Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Eneo gani Dodoma rent ni sawa na Masaki, Oysterbay, Ada Estate,Regent Estate etc.
Maeneo ya high end Dodoma, ila of course sio kwa kulinganisha na hayo maeneo uliyotaja ya Dar, hayo kwanza rents zake unakuta ni kwa dola. Kama ulikua unamaanisha maeneo hayo uliyotaja, ni sahihi kabisa!
 
Kwelinhiyo biashara mie sitakiwi fanya maana nitaweka hidden camera nione watu wanavyo kata uno
Hahaha..........ila wewe sometimes sijui unawazaga nini?

Unashangaa mbona Kila nikipita mapokezi, jamaa wananicheka kumbe camera zinaonesha kwenye show ni sekunde 15 tu inaonesha umeshawashusha Wazungu 😜
 
Ni kweli, hotel inahitaji tu location sahihi, ukipatia hapo unapiga sana hela.
Pia, hotel inahitaji capital ya kutosha pamoja na operation costs (wafanyakazi, usafi, misosi).
Kweli kabisa ukiweza hayo unapiga pesa balaa. Kuna sehemu nimeipania sema pesa ya kuwekeza ndio haijatimia. Nina mpango wa kuweka vyumba 15 tu na hapo kila chumba pesa ya chini Kwa siku ni laki 5 Kwa chumba. Hapa ninapozungumza ambayo wako kwenye maeneo hayo wameshajaza vyumba kuanzia July Hadi October
 
nachukua mawazo ya humu afu nachanganya na mawazo kutoka kwa member mmoja humu yeye anamiliki lodge kama sikosei anaitwa Grahams nione kipi kinalipa kati ya nyumba za kupangisha VS lodge
Lodge inalioa ukiweka mahali sahihi. Na usichaji pesa nyingi. Elfu 20 tu unaweza piga pesa balaa
 
Kweli kabisa ukiweza hayo unapiga pesa balaa. Kuna sehemu nimeipania sema pesa ya kuwekeza ndio haijatimia. Nina mpango wa kuweka vyumba 15 tu na hapo kila chumba pesa ya chini Kwa siku ni laki 5 Kwa chumba. Hapa ninapozungumza ambayo wako kwenye maeneo hayo wameshajaza vyumba kuanzia July Hadi October
Mkuu,mbona tshs 500,000 kwa chumba kimoja kwa siku ni ndefu sana. Inazidi rate ya chumba cha kawaida kwenye hotels eg. Hyatt Regency Kilimanjaro,Rotana,Serena etc
 
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.

Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa.

Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).

Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana.

Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).

Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).

Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili.

Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit.

Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.

View attachment 3241776View attachment 3241777
Safi, hongera sana 👏
 
Laki 5 per night?🤔
 
Mkuu,mbona tshs 500,000 kwa chumba kimoja kwa siku ni ndefu sana. Inazidi rate ya chumba cha kawaida kwenye hotels eg. Hyatt Regency Kilimanjaro,Rotana,Serena etc
Tena hiyo ni ya chini. Ukikaa vizuri u apiga Hadi 1M Kwa chumba.
 
TheCrocodile hongera sana mkuu kwa hii hatua. Umejipata. Wewe sasa umeingia daraja la Kati la uchumi wa Tanzania.

Vipi ungepiga kodi 200k kwa mwezi usingepata wapangaji?
📌Angeweka na jiko la kishkaji kwa ndani ndio habari ya mjini kwa sasa angepiga pesa,pia vitu kama umeme wa kujitegemea na maji separate meter ukimwambia mtu 200K ni reasonable kabisa.

📌Vibachelor vya skuizi havitaki kushare na umbea umbea kila kitu humohumo ndo mambo yao.

Design ya hivi👉CHUMBA MASTER,SEBULE,JIKO NA UMEME MAJI KUJITEGEMEA unakula hela NA KUPANDISHA KODI KULINGANA NA SUPPLY AND DEMAND BILA WASIWASI mpaka unasahau. Hizi design Kutoka kwenye fashion baadae sana.

Ila hongera🤝 hata humo bado unapata hela nzuri tu.

Nampango wa kuja kuzika hela huko kibaha maana mji umehamia huko kwa sasa😄😄😄
 
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.

Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa.

Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).

Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana.

Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).

Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).

Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili.

Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit.

Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.

View attachment 3241776View attachment 3241777
Hongera sana mkuu, haya ukachukue form sasa ya kwenye chama cha wapangishaji😅😅😅... Sema naona umetumia gharama kubwa sana kwenye kupaua hadi bati kutokana na aina ya mjengo uliojenga.
 
Tena hiyo ni ya chini. Ukikaa vizuri u apiga Hadi 1M Kwa chumba.
Duuuuhh!! Hapo si inabidi investiment iwe kubwa sana? Na pia iwe yale maeneo ya kishua sana ya kitalii. Na in terms of accessories inabidi ziwepo za kutosha (eg swimming pool, etc). Mtu atalipia laki 5 per night bila swimming pool kwa mfano?
 
Asante sana mkuu. Kwa 200k ingekua parefu sana. Nilivyoset hapo ndo nimeanza, si unajua kodi huwa haishuki siku zote, inapanda tu juu. Kwa survey niliyofanya ya hayo maeneo, 150k ni kiwango cha juu kabisa (matawi ya juu). Ila with time, labda wakati na review kodi mwaka unaofuata labda inaweza fika huko!
Hiyo ni standard usiharakishe kwanza maana kwa maeneo kama KIMARA,MBEZI NA GOBA KUNA NYUMBA ZINA MPAKA JIKO NA MAJI UMEME UNAJITEGEMEA NA BEI BADO IPO INACHEZEA 130K-200K.

Maliza ukuta,weka paving na vikorombwezo kadhaa uwashike hao wapangaji wakae hata mwaka.
 
📌Angeweka na jiko la kishkaji kwa ndani ndio habari ya mjini kwa sasa angepiga pesa,pia vitu kama umeme wa kujitegemea na maji separate meter ukimwambia mtu 200K ni reasinable kabisa.

📌Vibachelor vya akuizi havitaki kushare na umbea umbea kila kitu humohumo ndo mambo yao.

Design ya hivi👉CHUMBA MASTER,SEBULE,JIKO NA UMEME MAJI KUJITEGEMEA unakula hela NA KUPANDISHA KODI KULINGANA NA SUPPLY AND DEMAND BILA WASIWASI mpaka unasahau. Hiiz design Kutoka kwenye fashion baadae sana.
Nakuelewa sana. Ila kuweka na jiko niliona mambo yangekua mengi sana, na pia kwa maeneo ya Kibaha, hiyo sio demand kubwa sana.
Ila kati ya ulivyovisema hapo, vingine vyote nimeweka ukitoa hilo la JIKO (Umeme & Maji kujitegemea, chumba master, full fence, some privacy).
 
Hongera sana mkuu, haya ukachukue form sasa ya kwenye chama cha wapangishaji😅😅😅... Sema naona umetumia gharama kubwa sana kwenye kupaua hadi bati kutokana na aina ya mjengo uliojenga.
bora hivyo amepaua ya hela yote kuliko HIDDEN ROOF.Hii amepaua na kusahau ila hidden roof ikifika masika(kuvuja) kilio, ikifika kiangazi kilio(joto).😄😄😄
 
Nakuelewa sana. Ila kuweka na jiko niliona mambo yangekua mengi sana, na pia kwa maeneo ya Kibaha, hiyo sio demand kubwa sana.
Ila kati ya ulivyovisema hapo, vingine vyote nimeweka ukitoa hilo la JIKO (Umeme & Maji kujitegemea, chumba master, full fence, some privacy).
Bado utapata mkuu wala usihofu.Ila in a long run for future competition pitiapitia page za madalili wa mbezi, kimara,goba huko instagram uone aina mpya ya ujenzi wa hivi vi min- aptment🤝🤝🤝

Usisahau kibaha ndipo mji unapohamia kwa sasa hivyo DEMAND YA USASA WA KUSHINDANA NA MAENEO KAMA GOBA,MBEZI,MADALE INAHITAJIKA KUVUTIA WATEJA ZAIDI👊
 
bora hivyo amepaua ya hela yote kuliko HIDDEN ROOF.Hii amepaua na kusahau ila hidden roof ikifika masika(kuvuja) kilio ikifika kiangazi kilio(joto)😄😄😄
Ni kweli Ila kuna nyumba fulani naona zinajengwa sana Kenya kuna namna bati zinawekwa kwa nyumba za biashara inasaidia sana kwenye kupunguza gharama ingawa nahisi na zenyewe itakua zinasumbua hapo kwenye joto😅😅
 
Back
Top Bottom