Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

nachukua mawazo ya humu afu nachanganya na mawazo kutoka kwa member mmoja humu yeye anamiliki lodge kama sikosei anaitwa Grahams nione kipi kinalipa kati ya nyumba za kupangisha VS lodge
Kati ya Lodge na Nyumba za kupangisha, ni Lodge pekee ndiyo inalipa Kwa kibiashara.

Ukiweza pitia Uzi wangu, nilielezea undani wa hizo biashara Kwa kuangalia muda unaotumika katika kurejesha Mtaji utakaotumika katika uwezekezaji.

Nikipata Utulivu nitakutag uusome ule Uzi
 
Ukarabati ni kitu muhimu kwenye majengo.

Na kama unakuwa karibu na majengo yako inakuwa rahisi lutembelea mara kwa mara na yale mapungufu unayolutana nayo unayafanyia kazi kuyarekebisha.
Yes, ni kweli. Na pia ukiwa unafanya ukarabati na nyumba ikabaki vizuri, unaiongezea thamani na ni rahisi kuongeza kodi. Nyumba ikichakaa inapunguza thamani yake.
 
Eneo lifikike kwa gari hata kama ni mbali, liwe karibu na rami au utoke kabisa rami ufike, lisiwe uswahilini na vichochoroni, liwe nje ya mji kidogo sio katikati kwenye joto kali na makelele.

Otherwise basi eneo liwe sehemu expensive kama Masaki, Oysterbay na Mikocheni na hapo upangishe apartments za maghorofa na sio ujenge.
Uko njema sana mkuu!
 
Mkuu naomba kuulza mfumo wa mashimo ya choo umetumia huu wa kisasa wanaosema unapoteza maji au ule tuliouzoea wa shimo kubwa na dogo?
Nimetumia mfumo tuliouzoea siku zote mkuu wa shimo kubwa na dogo. Nilitaka kutumia huo mfumo wa kisasa, ila gharama niliona zinakua kubwa sana.
 
Hata hiyo 150k kaweka parefu, kibaha ndo kodi hiyo? Hata km. Lol
Wakati wengine wanasema ni ndogo hiyo nimeweka😆😆. Na pia zilijaa kabla ya kuisha. Although kwa maeneo ya kule ni kweli hiyo ni matawi ya juu kweli. Kodi za kule nyingi around 80k- 100k.
 
Lodge faida yake kubwa ni moja cash then service, pia hakuna usumbufu wa kuharibika vitu, kusumbuana kodi
True. Japokua lodge sasa changamoto yake kwenye gharama za uendeshaji za kila siku..... Mfano lazima uwe na wafanyakazi, pia gharama za breakfast. Na pia uinahitaji usimamizi wa karibu sana, mambo yasiharibike. Ila nakubaliana na wewe, pesa ipo!
 
Back
Top Bottom