Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

How uwepo wangu unathibitisha uwepo wa Mungu?
Swali zuri. Nakujibu kwa swali, unakubali Kuna mwanzo yaani wa kwanza katika binadamu ? Huyu wa kwanza alitokeaje mpaka ukawepo wewe ? Je alitokana pasi na chochote au alijiumba yeye mwenyewe ?
 
Nimekuelewa vizuri sanaa mkuu.. Lakini ukiingia deeply kufikiria uumbaji wa vyote zikiwemo sayari na sisi viumbe ambao ni complex(Bin adam) lazima ukose majibu.. Ndio maana tunarudi kusema God creates all things.. Pia nikija kwenye ulimwengu wa shetani ambao upo against na mambo ya mungu yaani wachawi,waganga, mapepo nk nakuja kuamini Mungu Yupo
 
Umeona ulipokuja mm sijasema issue ni FAITH versus LOGIC.... NO NO NO..
Ninachojaribu kusema ni kwamba sio kila kitu ambacho ni real kinaweza jibiwa kwa mantiki/LOGIC mfano unaamini una AKILI lakini huwezi kudhibitisha hilo, na mengine mengi....

Sasa wewe unabisha alafu tukitaka majibu kutoka kwako huna hayo majibu unaweza ukawa very right lakini pia very USELESS, infact kwa watu wenye akili hupewi seat... Ndo maana sayansi kukataa theory ya creation ikaja majibu ya BIG BANG, ni ajabu kukataa bila kuwa na majibu... Katika vitu complex watu wanataka majibu....
 
Pamoja kwamba nami ninaamini Mungu yupo lakini hoja zako ni dhaifu sana kuwabadirisha wale wasioamini uwepo wa Mungu. You need to go deep into OBSERVATION OF IT.
 
Uwongo...serikali inatumia dini kutawala watu... Jiulize kwa Nini sakata la bandari, ushoga, n.k yote yalihubiriwa makanisani na misikitini...bila dini hii nchi ni ngumu sana kumobilize watu kufata agenda fulani..
Kwanini hiyo Serikali inapinga udini?
 
Ahsante Nimekuelewa mkuu. sasa hebu niambie sisi Tunaitwa akina nani. Na Tumetokea wapi according to Science?
 
Na huyo mungu yeye alitokea wapi? Acha upuuzi wewe usikute unawatoto na unawafundisha huu upuuzi . .....tusiwe wavivu wa kufikiri, wewe uliomba kuja huku duniani? Kama unaamini kwamba kabla haujaletwa huku ulikuwa kwa mungu wako, why akuchome moto? Kwann asikupe akili ambayo ingeweza kumkubali yeye tu? Kwanini alimuumba shetani? Kwanini aliumba dunia yenye uwezekano wa kuzini kuua,kuiba,kusema uongo,kulala njaa,kuulitaja jina lake bure,kukosa heshima kwa wazazi wake? ,kuuwawa,kuua nk!!!? Yeye anatofauti gani na binadamu alietengeneza gari, ambalo halina heshima? Kwamba linaweza kukugonga wewe ulielitengeneza,linaweza kuharbika then ulipeleke geriji au haujui gereji ya binadamu ni hospitali? , cha msingi mtuambie huyo mungu alitokea wapi? Hata kama alikuepo na ataendelea kuwepo basi tujue alikuepo duniani kutokea wapi?

Kukosa chanzo chetu isiwe sababu ya kuamini tu mungu yupo.

Yaani ukachomwe moto na mungu mwenye huruma,upendo,mkweli ,na mjuaji? Kwa kosa la kuzini , na hapo haujawahi kuomba kuzaliwa, au kutoa maoni kuhusu ulimwengu kuwepo ni sahihi?
 
Kukosa majibu hakuthibitishi Mungu yupo, kukosa majibu kunathibitisha hatuna majibu tunatakiwa tuongeze uchunguzi kujua majibu ni nini.

Jibu la Mungu ni jibu la kizembe la mtu aliyekosa majibu halafu hataki kufanya kazi ya kupata majibu, anamaliza swali kwa jibu rahisi tu la Mungu.

Mungu hayupo, ukiangalia the problem of evil kimantiki, Mungu hayupo.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, shetani, wachawi, etc, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna na hauwezi kuwa na mabaya, shetani, wachawi etc?

Mungu hayupo, shetani hayupo, hizo habari za Mungu na shetani ni stories za watu tu, ukizipima kimantiki unaona hilo wazi kabisa.

Tatizo watu hawataki kuangalia hizi habari kimantiki, wanaangalia kiimani na kimapokeo tu.
 
Akili ni nini? Na unajuaje hapa kuna akili na hapa hakuna akili bila kutumia logic?

Unajua ukishasema "unaamini una akiki lakini huwezi kuthibitisha hilo" ushatumia logic hapo?
 
Ahsante Nimekuelewa mkuu. sasa hebu niambie sisi Tunaitwa akina nani. Na Tumetokea wapi according to Science?
Sisi ni watu. Kwa mujibu wa sayansi hatujaumbwa na Mungu.

Kwa zaidi, soma vitabu vya sayansi, mimi sitaki kujitoa kwenye hoja ya msingi kwamba Mungu hayupo, na hakuumba ulimwengu. Hiyo ndiyo hoja yangu.

Kuhusu tumetoka wapi, hilo ni somo refu sana ambalo mimi mwenyewe bado nasoma.

Unaweza kujua jibu fulani si sahihi, kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi.

Ninachosema ni kwamba, jibu la Mungu si sahihi, tuliondoe, tufanye elimination, tuangalie kwingine.

Naweza kujua mwanamme mwenye miaka 30 leo hawezi kuwa na mama mzazi mwenye umri wa miezi 6 leo, bila hata ya kumjua mama mzazi wa huyo mwanamme ni nani.

Mimi ninachosema ni kwamba, mama mzazi wa huyu mwanamme mwenye miaka 30 si huyu binyi mwenye umri wa miezi 6 leo. Sijasema najua mama mzazi wa huyu mwanamme ni nani.

Ninachosema ni kwamba Mungu hayupo na ulimwengu haujaumbwa na Mungu, sijasema najua ulimwengu umeanzaje.

Naweza kujua jibu fulani si sahihi, kabla hata sijajua jibu sahihi ni lipi.

Tumeelewananhapo?
 
Kwanza sahihisha maana yako ya imani. Hilo nakuachia.

Nikuthibitishie mara ngapi ? Nimekwambia kuwepo kwako wewe Kuna thibitisha ya kuwa Mungu yupo.

Kisha nikakuuliza kwako wewe uthibitisho ni nini ?
Mkuu naona tuishie apa kwa sababu nimeshakuelewa wewe ni mtu wa aina gani akuna nitakalo jifunza kutoka kwako[emoji120]
 
[emoji2957] tumeshtuka tunadanganywa sana
 
Sidhani ata kama wanasoma hizi hoja, au wanakimbilia kutoa tu majibu ya kiimani
 
Akili ni nini? Na unajuaje hapa kuna akili na hapa hakuna akili bila kutumia logic?

Unajua ukishasema "unaamini una akiki lakini huwezi kuthibitisha hilo" ushatumia logic hapo?
Sasa tumia hiyo logic kudhibitisha kama una akili...
 
Sasa tumia hiyo logic kudhibitisha kama una akili...
Akili ni nini? Wewe ndiye umeitaja akili, define akili.

Halafu, hata nikishindwa kuthibitisha nina hiyo akili, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Ninaweza kusema kuwa mimi kushindwa kufanya chochote ninachotaka kufanya ni ushahidi kwamba Mungu muweza yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo Mungu huyo, viumbe wote wangeweza kufanya yote wanayotaka, na yale ambayo yangekuwa si mazuri, Mungu angewaziba wasiyajue na kuyataka.

Hivyo, mimi kutoweza kuthibitisha chochote ninachotaka kuthibitisha ni ushahidi kwamba Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.

Unaelewa hoja yangu ni kwamba Mungu hayupo, hoja yangu si kwamba mimi nina akili?

Sasa mbona unaacha kujibu hoja yangu kwa kuthibitisha Mungu yupo, unanitaka nithibitishe akili, kitu ambacho jwanza mini sijawahi kusema nina akili, weee huja define akili ni nini, na hata nikishindwa kuthibitisha nina akili, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo, acha kuleta hoja tofauti ambazo mimi hata sizisimamii, halafu ukanipachika kwa lazima na kunitaka nizithibitishe.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Hiyo mtu hata haelewi umuhimu wa definition, ndiyo maana nimemuuliza akili ni nini kashindwa kutueleza.
😂Ila mi nachokuambia reality ni kwamba kwa educated peers atheism inakuwa kitu normal, watu wengi ni passive Muslims/christians, watu wengi Wanaona uhuni wa ma fake pastors n sheikhs.. watu Wanaona problems za evil, instruction, errors n inconsistent revelations, watu Wanaona vyote, watu ambao bado wameshika dini ni wale watu uneducated au wale walikuwa indoctrinated Sana kuamini supernatural Kama uchawi na mapepo...others most ppo as we grow tunaona flaws nyingi za dini...Watu siku hizi wanajiita Mara spiritual but not religious ndo hivyo...so critical thinking inakuwa na ushahidi wake ni huku jamii forums na peers wetu pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…