Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!

Kakurupuka sana..hiyo makala ameshaikata na mkasi kashaimbatanisha na invoice kwenda kwa PRO wa kampuni ili alipwe kwa kuwafanyia publicity
 
Kumbe ukiacha ujinga wa kumpaka mafuta Hangaya unakuaga na akili?
 
Kakurupuka sana..hiyo makala ameshaikata na mkasi kashaimbatanisha na invoice kwenda kwa PRO wa kampuni ili alipwe kwa kuwafanyia publicity
Mkuu Mavipunda , kiukweli umenichekesha ulipozungumzia kuikata makala na mkasi na kuituma kwa PRO!. Nimecheka kwasababu zamani enzi za ujana, nilishafanyaga sana huo mchezo!. Kihabari hiyo inaitwa "newspaper clippings". Siku hizi hakuna tena hizo kitu, magazeti yote yanaanza kwa kuwa digitized, wanatoa digital copy, ndio kisha wanapeleka ku print. Hivyo digital copies za magazeti yote zipo, huna haja ya kukata , una copy tuu na kumtumia link. Mimi nasisitiza, kazi ya uandishi naifanya just for the love of it, nafanya bure, kwa kujitolea, silipwi.
P
 
Mkuu, hawa wazee wa Cold-War nimekutana nao sehemu nyingi na wengine nimefanya nao kazi. Nikiri na kusema kwamba wao ni watu ambao hawawezi kabisa kubadilika, itakuwa ni makosa makubwa kutegemea akili zao zilizochoka kutatua matatizo ya kizazi chetu. Hata sisi itafika siku tutachoka na hatutakuwa na uwezo wa kukitatulia kizazi kijacho matatizo yao. Tutawasikiliza, tutawaheshimu, tutathamini mchango wao, lakini hili la kutegemea wana-CCM na wanausalama wenye miaka 60,70 na 80 kututatulia sisi kizazi kipya matatizo yetu, IT'S A BIG NO.

Kama ulivyozungumzia mfumo mzima wa Cronyism & Patronage, waliotengeneza ni wao wenyewe. Nenda CCM, JWTZ, TISS, BoT, Foreign Affairs, MoF na taasisi nyeti nyingine utakutana na majina ambayo ushawahi yasikia. Sasa hapa utategemea jambo gani kutoka kwa watu wa namna hii kweli ??? Ifike mahali tufanye maamuzi magumu kwamba, These Old People had their chance and they blew it.......

Nchi hii ina watanzania vijana asilimia 60% nzima, uchumi wa dunia umebadilika sana, tuko kwenye mfumo wa soko huria (Free-Market). Kuendelea kutegemea mawazo ya watu ambao maisha yao yote walikuwa ni waajiriwa wa serikali ya kijamaa na chama, ilhali hawajawahi kujihusisha kabisa na kufanya biashara yoyote ile kubwa kwenye maisha yao, itakuwa ni jambo la aibu kwetu sisi wasomi wa kizazi hiki.

Mwarobaini wa kuitoa nchi hapa ilipo ni kuwang'oa hawa watu kinguvu tu,...
 
Kula tano mwanangu, bila machafuko tutaendelea kutawaliwa na hawa hawa wajamaa uchwara na familia zao. Lazima tufanye mapinduzi ili tuweke mifumo upya na kwa usahihi
 
Hawa wazee sio wa kuwatosa mkuu....bado tunaweza kuwatumia kama rejea kwa kuangalia walipokosea na wanaweza kutushauri wakati mwingine....

...ila washauri tu sio kutupangia na kutulazimisha cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…