwa gari unalotaka kununua lipo katika hali inayokuridhisha, ni.
Ni muhimu kujua gari hilo liliingiaje nchini, hapa nazungumzia documents. Watumishi huwa ni rahisi kupata magari utakuta labda minadani huko walijiuzia magari, na wale wengine wanaojimilikisha magari yaliyokamatwa na kutelekezwa, na wale wenye misamaha ya kodi, unaweza kudhani kwamba sababu mtu huyu ni mtumishi basi ninaweza kumuamini, ukaishia kutoa hela zako ambazo ulitafuta kwa taabu, baada ya kulipia gari kuna hatua nyingine muhimu ambayo ni kuhamisha umiliki.
Ndipo unaweza kugundua kuwa umeuziwa gari ambalo huwezi kulimiliki, pengine kumbukumbu/taarifa zisiwepo mamlaka ya forodha (Hii ni kwa magari mengi yaliyoibiwa nchi za jirani na kutelekezwa) wakati wa kuyauza yanatengenezewa kadi ya “Haraka” ushauri unapotaka kununua gari hususani kutoka kwa kundi tajwa usiseme tu “ngoja nikamlete fundi wangu” ni Bora pia ukaenda na kadi mamlaka ya forodha kujua gari hilo liliingiaje nchini (kumbuka sisi hatuna viwanda vya magari), angalia pia liliingiaje kwa matumizi gani, pia limepita kwa wamiliki wangapi na kama jina la muuzaji ndiyo jina la mmiliki, pia kama lina msamaha wowote wa kodi. Yote haya ni ili kujiridhisha usije ukanunua gari ambalo huwezi kulimiliki.