Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Mwambie awaokoe watoto, akina mama na watu wote wa gaza.
Just imagine, Watoto wasio na hatia yeyote ile wala ufahamu wowote ule wanakufa kwa vita na majanga ya asili mbalimbali yaliyopo duniani.

Halafu una ambiwa, Mungu ni mwema sana mwenye huruma na upendo na huokoa watu kwenye shida na vita.

Maelfu ya watoto wamekufa huko Gaza lakini Mungu anaye daiwa ni mwema, mwenye huruma na upendo AMESHINDWA KUWA OKOA watoto hawa...

Yani kama huyo Mungu yupo ni mkatili sana na Muuaji mkubwa sana.

Murderer God.
 
Haya maandiko yana tofauti gani na vitabu vya hadithi?

Hapo hujathibitisha uwepo wa Mungu, umeleta tu hadithi za kufikirika.
 
Kiufupi tu binadamu ndio kamuumba Mungu na kumfanya awe mkuu ,ni yupo kichwani tu kwa mhusika.
 
Usimfundishe Mungu namna anavyowalinda watu wake, halafu wewe, sio ya kwamba Mungu hajaumba watu wema ni wewe uchague kuwa mwema au kubaki kama wewe ulivyo, nyie watu wa sampuli yako ndiyo mnasababisha maafa kama haya
 
Wewe tuambie au tuonyeshe ulazima wa Mungu kuumbwa.

Je unajua nini maana ya Mungu ? Yaani yule aliye umba ambaye ni mkamilifu vipi awe ameumbwa ?

Unaamini infinity ina exist ?
Mungu kaumbwa na fikra za watu baada ya kujiuliza maswali wanayoshindwa kuyajibu , ndio maana kila jamii ina fikra za Mungu kwa mitazamo tofauti.
 
Kama Mungu yupo na alitaka tusimkufuru, Aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kumkufuru?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote pasipo kumkufuru?
إنا هدينه السبل إما شاكرا وإما كفور
Kwa yakini sisi tumemuelekeza njia IMA awe mwenye kushukuru na IMA awe mwenye kukufuru

##chaguo ni lako##
 
Mungu yupo ndani ya kichwa cha muamini ndio , mwamba yupo sahihi.
 
Mithali 5:5

mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia
 
Mithali 5:7

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
 
Mithali 5:10

Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali
 
Mithali 5:15


15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.

16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…