u, hawa wazee wa Cold-War nimekutana nao sehemu nyingi na wengine nimefanya nao kazi. Nikiri na kusema kwamba wao ni watu ambao hawawezi kabisa kubadilika, itakuwa ni makosa makubwa kutegemea akili zao zilizochoka kutatua matatizo ya kizazi chetu. Hata sisi itafika siku tutachoka na hatutakuwa na uwezo wa kukitatulia kizazi kijacho matatizo yao. Tutawasikiliza, tutawaheshimu, tutathamini mchango wao, lakini hili la kutegemea wana-CCM na wanausalama wenye miaka 60,70 na 80 kututatulia sisi kizazi kipya matatizo yetu, IT'S A BIG NO.
Kama ulivyozungumzia mfumo mzima wa Cronyism & Patronage, waliotengeneza ni wao wenyewe. Nenda CCM, JWTZ, TISS, BoT, Foreign Affairs, MoF na taasisi nyeti nyingine utakutana na majina ambayo ushawahi yasikia. Sasa hapa utategemea jambo gani kutoka kwa watu wa namna hii kweli ??? Ifike mahali tufanye maamuzi magumu kwamba, These Old People had their chance and they blew it.......
Nchi hii ina watanzania vijana asilimia 60% nzima, uchumi wa dunia umebadilika sana, tuko kwenye mfumo wa soko huria (Free-Market). Kuendelea kutegemea mawazo ya watu ambao maisha yao yote walikuwa ni waajiriwa wa serikali ya kijamaa na chama, ilhali hawajawahi kujihusisha kabisa na kufanya biashara yoyote ile kubwa kwenye maisha yao, itakuwa ni jambo la aibu kwetu sisi wasomi wa kizazi hiki.
Mwarobaini wa kuitoa nchi hapa ilipo ni kuwang'oa hawa watu kinguvu tu,...