SoC02 Uwekezaji wa kumbi na maeneo ya starehe vijijini ni fursa kubwa kwa sasa na sio kilimo na ufugaji pekee

Stories of Change - 2022 Competition

Rangi ya chai

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
7
Reaction score
9
Inafahamika kuwa kilimo na ufugaji ndio fursa pekee maeneo ya vijijini. Ni kweli ni fursa kubwa asilimia 98 ya wakazi waishio vijijini wanajishughulisha na kilimo pamoja ufugaji kuendesha maisha yao.

Wanauza mazao na mifugo na kujipatia fedha nyingi wakati wa mavuno ,fedha zinakuwa ndani muda wote kwani asilimia kubwa hawana akaunti za benki .

Vijiji vingi kwa sasa hapa nchini vinaboreshwa Sana ,Kwani vingi hivi sasa vina umeme ,Barabara zinazopitika. Kupitia tarura inafanya kazi kubwa Sana kuboresha miundo mbinu ya Barabara vijijini. Mawasiliano ya simu, internet pamoja na tv (vig'amzi) mbalimbali hivi sasa vinapatikana hadi vijijini.hivyo basi mpira ,tamthilia na taarifa mbalimbali kwasasa vijijini ni kitu Cha kawaida watu wanafuatilia Sana na shangwe kama zote.

Kwa kupitia mabadiliko hayo maisha ya vijiji vingi vilivyochangamka yanashabiana na maisha ya watu waishio mijini. Kuanzia mitazamo, mavazi, vinywaji, ulaji nk

Kumekuwa na changamoto ya maeneo ya starehe na kumbi mbalimbali pamoja na huduma Bora. Watu wananywea bia kwenye matembe, huku wamekalia vigoda, ndoo hata mawe na madumu. Na wahudumu walio vaa magauni marefu na vitenge. Mziki ni mdogo na usio kuwa na ubora yani flash au memory kadi wimbo unatafutwa kwa kupelekwa mbele au nyuma inachukua dakika nyingi kupata wimbo huo. Meza fupi au kireti la soda au bia linapinduliwa kuwa meza , kuchukua kinywaji mpaka uiname Yani huwa inakera sana. Kifupi mazingira ni mabovu kupita kiasi.

Pamoja na mazingira kuwa mabovu lakini wateja ni wengi ,wanakunywa na kula katika migahawa michafu. Lakini kwa mauzo yanaweza kuwa juu hata kuliko baadhi ya migahawa na baa zilizopo mjini.

Hivyo kwasasa kumbi za starehe,migahawa standard, maeneo ya burudan ni fursa kubwa vijijini.
Ukijenga baa nzuri isiyokuwa na gharama kubwa ,weka mazingira mazuri ndan na nje, hewa Safi ,sakafu Safi isiyo na vumbi. Mziki mzuri wa laptop na kamixer kakiaina. Wahudumu wenye Kufahamu umhimu wa huduma kwa wateja. Ipambe baa yako kwa michoro na kaunta yenye kuvutia hakika utapiga hela.

Sambamba na baa weka guest house standard tu ,vyumba kitanda na runinga fulan. Weka Sakafu chini, hata ukijenga kwa tofuali za kuchoma kupunguza gharama hakika utapiga hela .

Pembeni yake weka mgahawa standard , vyakula ni vilevile Lakin wewe boresha mazingira Safi, nyama choma ,supu muda wote kwani upatikanaji wake pia sio mgumu vipo.weka viti vingi ,meza ,vitambaa vya meza ,vyombo vingi vizuri hakika utapiga hela.
Ukumbi wa mziki na mziki mkubwa walau katika wiki watu wanacheza Mara moja kwa viingilio vya kawaida tu ,2000 mpaka 3000 hakika utapiga hela.

Hivyo ukiwekeza katika vijiji kadha vilivyochangamka akasimika na kuboresha niliyo yasema hapo juu ,,basi wewe kazi yako itakuwa ni kutembelea hivyo vijiji kukusanya mapato .
NB: kama ilivyo kwa vijana wa mijini wanavyotafuta Kisha wanakwenda kutumia ndivyo ilivyo kwa vijana wa vijijini ,hivyo kinachokosekana ni hayo maeneo ya starehe kama nilivyoeleza hapo juu.

Kuhusu mzunguko wa fedha ni kweli baadhi ya vijiji huchangamka zaidi wakati wa mavuno pekee. Lakin kwa sasa inakuwa ni tofauti , vijiji vingi vinachangamka muda wote.
Kwa mfano Kijiji ninachoishi kwa sasa muda wote kipo vizuri ingawa kinakuwa vizuri zaidi wakati wa mavuno( msimu).

Wakati wa msimu hela nyingi Sana ,unaanza mwezi mach,msimu wa choroko. Kisha tunaingia katika mazao mengine kama vile mtama , mahindi na mpunga. Mwisho tunaingia katika msimu wa pamba tunakwenda mpaka septemba.

Kisha mashamba yanaanza kuandalia kwa vibarua vijana wanapata hela. Kisha msimu wa kilimo vijana wanalima vibarua vya kutosha wanapata hela nyingi na zote huishia kwenye burudani na starehe , unakaa kidogo msimu wa mauzo unagonga hodi. Achilia mbali biashara ya mifugo ambayo Haina msimu ni muda wote.

Nimalize kwa kusema KUWA " UWEKEZAJI WA MAENEO YA STAREHE NA BURUDANI VIJIJINI NI FURSA KUBWA KWA SASA.

Ukiamua kubishana na andiko hili fanya kwanza tafiti Anza na Kanda ya ziwa, fika mpaka Shinyanga ndanindani kishapu ,mwakipoya nk.
 
Upvote 3

Umesomeka Sana mkuu 🥂
 
Back
Top Bottom