Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Mkuu
Karibu sana mkuu.
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.
Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa. Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).
Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana. Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).
Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).
Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili. Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit. Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.

MKUU UNAONAJE UKAZIGEUZA LODGE NA CHUMBA KWA SIKU ULIPISHE ELF 30. Nawazaga lodge kuliko kupangisha kwa mwezi

Naona hii kitu ni nzuri kama ukiwa na hela zako unataka kuzichimbia, na unataka return ya muda mrefu kidogo kidogo. Demand ni kubwa sana ukipata eneo zuri. Hizi za kwangu ziligombaniwa sana, zilipata watu kabla hata sijaanza finishing, tayari zilikua full.
Najikusanya tena niangushe zingine, naona na
Sahihi 💯
 
Real estate business, it real pays hasa kwasisi wenye Ndoa na kazi za kuajiriwa maana hatuna muda mzuri wa kusimamia biashara binafsi

Binafsi naendelea kujifunza juu ya biashara nyumba hotel/airBnB

Nikiona Zinalipa, nitajaribu kufanya Mwaka ujao Mungu akinipa Uhai
Aah sasa nimekumbuka ni wewe, juzi usiku sana nilichangia uzi mmoja wa airBnB nikataka nimtag member anayependa real estate ila sijawahi ona anazungumzia airBnB. Vipi guest yako mkoani inaendeleaje, nilipendekeza uweke free breaksfast.
 
Huo Uzi sijauona Mkuu, labda niperuzi kwenye jukwaa husika

Nashukuru nilifanyia kazi yale maboresho yako, alhamdulillah biashara inaendelea vizuri

Nimeanza Ujenzi wa lodge ya pili

Mungu akipenda miezi 2 ijayo huenda nikaikamilisha

Kila la heri kwenu nyote wapambanaji 👏👏💪
 
Umeielewa vyema sana real estate mkuu!
 
Aah sasa nimekumbuka ni wewe, juzi usiku sana nilichangia uzi mmoja wa airBnB nikataka nimtag member anayependa real estate ila sijawahi ona anazungumzia airBnB. Vipi guest yako mkoani inaendeleaje, nilipendekeza uweke free breaksfast.
Huyu jamaa kaisanukia sana sekta ya real estate aisee!
 
Huo Uzi sijauona Mkuu, labda niperuzi kwenye jukwaa husika

Nashukuru nilifanyia kazi yale maboresho yako, alhamdulillah biashara inaendelea vizuri

Nimeanza Ujenzi wa lodge ya pili

Mungu akipenda miezi 2 ijayo huenda nikaikamilisha

Kila la heri kwenu nyote wapambanaji 👏👏💪
Kupambana muhimu mkuu, hadi kieleweke!
Naona business ya lodge umeilenga mkuu!
 
Kupambana muhimu mkuu, hadi kieleweke!
Naona business ya lodge umeilenga mkuu!
Hakuna kukata tamaa hadi kieleweke Mkuu 💪

Biashara ya Lodge nimetokea kuielewa sana Mkuu, na iwapo fedha zingekuwa zinapatikana ningehamia kwenye Biashara ya Hotel

Kwenye hayo maeneo, fedha ipo maana mtu halali hadi alipe Chumba 🤗
 
Huo Uzi sijauona Mkuu, labda niperuzi kwenye jukwaa husika

Nashukuru nilifanyia kazi yale maboresho yako, alhamdulillah biashara inaendelea vizuri

Nimeanza Ujenzi wa lodge ya pili

Mungu akipenda miezi 2 ijayo huenda nikaikamilisha

Kila la heri kwenu nyote wapambanaji 👏👏💪
Nimechelewa ila kama bado hujaifanya airbnb jitahidi weka uzio. Kisha weka pavements, ukoka na maua ndani bila kusahau miti ya matunda na kivuli. Weka tank la maji na emergency generator. Ungeweza zaidi weka na swiming pool. Pia samani za ndani ziwe nzuri na uweke TV kubwa, taa za kisasa nzuri. Si lazima ufanye vyote kwa pamoja ila hakikisha mwisho wa siku vyote nilivyotaja vinakuwepo, baadae Mungu akibariki unaweza jikuta ndio biashara yako hii unakuwa na apartments kadhaa.

After that una uhakika wa kupata wateja wa hela nzuri. Alafu usiseme wazungu tu, ukifanya hivyo wateja wako 90% wanakuwa wabongo wanaofanya retreat nyumbani kwao na wanaotaka faragha. Na hauitangazi airbnb peke yake hata Instagram unakuwa na wateja wengi.

All the best. Ningependa kujua ulijenga kwa gharama gani na ilikuwa mwaka gani.
Uzi wa muda ila niliona juzi nikachangia hivi
 
Real estate business, it real pays hasa kwasisi wenye Ndoa na kazi za kuajiriwa maana hatuna muda mzuri wa kusimamia biashara binafsi

Binafsi naendelea kujifunza juu ya biashara nyumba hotel/airBnB

Nikiona Zinalipa, nitajaribu kufanya Mwaka ujao Mungu akinipa Uhai
Hapo kwenye hoteli kunalipa sana ukiiuweka mahali sahihi.
 
Kuna maeneo nyumba bei rahisi yaani Kodi 250k kwa mwezi 🤣 halafu kuna watu bado wanalalamika maisha magumu...
Huku kwetu ungepanisha kwa 200k hadi 250k na hakuna angelalamika hata kidogo
 
Back
Top Bottom