Hahaha mkuu usinitafutie ugomvi na
Mnafiki Wa Kujitegemea
Hapana mkuu,ni muhimu kujadili suala la maendeleo ya watu kijamii,kiuchumi na kiutamaduni pasipo kuhusisha dini.
Kuhusu uwekezaji wa Dubai Ports World kwenye bandari yetu/zetu shida si muwekezaji,bali shida ni aina ya mkataba ulivyokuwa/ulivyo.
Sijauona huo unaotajwa kufanyiwa marekebisho lkn km umefanyiwa marekebisho ni jambo jema kwani kwa ninavyosikia kwa sasa ni wazi kwamba jamaa wamepewa miaka 30,ni ktk bandari moja tu na tathimini itakuwa ikifanyika kila baada ya miaka mi 5.
Sasa km hayo marekebisho yamefanyika na ninyi hamkupenda iwe hivyo basi ni maono yenu km ambavyo sisi Watanganyika tulio wengi tulitamani iwe hivyo.
Si hivyo tu,mimi ni Msabato kwa imani lkn siwezi kukubaliana na unyanyasaji ambao wamekuwa wakifanyiwa watu wa Palestine na kwingineko duniani kwa kigezo cha imani za kidini.
Ni upumbavu wa kiwango cha juu sana mimi kuwaunga mkono Israel eti kwa sababu ya vivutio vya utalii wao huku wakitulaghai kuwa ndiko alikozaliwa,zikwa Yesu.
Si hivyo tu,hata vile vivutio vya utalii kule Maka na Madina ambako watu kwa kulazimishwa wanapeleka kokoto eti wanaambiwa kuwa ni kumrushia jiwe shetani,wanatoa fedha nyingi na kuambulia jina eti El Hadji.
Simo ndani ya upuuzi wa dini mimi,ninacho kujua mimi dini ni taasisi za kifedha zenye mifumo ya unyinyaji,hivyo huwa ninaenda ili tufahamiane na kuimarisha upendo kati yetu na jirani zetu.