Kiranga anaujua mziki wa waislamu, hana hoja za kushindana na waislamu huyo asieamini uwepo wa Mungu, mzee wa contradiction, mzee wa kukopi na paste 😁....
Kisai njoo huku sheikh
Sishindani na Waislamu.
Waislamu wameambiwa kuna watu fulani wasibishane nao, kwani Allah kashawafanya mioyo yao iwe mizito, kawaziba macho na masikio, na atawapa adhabu kali.
Waislamu wanajua kwamba hawatakiwi kujibizana nami. Atakayejibizana nami hata Uislamu haujui.
Ndiyo maana huwezi kukuta nabishana na Mzee Mohammed Said kuhusu haya mambo. Mzee Mohammed Said anaujua Uislamu na hawezi kubishana na mimi.
Ni nyie vifulambute tu msiosoma hata hiyo Quran mnaojishaua hapa.
Unataka kubishana na mtu wakati Quran ishakukataza. Kitabu chako mwenyewe cha dini hukijui, una ki contradict.
Namulika ujinga kwa mwanga wa ujuzi.
Huyo Kisai nimemtoa ignore list kwa ombi maalum, kaja anakataa mantiki, anakataa sayansi.
Nikamwambia hivi, basi usitumoe mantiki ya lugha wala teknolojia ya kisayansi ya JF na internet.
Tumia njia zako zisizotumia sayansi ya JF na internet au mantiki ya alphabet na lugha kuwakilisha mada zako.
Nikamrudisha ignore list.
Na wewe ukishadadia mashindano ya ligi na wajinga wanaokataa mantiki kwa style ya "Baniani mbaya, kiatu chake dawa" inayoonesha hujui kufikiri, na hujafikia viwango vya kujadiliana nami, nitakupeleka ignore list vilevile.
Sina tatizo kumpeleka mtu yeyote ignore list ili kuondoa mizozano ya kijinga isiyo na tija na iliyo chini ya viwango.