Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Just imagine, Watoto wasio na hatia yeyote ile wala ufahamu wowote ule wanakufa kwa vita na majanga ya asili mbalimbali yaliyopo duniani.

Halafu una ambiwa, Mungu ni mwema sana mwenye huruma na upendo na huokoa watu kwenye shida na vita.

Maelfu ya watoto wamekufa huko Gaza lakini Mungu anaye daiwa ni mwema, mwenye huruma na upendo AMESHINDWA KUWA OKOA watoto hawa...

Yani kama huyo Mungu yupo ni mkatili sana na Muuaji mkubwa sana.

Murderer God. View attachment 2835493
Hao wauwaji ndo wameleta vitabu na kuaminisha watu kwamba wao ni taifa teule, mala Mungu wao ni Mungu wa dunia nzima na propaganda kibao za dini.

Cha kufanya ni kuachana na huo utapeli wao wa dini zao.
 
Imagine Vita ya Gaza,
Kuna watu wanajitoa muhanga ili wakafe na watu wengine kisa pepo .

Na wengine wanafanya mauaji Kwa kisingizio ardhi wamepewa na mungu, mungu Gani mwenye upendeleo wa kuwapa ardhi watu Fulani Tu,

Je SS wa tz 🇹🇿 mbona ardhi tumeipigania ss wenyewe, bila mungu kutusaidia

Mbona mungu analeta majanga kwa viumbe wake aliowaumba, badala ya kuleta Amani duniani
 
Kuna jambo limenisukuma sana kuandika huu Uzi.
Mambo ambayo yanaendelea kuhusu uwepo wa mungu.
Kuna baadhi ya watu wa amini hakuna mungu nk.

Ni ingie kwenye point
Uwepo wa mungu una dhihirika kwa alama zake na viumbe vyake.

Hebu tutafakari kama hakuna mungu nani alieumba bahari, jua, mbingu, binadamu, wanyama hivi vitu vimetokea vipi kama hakuna alieviimba.

Leo hii hata ukimchukuwa mtoto mdogo wa miaka mitatu ukamuuliza nani kaumba mbingu atakujibu mungu.

Vipi mtu mzima mwenye akili timamu unashindwa kutambua hilo.

Yapo mambo mengi sana yana thibitisha uwepo wa mungu naweza kesha kuelezea kiufupi, Tufahamu mungu yupo na yeye ndo ametuumba sisi ili tumuabudu yeye tu.
Malumbano juu ya uwepo wa Mungu hayapo kwenye hoja yupo au hayupo, bali kwenye yukoje na lengo lake ni lipi! Mfano, wengine wanasema Yesu Kristo ni Mungu, wengine kama wewe kuwa lengo la Mungu ni kuabudiwa.
 
Hutumii akili wewe, Mungu muumbaji anawezaje kuumbwa......hapo ndo mnapokwamia na huyo mwenzenu kiranga.
Una thibitisha vipi Mungu ni muumbaji?

Au ni kwa vile maandiko yako ya kidini yame kuaminisha hivyo?

Niki andika kitabu kika aminiwa na watu wengi kwamba Infropreneur ni muumbaji wa dunia utakubali kwamba Infropreneur ni muumbaji wa dunia?

Kwa vile imeandikwa hivyo na kuaminiwa tu hivyo?
 
إنا هدينه السبل إما شاكرا وإما كفور
Kwa yakini sisi tumemuelekeza njia IMA awe mwenye kushukuru na IMA awe mwenye kukufuru

##chaguo ni lako##
Sasa Allah huyo, ana elekeza watu njia IMA tuwe wenye kushukuru IMA wenye kukufuru (kama ilivyo andikwa kwenye hiyo Quran yenu)

Yani una machaguo mawili uliyopewa na Allah huyo kwa maagizo yake mwenyewe kulingana na Quran yake, Kwamba unaweza kushukuru au kukufuru

Halafu Allah huyohuyo akikufuriwa mnasema ni dhambi au kosa?

Hivi huyo Allah anajielewa kweli?

Wakati anaweka chaguo la kuweza kukufuriwa, Alikuwa hajui kwamba hapaswi kukufuriwa?
 
Kama mambo yangefanyika kwa Abracadabra dunia / ecosystem / nature isingekuwa this mechanical.., Yaani An entity of love itengeneze kitu ambacho sio efficiency 100% kinahitaji kuua vingine ili chenyewe kiweze kuishi ? Yaani Law of the fishes governing this so called harmonious system ? Yaani tunakuwa governed na Matsya Nyaya ?
 
Kwanini kumekua na wimbi kubwa sana mnaekosoa uwepo wa Mungu au kudhihaki Mungu sio chochote? Uzuri Mungu sio mwingi wa hasira kama binadamu bali huchukizwa na yule asienenda kwa nyia zilizo nyofu,tuamini ipo siku hakika atajidhihirisha kwenu ili mumfahamu ya kuwa yeye yupo na anawezo wa kufanya lolote, wakati wowote na kwa vile inavyompendeza.

Unaweza kuprove sio mwepesi wa hasira? Unaweza vipi kupima hasira yake na kusema kwa kiasi hiki sio mwepesi wa hasira?
 
Hapo ndipo tatizo lilipo.

Hujui habari nyingi sana zilizoandikwa Kiingereza na mimi siko hapa kukufunza Kiingereza.

Kama hujui Kiingereza sina hata haja ya kuendelea kujibizana nawe, kwa sababu kuna mengi sana utanipa kazi ya kukutafsiria na sina muda huo.

Wewe kutojua Kiingereza ni ushahidi kwamba Mungu hayupo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, asingekupa umasikini wa kutojua lugha yoyote iliyopo duniani.

[emoji23][emoji23]
 
Imagine Vita ya Gaza,
Kuna watu wanajitoa muhanga ili wakafe na watu wengine kisa pepo .

Na wengine wanafanya mauaji Kwa kisingizio ardhi wamepewa na mungu, mungu Gani mwenye upendeleo wa kuwapa ardhi watu Fulani Tu,

Je SS wa tz [emoji1241] mbona ardhi tumeipigania ss wenyewe, bila mungu kutusaidia

Mbona mungu analeta majanga kwa viumbe wake aliowaumba, badala ya kuleta Amani duniani
Tena ardhi ya Tanzania ina thamani mara elfu kuliko kile kipande cha jagwa pale mashariki ya kati.
 
Sasa Allah huyo, ana elekeza watu njia IMA tuwe wenye kushukuru IMA wenye kukufuru (kama ilivyo andikwa kwenye hiyo Quran yenu)

Yani una machaguo mawili uliyopewa na Allah huyo kwa maagizo yake mwenyewe kulingana na Quran yake, Kwamba unaweza kushukuru au kukufuru

Halafu Allah huyohuyo akikufuriwa mnasema ni dhambi au kosa?

Hivi huyo Allah anajielewa kweli?

Wakati anaweka chaguo la kuweza kukufuriwa, Alikuwa hajui kwamba hapaswi kukufuriwa?
Yani ni sawa na baba aweke mtego kwa wanae wa chupa ya chai wasivunje , huku alishapanga na kujua atakae vunja , na kuja kumwadhibu atakae vunja, wakati alishapanga wa kuvunja na kujua atakae vunja .
 
Tena adhri ya Tanzania ina thamani mara elfu kuliko kile kipande cha jagwa pale mashariki ya kati.
Kuna, Bible kwenye kurasa za nyuma kuna mpaka Ramani ya Nchi ya ahadi, eti mungu kawachorea Wana wa Israel Ramani ya inchi aliyo wahidi,

Ukweli Israel imejipigia promotion Sana kwenye Bible.

SEMA watu ni waoga kufikiri nje ya box
 
Hawa watu sijui hawa elewagi?

Dini zimepumbaza Akili zao.
Sio rahisi mkuu , ila wakifikiri vizuri hujikuta wanakua na mgogoro wa nafsi kwa sababu kuna vitu ata mtoto mdogo anaelewa tu .

Sema shida inakuja pale mtu kajengwa hivyo toka mtoto kwa vitisho na ahadi kibao .

Wengi wanaogopa kwa sababu wakifa wanahisi kuna adhabu na maisha tena .
 
Una thibitisha vipi Mungu ni muumbaji?

Au ni kwa vile maandiko yako ya kidini yame kuaminisha hivyo?

Niki andika kitabu kika aminiwa na watu wengi kwamba Infropreneur ni muumbaji wa dunia utakubali kwamba Infropreneur ni muumbaji wa dunia?

Kwa vile imeandikwa hivyo na kuaminiwa tu hivyo?
Andika tuone kama utaaminiwa.
 
Usimfundishe Mungu namna anavyowalinda watu wake, halafu wewe, sio ya kwamba Mungu hajaumba watu wema ni wewe uchague kuwa mwema au kubaki kama wewe ulivyo, nyie watu wa sampuli yako ndiyo mnasababisha maafa kama haya
Kwa hiyo sisi Atheists ndio tuna sababisha vita?

 Hivi wewe unafikiri sawasawa kweli ?

Vita vingi vimepiganwa na vinapiganwa kwa kigezo eti kueneza neno la Mungu?

Angalia magaidi ya Islamic state,
Al-Qeida, Al-shabaab, Boko Haram n.k yakipigana vita wanapayuka payuka Allah Akbar! Allah Akbar! Allah Akbar! Kwa kigezo kwamba wana mpigania Mungu (Allah) kupata thawabu....

Hivi huyo Mungu neno lake lina enezwa kwa vita?

Halafu ndio mnadai Mungu huyo ni mwema mwenye upendo na huruma?

Wanao ongoza kusababisha maafa ni watu wanao mwamini huyo Mungu.

Kibwetere wa Uganda alichoma waumini wake wakamwone huyo Mungu, Paul Makenzie yule mchungaji wa Kenya kaua maelfu ya watu msituni shakahola kwa kuwashindisha njaa waumini wapumbavu wafia dini wakamwone Yesu...!!!!

Hivi kwa mifano hiyo tu, kati ya sisi Atheists na nyie wafia dini na Mungu wenu huyo nani ana ongoza kusababisha maafa makubwa?

Leta uthibitisho wowote ule au takwimu zikionyesha kwamba tusio mwamini Mungu tumeleta maafa.

Skia wewe, Atheists ni watu peace sana, free thinkers na tuna uwezo mkubwa sana wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom