Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Iwapo kutakua hamna maintenance kama mpangaji kaondoka inarudi. But hapo kuna operation cost zitakuja baada ya miaka miwili.

Pia bado anajenga ukuta. Akimaliza ataweka geti. Akimaliza wapangaji watataka paving.

So real return unakuja kuipata kuanzia miaka 8-10...
Yeah mkuu, uko sahihi, mahesabu ya kwenye makaratasi na reality on ground yaweza kuwa tofauti. Lakini yote kwa yote, ni uwekezaji mzuri wa long term.
 
Hiyo biashara inalipa ila inahitaji uwe na michongo mingine watu wanashindwa kuwekeza hapo sababu yakutaka faida ya haraka binafsi nipo kwenye utekelezaji wa kuwekeza kwa style hiyo japo inabidi niwe mpole make ni mikoani ila itanilea
 
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.
Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa. Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).
Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana. Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).
Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).
Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili. Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit. Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.
Hongera mkuu. Milioni 76 kujenga units 8 ni matumizi mazuri ya pesa naona ulitumia gharama ndogo za ujenzi ni kila unit 9,500,000 ambapo ni chumba, sebule na choo. Very fair
 
Back
Top Bottom