Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!

Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!

Total kawasome vizuri hawa jamaa huko west africa na miradi yao kule Chad na Congo brazzavile... Total from france, kaisome kitu inaitwa french Africa na makampuni kama total influence yake....Moja ya project ya french Africa ni Gabon na Burkin faso..

Total amemnunua Anadarko pale Msumbiji, yuko na project kuubwa sana ya LNG....tayari RPF vijana wa PK wako pale...

Mengine magumu bwana Pasco nenda kayachimbe...
Kakurupuka sana..hiyo makala ameshaikata na mkasi kashaimbatanisha na invoice kwenda kwa PRO wa kampuni ili alipwe kwa kuwafanyia publicity
 
Umetoa mifano mingi ya kupanua bongo zetu....

Ila ni makampuni gani nguli na ya kibepari duniani yasiyo na KASHFA tofauti?!!!

Afrika tungekuwa na uwezo wa vitendea kazi na miundombinu ikiambatana na UWIANO SAWA WA KIBIASHARA tungeyachimba wenyewe madini na mafuta yetu......

Kuutafuta huo usawa 💯 p ndiko kuliko wagharimu WATAWALA WENGI WA KWANZA barani humu....

Hoja yangu si kushajiisha KUPIGA MAGOTI kwao bali tulipo ni kuhakikisha angalau TUNAFAIDIKA kwa raslimali zetu zilizopo kwa mintaarafu ya "WIN-WIN SITUATION"!!!

#SIEMPRE JMT
#NCHI KWANZA KABLA YA NAFSI ZETU🙏
Kumbe ukiacha ujinga wa kumpaka mafuta Hangaya unakuaga na akili?
 
Kakurupuka sana..hiyo makala ameshaikata na mkasi kashaimbatanisha na invoice kwenda kwa PRO wa kampuni ili alipwe kwa kuwafanyia publicity
Mkuu Mavipunda , kiukweli umenichekesha ulipozungumzia kuikata makala na mkasi na kuituma kwa PRO!. Nimecheka kwasababu zamani enzi za ujana, nilishafanyaga sana huo mchezo!. Kihabari hiyo inaitwa "newspaper clippings". Siku hizi hakuna tena hizo kitu, magazeti yote yanaanza kwa kuwa digitized, wanatoa digital copy, ndio kisha wanapeleka ku print. Hivyo digital copies za magazeti yote zipo, huna haja ya kukata , una copy tuu na kumtumia link. Mimi nasisitiza, kazi ya uandishi naifanya just for the love of it, nafanya bure, kwa kujitolea, silipwi.
P
 
paragraph ya mwisho: hawa wazee baada ya kuanguka kwa ujamaa walibaki hawana plan B pamoja na mzee mwenzao JKN....wakabaki na siasa zilezile bila kujifunza na kuelewa uelekeo mpya wa dunia, matokeo yake wamebaki na ideology ileile ya kizamani kichwani kama mji uliotekelezwa na kubakia magofu matupu...

Wazee hawa wangenifunza uelekeo mpya wa dunia na kuwekeza kwa kuwapa maarifa vijana na kuandaa succession plan kwa kizazi kipya bila shaka tusingefika huku...lack of plan and jelous wanaona wao ndio pekee wenye akili yakuliokoa hili Taifa ilihali wao ndio waliolizamisha...kifupi wanataka tutumie akili ile ile iliyofeli tujinasue kwenye tope which is very impossible..

Vijana wa sasa wanahitaji kasi ya maendeleo na sio waoga kurisk na kwenda mbele, Vijana hawa wengi huumia sana nchi yao inapoitwa masikini ilihali sio masikini na inaweza kutoka hapa..Mifumo na hawa wazee wasipokuwa makini watalipa deni kubwa ambalo madhara yake ni damu za watu...

Hatujachelewa, zianzishwe forum kila mahala kuanzia vyuoni, mitaani, mitandaoni, hawa wazee na watu wa system watoke huko walikojifungia wakae na hiki kizazi kuona namna bora ya kufanya reform kwenye mifumo na damu mpya yenye kasi, akili na mawazo mapya iweze kuingia kilingeni na kusongesha Taifa mbele, tuachane sasa na hii mifumo ya watoto wastaafu, michepuko, kamlete, UVCCM, watoto wa vigogo, turudishe Taifa kwa watanzania wote ili kila mwenye akili na uwezo atumikie Taifa hili...
Mkuu, hawa wazee wa Cold-War nimekutana nao sehemu nyingi na wengine nimefanya nao kazi. Nikiri na kusema kwamba wao ni watu ambao hawawezi kabisa kubadilika, itakuwa ni makosa makubwa kutegemea akili zao zilizochoka kutatua matatizo ya kizazi chetu. Hata sisi itafika siku tutachoka na hatutakuwa na uwezo wa kukitatulia kizazi kijacho matatizo yao. Tutawasikiliza, tutawaheshimu, tutathamini mchango wao, lakini hili la kutegemea wana-CCM na wanausalama wenye miaka 60,70 na 80 kututatulia sisi kizazi kipya matatizo yetu, IT'S A BIG NO.

Kama ulivyozungumzia mfumo mzima wa Cronyism & Patronage, waliotengeneza ni wao wenyewe. Nenda CCM, JWTZ, TISS, BoT, Foreign Affairs, MoF na taasisi nyeti nyingine utakutana na majina ambayo ushawahi yasikia. Sasa hapa utategemea jambo gani kutoka kwa watu wa namna hii kweli ??? Ifike mahali tufanye maamuzi magumu kwamba, These Old People had their chance and they blew it.......

Nchi hii ina watanzania vijana asilimia 60% nzima, uchumi wa dunia umebadilika sana, tuko kwenye mfumo wa soko huria (Free-Market). Kuendelea kutegemea mawazo ya watu ambao maisha yao yote walikuwa ni waajiriwa wa serikali ya kijamaa na chama, ilhali hawajawahi kujihusisha kabisa na kufanya biashara yoyote ile kubwa kwenye maisha yao, itakuwa ni jambo la aibu kwetu sisi wasomi wa kizazi hiki.

Mwarobaini wa kuitoa nchi hapa ilipo ni kuwang'oa hawa watu kinguvu tu,...
 
Kula tano mwanangu, bila machafuko tutaendelea kutawaliwa na hawa hawa wajamaa uchwara na familia zao. Lazima tufanye mapinduzi ili tuweke mifumo upya na kwa usahihi
u, hawa wazee wa Cold-War nimekutana nao sehemu nyingi na wengine nimefanya nao kazi. Nikiri na kusema kwamba wao ni watu ambao hawawezi kabisa kubadilika, itakuwa ni makosa makubwa kutegemea akili zao zilizochoka kutatua matatizo ya kizazi chetu. Hata sisi itafika siku tutachoka na hatutakuwa na uwezo wa kukitatulia kizazi kijacho matatizo yao. Tutawasikiliza, tutawaheshimu, tutathamini mchango wao, lakini hili la kutegemea wana-CCM na wanausalama wenye miaka 60,70 na 80 kututatulia sisi kizazi kipya matatizo yetu, IT'S A BIG NO.

Kama ulivyozungumzia mfumo mzima wa Cronyism & Patronage, waliotengeneza ni wao wenyewe. Nenda CCM, JWTZ, TISS, BoT, Foreign Affairs, MoF na taasisi nyeti nyingine utakutana na majina ambayo ushawahi yasikia. Sasa hapa utategemea jambo gani kutoka kwa watu wa namna hii kweli ??? Ifike mahali tufanye maamuzi magumu kwamba, These Old People had their chance and they blew it.......

Nchi hii ina watanzania vijana asilimia 60% nzima, uchumi wa dunia umebadilika sana, tuko kwenye mfumo wa soko huria (Free-Market). Kuendelea kutegemea mawazo ya watu ambao maisha yao yote walikuwa ni waajiriwa wa serikali ya kijamaa na chama, ilhali hawajawahi kujihusisha kabisa na kufanya biashara yoyote ile kubwa kwenye maisha yao, itakuwa ni jambo la aibu kwetu sisi wasomi wa kizazi hiki.

Mwarobaini wa kuitoa nchi hapa ilipo ni kuwang'oa hawa watu kinguvu tu,...
 
Changamoto kubwa ambayo tunayo Tanzania, ni wale wazee wajamaa wa kipindi cha Nyerere ambao binafsi huwa siwaelewi kwanini wanachukia sana wawekezaji na ukiwaambia tufanye njia gani, wao huishia kusema TUJITEGEMEE lakini hawatupi njia sahihi ya Tanzania kufanya hivyo. Kiufupi wao ndiyo waliifikisha nchi hapa na siasa zao mbovu, na bado wao wanadhani kwamba walihujumiwa na mabeberu, nothing is ever their fault....
Hawa wazee sio wa kuwatosa mkuu....bado tunaweza kuwatumia kama rejea kwa kuangalia walipokosea na wanaweza kutushauri wakati mwingine....

...ila washauri tu sio kutupangia na kutulazimisha cha kufanya.
 
Back
Top Bottom