Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

TheCrocodile hongera sana mkuu kwa hii hatua. Umejipata. Wewe sasa umeingia daraja la Kati la uchumi wa Tanzania.

Vipi ungepiga kodi 200k kwa mwezi usingepata wapangaji?
Asante sana mkuu. Kwa 200k ingekua parefu sana. Nilivyoset hapo ndo nimeanza, si unajua kodi huwa haishuki siku zote, inapanda tu juu. Kwa survey niliyofanya ya hayo maeneo, 150k ni kiwango cha juu kabisa (matawi ya juu). Ila with time, labda wakati na review kodi mwaka unaofuata labda inaweza fika huko!
 
Well done mkuu.....
Hapo maanayake ndani ya miaka mitano na nusu utakua umesha rudisha gharama za ujenzi, then unaanza kula faida polepole
Iwapo kutakua hamna maintenance kama mpangaji kaondoka inarudi. But hapo kuna operation cost zitakuja baada ya miaka miwili.

Pia bado anajenga ukuta. Akimaliza ataweka geti. Akimaliza wapangaji watataka paving.

So real return unakuja kuipata kuanzia miaka 8-10...
 
Hongera fanya sherehe ya uzinduzi Wana JF tuje tuserebuke na kuombea!
 
Kwa Dodoma kama maneno ya Ilazo, Kisasa ungelamba hiyo200k!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…