Nimecheka sana, ndio maana nikasema hivi, shida hamsomi. Aya ziko wazi mno kiasi ambacho mpaka mtu unajiuliza akili zenu zipo wapi ?Quran-2:256: There is no Compulsion in religion…. ( hakuna kulazimishana)
Quran-9:29: Fight those who do not profess the true faith (Islam) till they pay the polltax (jiziya) with the hand of humility.
Quran-9:5: Then, when the sacred months have passed, slay the idolaters wherever ye find them and take them captive, and besiege them and prepare for them each ambush….
Quran-47:4: When you meet the unbelievers in the Jihad strike off their heads….
Quran-2:191: And slay (kill) them wherever ye catch them, and turn them out from where they have turned you out such is the reward of those who suppress faith.
Quran-8: 65: O Apostle! Rouse the believers to the fight…(against) unbelievers.
Ondoa contradiction.
Kwanza nakupa faida hii kabla ya kuondoa huo unao ona ni utata. Ukitaka kujua maana ya fulani katika Qur'an, angalia aya ya kabla yake inaongelea nini, na aya ya baada yake inaongelea. Kisha fanya ujue sababu ya kushuka aya husika kadhalika Mtume aliielezea vipi aya hiyo na maswahaba zake waliielewa vipi aya husika.
Imam Shawkaniy anasema ukiona kwenye Qur'an Kuna mgongano basi ilaumu akili na elimu yako kwa kushindwa kujua maana ya hiyo.
Naam hakuna kulazimishana katika dini. Hii aya ya 256 katika sura ya pili inasomeka hivi kwa ukamilifu :
256. Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. (al-Baqarah : 256)
Ya kwamba hakuna kulazimishana au kumlazimisha mtu kuingia katika Uislamu sababu kila kitu wazi na uongofu umeshapambamuliwa.
Ama aya ya 29 katika sura ya 9, inasomeka hivi :
29. Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii. (at-Tawbah : 29)
Aya hii kadhalika Iko wazi, inaamrisha kupigana na wasio amini, sababu Hawa ni watu waovu na ni maadui wa Allah, aya hii imeshuka tayari Uislamu umeshika hatamu, na sheria inasema ili mtu asiyekuwa Muislamu abaki kwenye ardhi ya Waislamu ni aidha awe Muislamu kwa hiari yake au atoe (Jizya) kwa maana alipe Kodi.
Bado hakuna mgongano katika aya hizo zaidi ya ujinga wenu na kutokusoma. Vijana someni mambo haya mapesi sana.
Narudi kuendelea hapa nilipoishia.