Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Katika vifungu vilivyozitaja hizo bandari yametumika maneno ya kingereza 'will' yasiyoonyesha kwamba ni ulazima wa kufanyika kwa jambo husika.Bandari za Kigoma, (ziwa Tangaynyika) Mwanza (ziwa Victoria/Nyanza), Ruvuma (ziwa Nyansa) zote hizo zimo ila zimetajwa kwa tafsida (bandari zilizoko kwenye bahari na maziwa yote)
Wanachukua asilimia nane tu ya eneo zima la bandari, mengineyo yote tumeachiwa sisi wajuaji wa kitanzania.
Kuna maeneo mengi tu tunayolalamika kuwa yatachukuliwa na mwekezaji wakati hatuna uwezo wa kuyaendeleza sisi wenyewe, eneo la majahazi limekaa tu na uendeshaji ule ule wa kizamani.
Haraka sana tunakimbilia akili za kichoyo kwamba wanyama wetu wanaibiwa, ardhi yetu inaibiwa wakati sisi wenyewe aidha ni mafisadi wakubwa au hatuna ubunifu wowote wa kuendeleza utajiri tunaopewa na Mungu.