Ok, hongera sana mkuu, tutakua ni majirani sana maeneo ya hapo. Hata hizi ziko maeneo ya huko huko. Hizi nimezitenganisha. Hata ukuta nitakavyojenga nitazitenganisha na kuweka ukuta katikati yake, na kutakua na mageti mawili, kila jengo na geti lake! Maeneo ya Kibaha uhitaji wa makazi ya low to middle costs ni mkubwa sana kwa sababu kuna viwanda vingi sana, na hakuna makazi yenye ubora kwa ajili ya wale wafanyakazi, wengi huwa wanahangaika kutafuta makazi mazuri. Hapo ndo nilipoona gap. Hizi nyumba zilijaa booking ya kupangishwa kabla hata hazijaisha!